Rais Magufuli: Nitatumbua majipu hadi yaishe

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
RAIS John Magufuli ametoa mwito kwa Watanzania kumuombea ili aendelee kuwashughulikia wote wanaofanya ubadhirifu wa fedha za umma kupitia kampeni yake ya kutumbua majipu.

“Nataka niwahakikishieni kuwa nitaendelea kutumbua majipu yote mpaka yaishe, na naomba mniombee ili kazi hii ya kutumbua majipu ifanyike kwa mafanikio,” alisema Dk Magufuli.

‘’Arusha sitawaangusha, Kilimanjaro sitawaangusha, Watanzania sitawaangusha. Sasa ni wakati wa kuchapa kazi tu ili nchi yetu isonge mbele kwa sababu ni tajiri. Imejaliwa kila kitu na hilo linawezekana kabisa’’ Alisema.

Alitoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha jana, alipotua kwa ziara ya kikazi ikiwa ni ya kwanza kwao tangu achaguliwe kushika wadhifa huo Novemba 5, mwaka jana.

Dk Magufuli aliwasili mkoani Arusha, ambako kesho atatunuku Kamisheni kwa maofisa wanafunzi wa kundi la 57/15 katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli mkoani hapa.

Rais Magufuli aliwasili mjini Arusha akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), alikotua kwa ndege akitokea jijini Dar es Salaam na kupokewa na mamia ya wananchi. Akiwa uwanjani hapo, Rais Magufuli aliwashukuru wananchi kwa mapokezi makubwa aliyoyapata na aliwaeleza kuwa uchaguzi umekwisha, kilichobaki ni kazi tu.

“Nawashukuru sana ndugu wananchi kwa mapokezi haya makubwa, naomba kuwahakikishia kuwa uchaguzi umekwisha na sasa kilichobaki ni kuchapa kazi tu,” alisema Rais Magufuli. Akiwa njiani kutoka KIA, Rais Magufuli alisimamishwa na wananchi wa njiapanda ya KIA, Kikatiti, Usa River, Tengeru na Mount Meru mjini Arusha ambako huko kote pamoja na kusisitiza kuwa uchaguzi umekwisha na kilichobaki ni kuchapa kazi, aliwahakikishia kuwa hatawaangusha.

Aidha, Rais Magufuli alisema tayari serikali imeanza kutoa fedha kwa ajili ya kugharimia elimu ya msingi na sekondari baada ya kufuta ada na alionya kuwa watumishi wa umma hususani wakuu wa shule watakaothubutu kufanya ubadhirifu wa fedha hizo watashughulikiwa.

Alisema yote aliyoyaahidi kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na Watanzania kwa ujumla, ikiwemo ujenzi wa barabara za Arusha, kulipa fidia za wananchi na kufuta ada ya shule za msingi na sekondari yanatekelezwa.

Rais Magufuli alisisitiza kuwa serikali yake haitawabagua Watanzania kwa dini zao wala makabila yao na wala haitawabagua kwa misingi ya vyama vyao na kanda zao. Aliwataka Watanzania wote kuiweka mbele Tanzania na kushirikiana kuiendeleza.
SOURCE:Habarileo.
==============================================================
81.jpg

DSC00788.JPG

DSC00786.JPG

Baadhi ya wananchi waliojitokeza barabarani kumlaki Rais Magufuli kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)
POM3.jpg
 
Uongozi wa aina hii nilitamani kwa muda mrefu uwepo nchini. Matamanio yangu yamekuwa ni ndoto iliyotimia.

Tanzania ilihitaji kwa muda mrefu Rais ambaye ni no-nonsense and results-driven. Tanzania imempata Rais Magufuli.

Kuna wengine nimesikia wanasema he’s a cross-breed, part Sokoine and part Mrema.

Mimi ninasema Rais Magufuli is own man who man up.

There are few people still asleep or don’t want to accept reality!

They need to wake up to the new dawn!

Tanzania ya Rais Magufuli siyo ya jana iliyokuwa kwa kiasi kikubwa Laissez-faire and dysfunctional.
 
MsemaUkweli nitamuamini Magufuli pale atakapoingilia kwenye MAJIPU haswa!!!!!!!!!!!Kama UDA hivi,MENO ya TEMBO,ESCROW na yale majina ya ESCROW kule Stanbic,kumchukulia hatua yule Singasinga wa ESCROW hapo ndipo nitasema anajitahidi,lakini kwa sasa sina uhakika.Naona anavyotumbua ni vichunusi tu
 
Tumpe nafasi, hata haya anayoyafanya si haba. !
 
Tetty ni haki yako kibinadamu na kikatiba kutomuamini yeyote!

Binadamu tunatofautiana kifikra na kimtazamo!

Mimi nimejenga hoja katika msingi wa kile ambacho Rais Magufuli amekifanya kivitendo mpaka sasa.

Wewe unasubiri afanye yale ambayo wanasiasa wamekuaminisha kama yapo!

Ni hawa hawa wanasiasa waliotuambia Lowassa ni fisadi namba moja lakini kwa sasa wanatuambia Lowassa siyo fisadi bali mfumo ndiyo fisadi.

Ninafahamu kina Tomaso wa kwenye Biblia ni wengi sana duniani lakini hata hivyo walishapewa majibu yao mapema!

Rais Magufuli kama binadamu, anatoa majibu kwa kina Tomaso kila siku!
 
MsemaUkweli nitamuamini Magufuli pale atakapoingilia kwenye MAJIPU haswa!!!!!!!!!!!Kama UDA hivi,MENO ya TEMBO,ESCROW na yale majina ya ESCROW kule Stanbic,kumchukulia hatua yule Singasinga wa ESCROW hapo ndipo nitasema anajitahidi,lakini kwa sasa sina uhakika.Naona anavyotumbua ni vichunusi tu
Mkuu nenda hospital na waambie wakupime ugonjwa wa "Ushabiki-Maandazi Disorder"...unaonyesha dalili zote kuwa na huo ugonjwa wa akili
 
Kuna Majipu mengine hashikiki na Siku akiwagusa......ndio maana kapunguza Speed baada ya Wale wazee kumtembelea Ikulu...
 
Tumpe nafasi, hata haya anayoyafanya si haba. !
Kuna wengine hawataki kuiona picha iliyoko mbele yao!

Usitegemee kama wataweza hata kusoma!

Hii ni dhana iliyojengwa na wanasiasa uchwara ambao wanasema, ukiwa mpinzani lazima upinge kila kitu, otherwise utakuwa msaliti.
 
Atakamua majipu ya wakati wa utawala wake,msidhani ataanza kufuatilia waliofirisi kampuni ya RTC au SUKITA
 
t
MsemaUkweli nitamuamini Magufuli pale atakapoingilia kwenye MAJIPU haswa!!!!!!!!!!!Kama UDA hivi,MENO ya TEMBO,ESCROW na yale majina ya ESCROW kule Stanbic,kumchukulia hatua yule Singasinga wa ESCROW hapo ndipo nitasema anajitahidi,lakini kwa sasa sina uhakika.Naona anavyotumbua ni vichunusi tu
Tetty urewedi yaani huoni jitihada zilizofanyika angalia Bandari hata mm nilikua sijui uozo pale kuokoa matrilioni sio mchezo hao s na crow watajipanga,na minjino ya ntembo yatatulizwa mkuu ameanza na kujenga uchumi hasa kwenye main source of economic growth accelarator
 
Akamue tu kama ana nia ya dhati!, kundi linalomuombea ni kubwa sana nyuma yake. Wanaombeza ni wachache sana asihofu; aendelee na kazi Mungu yu Pamoja nae. akumbuke KWENYE SAFARI YA MAMBA NA KENGE WAMO, asife moyo wanaodai kumtolea kauli za kumvunja moyo
 
Washaanza kumkosoa kama ambavyo atakosolewa tu na wahafidhina ndani ya chama chake, juzi Kinana kawaambia wabunge wa chama chake waikosoe serikali waweke maslahi ya wananchi mbele Jana mmemsikia Membe kamkosoa pia katika suala la baraza la mawaziri na safari za nje kazi bado ni ngumu mkuu na watakao muangusha ni watu ndani ya chama chake sababu wengi ni wala rushwa ambayo Dr JPM anajitahidi kuiziba mianya yake.
 
b
MsemaUkweli nitamuamini Magufuli pale atakapoingilia kwenye MAJIPU haswa!!!!!!!!!!!Kama UDA hivi,MENO ya TEMBO,ESCROW na yale majina ya ESCROW kule Stanbic,kumchukulia hatua yule Singasinga wa ESCROW hapo ndipo nitasema anajitahidi,lakini kwa sasa sina uhakika.Naona anavyotumbua ni vichunusi tu
bado kukutumbua wewe ndio utaamini majipu yanatumbuliwa. its a matter of time na hii ndio procedure.
 
MsemaUkweli nitamuamini Magufuli pale atakapoingilia kwenye MAJIPU haswa!!!!!!!!!!!Kama UDA hivi,MENO ya TEMBO,ESCROW na yale majina ya ESCROW kule Stanbic,kumchukulia hatua yule Singasinga wa ESCROW hapo ndipo nitasema anajitahidi,lakini kwa sasa sina uhakika.Naona anavyotumbua ni vichunusi tu

escrow na singasinga............siyo nchi itatikisika ila dunia nzima itasimama
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom