Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,291
- 2,466
Msichoke kusoma.
Kwa kasi uliyoanza nayo, wenye weledi wa uchambuzi wanaona unakoelekea siko. Wanatamani kwanza kama ungekaa na jopo la wataalam na kutengeneza Dira ya Taifa ndipo wewe na timu yako muweze kupita humo kwenye dira, tofauti na sasa ambapo kila mteule wako anakuja na dira yake. Mwisho wa siku tutakuwa Taifa la vidira vilivyoambatana kama viraka kwenye vazi. Kwa kuweka dira ndipo unaweza kusema sasa unaitafuta na kuitimiza ile ndoto yako uliyokuwa ukiipigia chepuo, ya ‘Tanzania ya Magufuli’
Binafsi ningependa kuangazia mambo mawili ambayo kwa namna yake yameweza kuchambuliwa na wadau wengine. Nami kwa upande wangu nikaona si mbaya kuweka yangu. Jambo la kwanza ni upande wa siasa na upinzani wa kisiasa. Jambo la pili ni vijana na changamoto zao, hasa kauli yako ya pool table… Kwa kuanza na la siasa, ni wazi kuwa kile kinachoendelea katika siasa za Tanzania kwa sasa kwa asilimia kubwa kina Baraka zako. Umebairki siasa za utengano. Si lazima uwe Mwenyekiti wa chama chenu ili kuchukua hatua kutokomeza kadhia hizi za kisiasa zinazoendelea Bara na Zanzibar. Unawachukia viongozi wa upinzani kama vile wameua. Sidhani kama umesahau kipindi kile cha kampeni ulisafiria kauli mbiu zao kama vile kauli ya Mabadiliko. Ukadiriki kubadili M4C (Movement for Change) ya CHADEMA na kuiita M4C-Magufuli for Change. Ukaomba kura toka kwa wanachama wa vyama vyote na ukaahidi kuwatumikia sawa. Wako wanachama wa vyama pinzani kwa mahaba na ushawishi wako waliamua kukupa kura wewe (na si chama). Ukijua fika kuwa chama hakiuziki wala hamkutaka kutumia kauli kama iliyotumika mwaka 2005 wakati wa uchaguzi mkuu ya CHAGUA CCM. 2015 mkaona hapa mtu kwanza chama baadaye, mkaja na kauli ya CHAGUA MAGUFULI.
Iweje leo tena chama kiwe kitamu kuliko watanzania? Karibia nusu ya watanzania ni wapinzani. Hilo lilijidhihirisha kwenye uchaguzi mkuu uliopita. Si Bara, si visiwani. Kama wapinzani ndio wamekuwa chachu ya ccm kutaka kufanya mabadiliko ya kweli, kwa nini kuwachukia hivyo viongozi wa upinzani? Ilishafika hatua hata viongozi wa upinzani wakaanza kukukubali, lakini sasa hata ufanye jema kiasi gani, kama huwakubali wapinzani kuwa ni sehemu muhimu ya maisha na siasa za kitanzania, kamwe hawatakukubali nao. Kauli kama vile upinzani utakufa Tanzania si sahihi. Ukiritimba hauna tija. Katika ukiritimba kuna ubabe na maamuzi ya pupa kwa kuwa hakuna ushindani. Hakuna demokrasia. Demokrasia inayohubiriwa Tanzania iko ndani ya chama tawala tu, kwamba viongozi wan chi watoke ndani ya chama kimoja. Hakuna rukhsa ya upinzani kushika Dola. Ndio tunayoona leo Zanzibar na hapa Dar es salaam. Hadi leo uchaguai wa Meya wa jiji ni kizungumkuti, na yote hii ni chuki tu dhidi ya upinzani. Viongozi wa upinzani wana wafuasi ambao ni wapiga kura wao. Leo hii wakiona kiongozi wan chi anawaburuza viongozi wao kuna kitu kinajengeka mioyoni mwao.
Pamoja na figisu zile za uchaguzi mkuu uliopita na hatimaye kuibuka kidedea, sasa wewe ni Baba wa watanzania wote; Bara na visiwani, wapinzani kwa wana ccm. Kauli ya kusema kwamba wanao washibe kwanza ndipo utazame kwingine inatoka wapi? Wewe si baba wa wote? Leo Mungu akiibuka na kusema siwatambui nyie mataifa mengine, nawatambua Israel tu, patatosha? Kasi uliyo nayo inatokana na kasi ya upinzani nchini. Anayejisifia mbio asijisahau. Amsifie na anayemkimbiza.
Kuhusu vijana na kauli uliyotoa wakati unawaapisha wakuu wa mikoa ni wazi kwamba nayo imeleta mkanganyiko tena. Kwamba vijana wasicheze pool table wakafanye kazi. Na wakionekana wanazurura wakamatwe wapelekwe kwenye kamambi ya kilimo. Nakumbuka imeshapita miaka kama sita hivi tukiwa tunajadili jambo kama hili la vijana kujazana mijini na kufanya umachinga. Rafiki yangu akasema inatakiwa hao vijana wakamatwe wapelekwe kwenye makambi ya kulima, washonewe na sare kabisa…! Hakuna kijana anayependa kushinda akicheza pool table. Kwanza nitoe ufafanuzi hapa. Mheshimiwa itakuwa ulitolea tu mfano wa pool table, tena mida ya kazi. Bila shaka baada ya kazi ni ruksa kucheza pool table. Pamoja na mambo mengine, pool table ni ajiira za watu. Watu wamewekeza humo. Pengine hapo lilopo pool table kuna biashsra zingine zinaendelea, kama mama lishe, uuzaji wa vinywaji baridi, n.k. Na hao wauzaji ndio wachezaji. Ila sio big issue.
Big issue hapa ni kwamba Mh. Hukutazama upande wa pili. Sasa hivi kuna haya makampuni ya kubet. Yapo mengi sana hapa nchini na yana vituo vingi sana kama sheli za mafuta. Tageti yao ni vijana, hao hao wanaokatazwa kucheza pool table muda wa kazi. Haya makampuni yanaendesha kamari za michezo yote unayoijua, kuanzia soka hadi ngumi. Maduka haya ya kubeti yamefunguliwa sehemu ambazo kuna vijana wengi kama vile sokoni, vituoni, kwenye njia kuu, n.k. Asilimia 98 ya wanaobet ni vijana na wanabet kuanzia saa mbili asubuhi hadi usiku wa manane. Tumaini lao lipo kwenye kamari. Hawa vijana hawazalishi, na kama wanazalisha ni kidogo. Wanawatengenezea hawa wenye kamari hela ndefu sana. Kwa kuwa haya ni makampuni makubwa ndio kusema waachwe waendelee kumega akili na nguvu za vijana hawa ambao wameshalemazwa na kamari? Yani hiyo pool table ni cha mdoli. Mambo iko kwenye kubet. Na sasa wanajitangaza kwenye tv wakiwaeleza wateja wao wanaongeza vituo vya kubeti kwenye makazi yao. Niliona niliseme hili.
Suala la ajira kwa vijana ni tatizo, na kila mtu anaelewa. Suluhisho ni kilimo, ufugaji na viwanda kuliko huu uchuuzi wa sasa unaoendelea. Inaumiza kukutana na vijana wakiwa katikati ya jua kali la saa nane mchana wakiwa wabebeba maboksi ya vinywaji baridi njiani wakikimbizana katikati ya madaladala kuuza maji. Ukiacha hao wapo wanaotembeza mitumba, vyombo, n.k. Siku nzima yuko njiani. Hawa wasaidiwe. Na kuwasaidia ni kuboresha miundombinu (barabara, reli, madaraja, viwanja vya ndege, mashule, hospitali, masoko, umeme, maji, n.k.) vijijini ambako wengi wametoka. Ukifika Kariakoo kuna vijana wengi zana toka mikoani ambao wanafanya kazi za kidhalilishaji tu. Vijijini hakuna tena tegemeo. Warudishwe huko ila si kwa kulazimishwa bali kuwekewa vivutio. Hao ni kwa wale waliokimbia umande.
Kuna hili kundi la wasomi ambalo lipo katika hali ngumu zaidi. Bora huyo aliyekimbia umande ataosha hata magari na hakuna atakayemshangaa. Wasomi wengi wamebanwa katika kona ambayo kilio chao ni wao na Mungu wao. Mwanafunzi anapoingia chuoni anaambiwa yeye ni “Krimu ya Taifa”. Hii nimeisikia wakati wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa UDSM wanakaribishwa rasmi. Unapomwambia hivyo mwanafunzi tayari umemjengea tabaka, kwamba mi si kama wale. Mwanafunzi anasoma wee kisha anamaliza na anaingia kwenye soko la ajira. Bahati mbaya sana huyu msomi kaandaliwa kinadharia na kaandaliwa kuajiriwa. Huko ndiko anakutana na uhalisia, kwamba ajira zenyewe ni kasheshe, na zikiwepo ni za kujuana. Kwa hiyo unakuta vyuo nchini vinazalisha wahitimi mathalani 6000. Wanaofanikiwa kuajiriwa ni 1000. 5000 wanarabda mitaani. Fanya hivyo kwa miaka mitano.
Mwanafunzi huyu baada ya kukosa ajira kwa muda mrefu huku akiwa na elimu yake ya nadharia anaanza kutafuta namna ya kujiajiri. Anatumia nadharia zile kujiingiza kwenye ujasiriamali na kutengeneza michanganuo ya kibiashara kwa ajili ya kuombea fedha maana yeye mwenyewe hana! Hakopesheki! Hana dhamana! Anafanikiwa kutengeneza michanganuo yake na kuiwasilisha kwenye taasisi husika. Napo huko dana dana zinaanza tena mpaka msomi huyu anachoka. Akitazama ana elimu na hawezi kufanya ‘kazi za kishenzi’. Akitaka kazi za maana hazipati. Anabaki kati na kuanza kuchanganyikiwa. Ukweli kwa sasa taifa hili lina wasomi wengi sana wenye stress za maisha na hawajui wafanye nini. Nakumbuka Mwalimu wangu mmoja pale UDSM wakati anatufundisha alisema, na sijui kama wenzangu bado wanakumbuka. Mwalimu alisema, hakuna tofauti yoyote ya wewe mwenye digrii na asiye nayo. Tofauti moja ni kuwa wewe katika kuongea na kutenda una reference zaidi kwenye vitabu.
Mheshimiwa kwa kuyapitia haya, nikielewa unayafahamu, waangalie/tuangalie vijana, wasomi kwa wasiosoma ili kila mmoja apate stahili yake. Hii vurumisha ina hatima mbaya. Hata kukimbizana na machangudoa kwa sasa haina tija. Pengine uchangudoa sio uraibu/addiction kiasi cha mtu kushindwa kuacha. Vijana wapatiwe nyenzo tu na maisha yatkuwa mazuri. Leo ukiwatimua machangudoa mitaani, wana simu za kisasa. Biashara inaendelea kwenye mitandao ya simu. Utakagua simu ya mtu?
Kwa Tanzania yenye neema, Tanzania ya Magufuli, Tanzania ya watanzania wote, DIRA ya Taifa ni muhimu. Asanteni kwa kusoma. Mungu ibariki Tanzania.