Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Rais Magufuli akiwa anaendelea na ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa amzindua kiwanda cha vinywaji cha Jambo Food Product kilichojengwa mkoani Shinyanga.
Rais Magufuli: Serikali yangu haitayafumbia macho magazeti yanayoandika habari za uchochezi. Haswa magazeti mawili.
Rais Magufuli: Uchaguzi umekwisha sasa watu wachape kazi na mimi kama rais wenu nitaendelea kuilinda amani iliyopo.
Rais Magufuli: Vyombo vya habari vingine vinaandika habari vizuri isipokuwa magazeti mawili mabayo yamekuwa yakiandika habari kwa kuzigeuza kinyume na ukweli.
Rais Magufuli: Kiwanda hiki kitawaajili watu wote wenye chama na wasio na chama, hapa wapo hata watu wa Ujerumani.
Rais Magufuli amalizia hafla hiyo kwa kugawa vinywaji vinavyozalishwa na kiwanda hicho kwa wananchi waliohudhuria hafla hiyo.
========
Rais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 13 Januari, 2017 ameyaonya magazeti mawili yanayoandika habari za uchochezi na kupotosha wananchi kwa kuwa vinahatarisha amani ya nchini.
Rais Magufuli ametoa onyo hilo wakati akikagua na kufungua Kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji baridi mkoani Shinyanga.
Rais Magufuli amesema Serikali haitayavumilia magazeti hayo mawili kwa kuandika habari za uchochezi ambazo zinaweza kuhatarisha amani ya nchi kama ilivyotokea katika nchini ya Rwanda na kupelekea mauaji ya kimbari nchini humo.
''Serikali ya kutumbua majipu haiwezi kuacha kutumbua magazeti yanayofanya mambo ya uchochezi hatuwezi kuiacha Tanzania ikawa dampo la eneo la kuweka maneno ya uchochezi chini ya utawala wangu hilo halitakuwepo kuna magazeti mawili tu kila ukisoma wao ni kuchochea tu ikizungumzwa habari hii wao wanageuza hii nasema na nataka wanisikie siku zao zimeshafika kama wanasikia wasikie wasiposikia wasisikie lakini magazeti mengine na vyombo vyote vingine vinatoa uchambuzi mzuri sana''.
Rais Magufuli amesema Serikali yake haiwezi kuvumilia kuona amani ya nchi inahatarishwa na magazeti mawili kwani amani ndio chimbuko la maendeleo ya taifa lolote duniani.
Amesema bila kuwepo kwa amani hakuna mwekezaji atakayeweza kuja kuwekeza nchi, hata wawekezaji wa ndani watashindwa na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Rais Magufuli amesema uwepo wa amani nchini ndio uliowezesha wawekezaji wa Kiwanda cha Fresho cha kutengenezea mifuko ya kubebea bidhaa za chakula nchini na kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji baridi mkoani Shinyanga kujengwa mkoani hapo kwani bila amani visingeweza kujengwa.
Aidha ameitaka Benki ya Uwekezaji Nchini TIB na Taasisi nyingine za fedha kutoa mikopo kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika viwanda badala ya kuwakopesha wanasiasa ambao hutumia fedha wanazokopa kwa matumizi yasiyowanufaisha watanzania waliowengi
Rais Magufuli ameupongeza uongozi wa mkoa wa Shinyanga kwa kuanza kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya kutaka Tanzania ya viwanda kwa kujenga viwanda vingi mkoani humo ikiwa ni pamoja na viwanda hivyo viwili alivyovizindua katika siku yake ya mwisho ya ziara mkoani Shinyanga.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu
Shinyanga
13 Januari 2017.
------——-———
Rais John Magufuli amesema vyombo vya habari vinavyopotosha ukweli na kuleta uchochezi siku zake zinahesabiwa kwani Serikali yake anayoiongoza haiwezi kukubali kuvurugwa kwa amani ya nchi.
Amesema mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994 chanzo chake ni vyombo vya habari, hivyo hawezi kukubali hali hiyo itokee nchini.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa Kiwanda cha Jambo Food Plant mjini Shinyanga na matangazo yake kurushwa mubashara na Star Tv, Rais Magufuli amesema magazeti yote isipokuwa mawili, vituo vyote vya televisheni na redio nchini vinafanya kazi nzuri ya kuelimisha wananchi.
Rais Magufuli amesema Serikali yake haikatai kukosolewa na kwamba, magazeti mengine yanakosoa na kusaidia kutatua matatizo ya jamii, lakini hayo mawili (bila kuyataja) yamekuwa ni kupindisha kila kitu.
“Hayo magazeti kila ukisema hivi yanapindisha, siyataji kwa sababu yanajifahamu lakini yajue kwamba siku zake zinahesabika. Serikali ninayoiongoza haiwezi kukubali amani kuvurugwa,” amesema.
Chanzo: Mwananchi
=====
Habari hii imetumika ktk JamiiLeo