Rais Magufuli ni lini tutaona Drug Tycoon wa Bongo wanafikishwa Mahakamani na Kuhukumiwa?

abdulrahim

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
408
286
Kwa kweli naandika heading hii nikiwa na imani kwamba ni mapato mengi yamepotezwa kwa kushamiri kwa biashara ya madawa ya kulevya nchini Tanzania. Vijana wengi ambao ni nguvu kazi kwa taifa na wachache ambao wangeweza kutoa ajira kwa wengi wao waliowazunguka leo wao ndio wamekuwa wahitaji wa msaada(Kiuno bila mfupa & Kingkong).

Wauza ngada hawa hawa ambao wanafahamika na kutamba mtaani leo ndio wanakuwa mashujaa na kujitoa mbele ya mitaa na kutanua kwa magari na mijengo ya kifahari kwa kuwa hakuna ushahidi lakini ukienda kwa mateja wao wanayajua hayo yote.

Inaniuma saana kuona vijana wanaochipukia kuoana kwamba biashara ya ngada ndiyo yenye kulipa kwa haraka..leo hii ukipita maeneo mengi ya Kinondoni utalisadiki hili. Pia naumia zaidi kuona gari la maafande likiwa limepaki eneo ambalo ngada inauzwa na pembeni yake watu wanaendelea kuuziana unga huo pasipo hatua stahiki kuchukuliwa (Kinondoni manyanya case study)

Hivi nauliza kwamba.
1. Nchi hii imekosa taarifa za kutosha juu ya wauzaji wakuu wa ngada?

2. Drug Tycoon ndio wenye haki ya kuharibu vijana wa taifa hili, huku wakipigiwa ugeregere na vyombo vya usalama.

3. Intelijensia yetu ndio imeishia hapo pasipo kuona hatua stahiki zinachukuliwa.

Naomba sasa ni wakati wa serikali ya #HAPAKAZITU kuondoa matongo tongo yaliyojaa kwenye mboni zetu juu ya Wuzaji wa madawa ya kulevya na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya..

Ahsanteni,
 
Back
Top Bottom