Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Rais Magufuli haujafikisha mwaka mmoja ukifanya kazi hapo Ikulu. Unapohutubia uso wako hufanana na kile unachokiongea. Huo ni uzalendo na upendo wa kweli kwa taifa lako. Haujakamilika unao udhaifu wako mwingi tu kama vile binadamu yoyote yule alivyo.
Ushauri wangu wa bure ni kwamba mapambano ndio kwanza yameanza, mirija ya madalali wa kimataifa inaendelea kukatwa lakini kumbuka kuwa bado hawajachoka kutafuta njia nyingine za kufanya udalali wao. Huwa hawachezi mbali na Serena Hotel, White Sands, Kilimanjaro Hotel na nyingine zenye hadhi ya juu, lengo ni kutafuta channel kubwa kubwa.
Najua kuwa kwa sasa taasisi nzima ya urais ipo kazini kwa maana ya kufanya kazi zenye kuyagusa maisha ya wanyonge lakini kumbuka kuwa waliozoea kula bila ya jasho siku zote vichwa vyao havilali hata kama miili yao ipo vitandani.
Kumbuka kuwa aliyekutangulia aliitwa chaguo la Mungu, kumbuka kuwa ziliandikwa makala nyingi za kumlengesha ili aingie kwenye njia mbaya za kiuongozi. Mitego ni mingi sana na wewe ni binadamu.
Mama watoto anaweza kuwekewa mtego wa kuanzisha NGO ambayo mfadhili wake mkuu ni rais fulani mstaafu wa nchi zenye kutufadhili, lakini komaa na mwambie Mama kwamba ikulu ni mahali patakatifu hata kama wakati mwingine inaweza kugeuzwa pango la shetani kupitia mambo yanayofanyika kwenye mahoteli niliyoyataja hapo juu
Pambana mheshimiwa kwani vishawishi huenda vikibadilika kutokana na mabadiliko ya maendeleo ya dunia ya sasa. Kila la kheri.