Rais Magufuli polisi Arusha ni jipu

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
226
180

Shughuli za jeshi la polisi nchini zinaongozwa na sheria mbalimbali lakini kwa kiasi kikubwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,sheria ya jeshi la polisi nambari 322(police and Auxiliary services Act 2002 cap 322) sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai na kanuni za polisi(Police General Orders).

Polisi wanaweza kukamata,kufanya upekuzi,kushikilia,kupeleleza mtuhumiwa,kumhoji shahidi,kufanya mahojiano na mtuhumiwa,kutawanya waandamanaji wenye nia ovu na kuhakikisha usalama wa jamii lakini wanapaswa kufanya hivyo kwa kufuata taratibu na sheria na sio wapendavyo.

Sheria ya polisi inaeleza kuhusu uendeshaji wake,nidhamu,mamlaka ya kazi za polisi na mambo mengine yanayolihusu jeshi la polisi kutenda haki katika utendaji wao ili kutoa mfano wa kulinda sheria na kanuni za nchi.

Matumizi yoyote mabaya ya mamlaka au uzembe katika kazi ni utovu wa nidhamu na uhalifu na afisa wa polisi anayatenda hayo anapaswa kuchukuliwa hatua kwa kuwa jeshi la polisi lipo kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza kuhakikisha kuwa kila mtu wakiwemo askari polisi wanafuata sheria kila wakati.

Hivi karibuni kumekuwa na matukio ambayo yamekuwa yakifanywa na jeshi letu la polisi walipo katika kituo kikuu cha polisi cha kati jijini Arusha ambayo yumkini hayaleti picha nzuri kwa wananchi ambao ndio wadau wakubwa wa usalama katika nchi hii.

Kumekuwa na taarifa za vitendo vya rushwa,vipigo kwa mahabusu ,vitendo vya kubambikia kesi,watuhumiwa kulazimishwa kutoa maelezo kinguvu sanjari na tuhuma za askari kuiba mali za watuhumiwa wanaofikishwa mbele ya kituo hicho.

Mbali na tuhuma hizo pia kumekuwa na taarifa za baadhi ya askari wa kituo hicho kuwapelekea mahabusu sigara na pombe wakiwa ndani mahabusu kutoka nje ya kituo hicho baada ya kupokea fedha hakika hizi ni tuhuma ambazo hazipaswi kuachwa hivi hivi ni lazima kuwepo na mjadala wa kitaifa kuhusu hili.

Itakumbukwa ya kwamba wakati wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete akifunga mafunzo ya maofisa warakibu wasaidizi katika chuo cha kitaaluma ya Polisi Dar es salaam aliwahi kukemea vikali tuhuma za rushwa dhidi ya polisi huku akisema tafiti zinazofanywa na taasisi mbalimbali jeshi hilo bado linaoongoza kwa rushwa.

“Bado kuna wenzenu wachache ambao wanachukua rushwa,wachukulieni hatua ili mwondokane na aibu hii,msikubali watu wachache waharibu sifa ya jeshi la polisi”aliagiza Rais Kikwete

Miongoni mwa tafiti ambazo zimetoa matokeo yake hivi karibuni ni pamoja ni pamoja na taasisi ya AfroBarometers ambayo ilisema kuwa polisi wanaongoza kwa rushwa nchini kwa kiwango cha asilimia 50 wakifuatiwa na TRA na serikali za mitaa waliopewa asilimia 37 huku majaji na mahakimu wakiambulia asilimia 36.

Ni ukweli ulio dhahiri ya kwamba jeshi letu la polisi hususani kituo kikuu cha polisi cha kati Arusha kinapaswa kujisafisha na tuhuma hizi hazileti picha nzuri mbele ya hadhira na nchi kwa ujumla kwani hata Rais Kikwete ameliona hili na ndio maana kaamua kumwaga mchele hadharani.

Baadhi ya wakazi wa Arusha wamekuwa wakifikisha malalamiko kwa waandishi wa habari kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki kwa askari waliopo katika kituo hiki ambapo kwa sasa wamekibatiza jina kuwa”kuingia bure kutoka ni pesa”.

Baadhi yao wanasema ya kuwa askari wa kituo hiki wamegeuza majukumu yao na sasa wamejikita kufanya biashara kwa kuangalia fedha kutoka kwa watu mbalimbali wanaofika katika kituo hiki kufikisha malalamiko yao ili waweze kusaidiwa.

Ni lazima askari wa kituo hiki watambue ya kwamba wako hapo kwa mujibu wa sheria na taratibu za jeshi hilo kugeuza majukumu yao na kujikita katika kukusanya fedha kwa namna yoyote ile ni makosa makubwa ambayo yanapaswa kukemewa.

Ni nani asiyetambua ya kwamba dhamana ni haki ya mshatakiwa?lakini kwa kituo hiki hali imekuwa kinyume kwani baadhi ya wakazi wa Arusha wamekuwa wakilalamika kuwa hawapewi dhamana bila pesa kana kwamba dhamana imehalalishwa bila fedha haiwezekani.

Askari wa kituo hiki ni lazima warejee katika msingi ya haki na uwajibikaji bila visingizio vyovyote kwa kuwa chombo ambacho wananchi wanakitarajia katika utoaji wa haki na ni kimbilio kwao kinapopotoka kwa namna yoyote ile katika msingi yake ni janga la taifa.

Kama jeshi letu linavyojidadavua kwa kauli mbiu yao kwamba “Tii sheria bila shurti”vivyo hivyo polisi wa kituo hiki wanapaswa kufanya majukumu yao kwa kuzingatia sheria ya jeshi la polisi nambari 322 bila visingizio vya aina yoyote.

Ni lazima watambue ya kwamba hakuna aliye juu ya sheria watanzania wote wakubwa kwa wadogo,matajiri kwa maskini,wanaume kwa wanawake bila kujali dini wala itikadi,watumishi wa umma wote ni lazima watii sheria na anayekiuka ni lazima aadhibiwe kwa mujibu wa sheria.

Kimsingi ninachokiona hapa tatizo kwanza ni kwamba baadhi ya askari wa kituo hiki wamekaa kwa muda mrefu na hii imewafanya kufanya kazi kwa mazoea kutokana na kuishi katika mazingira yale yale hawa wamegeuka “Miungu watu” kwa kuwa wamejenga mitandao ya ulaji hawa wanastahili uhamisho.

ITAENDELEA........

NB;-

Ningependa kutoa ushauri kwa mkuu wa jeshi la polisi nchini,IGP Mangu kwamba sasa ni muda wake wa kukunjua makucha yake na kisha kuwamulika askari na viongozi wa kituo hiki kwa ujumla na kisha kuchukua hatua kwa kuwa kuendelea kubaki na askari wachache wenye mrundikano wa tuhuma hizi ni aibu kama Rais Kikwete alivyotamka.

Mwisho tunapenda kutoa rai kwa waziri wa mambo ya ndani hapa nchini,Charles Kitwanga kuanza uchunguzi wa baadhi ya askari wa jeshi la polisi mkoani Arusha na kisha kwuachukulia hatua kali za kiesheria.

Hizi tuhuma hazipaswi kuachwa hivi kwa kuwa zinachafua na kuharibu taswira ya jeshi letu la polisi na tunapozungumzia dhana ya utawala bora ni pamoja na kufanya marekebisho kwa jeshi hili na askari wachache wasio wahadilifu ambao wanaleta picha mbaya.

NB;-(Katika toleo lijalo tutawaletea matumizi ya pingu za jeshi la polisi mkoani Arusha pamoja na vitedo vya baadhi ya askari kushiriki rushwa kwa wafanyabiashara wa madawa ya kulevya na mirungi jijini Arusha)

NAKALA;-RAIS JOHN MAGUFULI
R.C ARUSHA
WAZIRI KITWANGA
IGP MANGU
OTHMAN RASHID(TISS)
VALENTINE MLOWOLA
KAMANDA WA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA
 
Attachments

  • download.jpg
    download.jpg
    6.9 KB · Views: 36
Kuna uhamisho wa whatsapp,kuna oc cid mmoja alihamishiwa mara kwa msg ya whatsapp ya kigogo wa police,yupo anahudumu police mara,Magufuli fumua jeshi kuanza upya si ujinga
 
Dhamira ya kutumbua MAJIPU isitumiwe kama kichaka cha kutaka kuwaharibia watu Kazi zao, maaana sasa inaonekana dhamira hii Mhe Raisi inatumika kama kete ya kuwafitini watumishi na Serikali, jambo hili lisipo chukuliwa kwa uangalifu wengi wataumia na watajenga chuki na serikali. Ni vyema Serikari pamoja na taasisi za serikali zakawa makini sana kabla ya kuwawajibisha wanao tuhumiwa maana sasa kinacho fanyika ni kutengeneza MAJUNGU dhidi ya watumishi.
 
Back
Top Bottom