Rais Magufuli tusaidie wanakyela

Rais Magufuli tusaidie wanakyela

Joined
Sep 29, 2018
Posts
45
Reaction score
18
Muheshimiwa Raisi tumeanzishiwa ushirika na tunalazimishwa kushiriki. Tangu tuanze kupeleka zao letu la kakao hatujawahi kamilishiwa malipo, kwamuda huu ndo tunakopwa kabisa, Tusaidie Rais wetu.

Tukilalamika tunaitwa NJEMKE yaani sio wakulima bali wafanyabiashara wadogo kitu ambacho sio kweli bali hatuna pakusemea maana wanasema serikali ndo imeamua kuanzishwa kwa ushirika.

Bibi yangu mjane miaka 80+ akiwa na wajukuu wa marehemu watoto zake anategemea kakao kwa maisha yake ya kila siku leo hii anakaa wiki mbili bilakupata pesa maana kakao zake hazilipwi na anategemea kakao kuendesha maisha yake.

Tusaidia wanakyela muheshimiwa
 
Poleni wanakyela, Rais atakua amesikia kilio chenu. Vp kuhusu Rungwe na Busokelo nako kunakokoa je hakuna ushirika huko?
 
Mwakyembe kaenda wapi tena?
Mwakyembe yupo Dar es salaam. Ndio walioleta ushirika sidhani kama atakua na msaada tena kwa watu wake maana wao waliangalia faida tu bila kuangalia negative impact kwa mtu wa kyela. Hali mbaya kwa mkulima kipindi hiki hatujui hata tufanyaje,
 
Poleni wanaKyela, Raisi atakua amesikia kilio chenu. Vp kuhusu Rungwe na Busokelo nako kunakokoa je hakuna ushirika huko?
Hiki nikilio cha wakulima wa wilaya zote tatu, kyela Busokelo na Rungwe, Kila mkulima analia kivyake. Tunaamini ni muheshimiwa Raisi ambaye atatatua tatizo hili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom