Hilo la wahadhiri bora afanye hivyo maana wameharibu wanachuo wengi sana wacha kije kizazi kipya wa wahadhili Ukipima elimu yao na wanavyofanya ni zaidi ya uharo hata hawa walioteuliwa Siku hazigandi mtashukuru kuondolewa vyuoni...
wewe kijana unawajua hawa waliokua vichwa wa department of chemistry pale UDSM?
Prof. Mubofu(hapo awali alikua Dr. Mubofu). Huyu alikua anafundisha chemical kinetics and electrochemistry. Sijaona mbadala wake pale UDSM. Walikuepo wadokta wakashirikiana nae pale ktk hio kozi, ila wote pumba tu, labda kidoooooogo Dr. Lytu aliyekua anafundisha enzymes kinetics. Pengo la Prof. Mubofu haliwezi kuzibika kirahisi kwa sasa, labda kwakuwa wavumilivu ktk kupata elimu ya chini ya viwango.
Dr. Mdachi, maarufu kama Dr. ENANTIOMER. Huyu alikua anafundisha organic chemistry II, maarufu kama ENANTIOMER. kozi ile wakati mwingine walikua wanashirikiana na Dr mmoja hivi, ambaye kifuupi hakua poa sana kiufundishaji na nkimalezi kama Dr. Mdachi. Kuondoka kwa Dr. Madachi pale depaartment organic Chemistry II halisi imepotea kwa muda, itayofundishwa pale itakua ni feki feki. Ila hata hivyo, nasikia kwakua kaondoka tu na sio kwamba kafariki; nasikia department imemuomba awe anakwenda kufundiha ili wanafunzi weendelee kuneeemeka na madini originl kutoka kwake, na sio feki.
Prof. Mdoe. Huyu alikua anafundisha basic analytical and physical chemistry, hasa katika kipengele cha physical chemistry. huyu ni mlimevu, ila pamojaa na ulemaavu, alikua anafundisha zaidi ya madokta vijana ambaao wao walikua wako beze kusema "we can skip this slide, and this and this ...", mpaka kozi inaisha. Kutokana na uweo wake mkubwa, alikua anachukuliwa na vyuo vingi sana ili akawape madini halisi watoto. Kasa kuondoka nahisi yule jamaa aliyekuja kutufundisha kipati fulani cha hiyo kazi kwa kutusomea 'slide' ndiye atakua kakabidhiwa kozi, hili ni jnga la taifa.
Kiufupi hakuna neema kwa kuondoka kwa hawa vichwa makini waliokua wanafundisha chemistry na kumfanyaa mtu aelewe chemstry.
Mwisho napenda kumuomba JPM asiwachukue Prof. Mhinzi, ambaye ni bingwa wa ingoganic chemistry anayefundisha chemistry alisi, sio contaminated chemistry; Prof. Othman, ambaye ni bingwa wa Instrumental Methods in Analytical
Chemistry; Dr. Kessy, ambaye anacheza miguu yote, ... Huyu baada ya kupata uzoefu wa kotosha akaacha kupoteza muda mwingi ktk kuelezea mambo hali inayopelekea kupoteza muda wa kufundisha, atakua mrithi wa prof. Mhizi au wa prof. Othaman kwa hapo baadae; Dr. Nyanddoro, ambaye anatakiwa aache kutisha wanafunsi na kuwawekea woga na hatiamaye kuwafelisha, badala yake atafute mbinu zaidi ya kuifundisha chemisty,.. huyu anaweza kua mrithi wa Dr mdachi hapo baadae ila baada ya kupata uzoefu wa kutosha na kubadilika kitabia; mdada mmojaa maahiri tanzania nzima ktk chemistry, Dr. j. Munisi,..... huyu kwakweli kwasasa hana mbadala ktk organic spectroscopy pale UDSM,.... japo kozi yake ni ngumu hivyo na maaswali yake ni magumu pia, ila material kutoka kichwani kwake husababisha wanafunzi kuelewa vyema na hatimaye wale gifted kupata A ktk mitihani yake; Dr. Mgina kafiti sana kwenye organic chemistry I, asiguswe huyu; na Dr. R. Peter, pingwa wa coodination chemistry asiye na mbadala kwasasa. Dr. Mkayula umri umeenda na ameshastaafu, ila pengo lake bado limemshika pale UDSM. Chondechonde rais, ulishajeruhi elimu ya Taanzania,ila usiguse kwa hao vichwa waliobaki, utaua elimu yetu.