Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,599
- 6,670

Si kwa sababu ya wabunge kumwita akakataa, la hasha!
Si kwa sababu ya kutumiwa na wauza madawa na kujifanya yupo kwenye vita dhidi ya dawa hizo huku akiifanya kazi hii kwa maelekezo ya wahusika wakuu ili kuua vita yenyewe kabla ya kufika kokote (akishirikiana na baadhi ya maafisa wa vyombo vya dola wasio na weledi wa kazi yao).
Si kwa sababu ya zile taarifa mfu alizokuwa akikupenyezea ili ang'are mbele zako na Taasisi nzima ya urais kuwa ni RC bora zaidi ya RC yeyote nchini.
Si kwa sababu ya tuhuma za kuwa na mali zenye mashaka mengi tangu akiwa DC na hata sasa ambazo vyanzo vyake idara nyeti zinajua na zimekudokeza mara kadhaa huenda hukujua athari zake.
Si kwa sababu ya yaliyotokea kupitia kijana huyu katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Jakaya Kikwete ambayo mengine kuyaandika ni aibu.
Si kwa sababu ya vyeti vyake vyenye utata, la hasha!
Ni kwa Matumizi Mabaya ya Madaraka. Amelewa madaraka, ameota mapembe na sasa asipodhibitiwa Taasisi ya Urais (si wewe kama Magufuli) itaingia fedheha kubwa zaidi ya kinachoonekana sasa.
Haya unayoona ni mvua za rasharasha, mvua kamili itanyesha Aprili 2017 na hutoamini athari itakayoikabili Ikulu yako na kuchafua legacy yako.
Unao muda, chukua hatua mapema!