Mr Hero
JF-Expert Member
- Jun 11, 2015
- 5,540
- 7,452
Rais Magufuli, amepiga marufuku usafirishaji mchanga kutoka machimbo ya madini kwenda nje ya nchi
Rais JOHN MAGUFULI, amepiga marufuku usafirishaji mchanga kutoka machimbo ya madini kwenda nje ya nchi , kwa madai ya kupimwa kubaini kama kuna madini ya dhahabu na viambata vyake.
Rais Magufuli ametoa msimamo huo wa nchi kabla ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha Tarazo (Tiles),cha Goodwll Tanzania Ceramic Company Limited,katika kijiji cha Mkiu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani,chenye uwekezaji wa dola milioni mia 400 kikitarajiwa kuzalisha tani 8,000 za tarazo kwa siku,kikitoa ajira za mojamoja kwa moja 1,500 na zisizo za moja kwa moja zaidi ya 4,000.
Rais Magufuli amesema wawekezaji wamekuwa wakikiuka taratibu kwa muda mrefu na kusema Tanzania imeliwa vya kutosha na kumuagiza waziri wa nishati na madini Profesa Sopspeter Muhongo kusimamia suala hilo.
Kuhusiana na kiwanda hicho,amewatahadharisha wananchi wa Mkuranga na maeneo ya jirani kuilinda amani katika eneo hilo kufuatia vitendo vya kihalifu vinavyoendelea mahala hapo katika siku za karibuni,na kusema kuwa watawakimbiza wawekezaji na wao ndio watakuwa waathirika kwa kukosa fursa kama zilizoletwa na kiwanda hicho na nyingine zinazokuja.
Wakati huo huo,Rais Magufuli,amezungumizia suala la njaa na ametoa rai kwa wanasiasa kuacha kuwadanganya wananchi kuwa hakuna mtu atakayepoteza maisha kwa njaa na kuwatahadharisha wananchi hao kuwa mtu asiyelima atakufa kwa njaa.
Chanzo: Ten
My take;
Nakumbuka agizo hili liliwahi kutolewa kipindi cha nyuma, sasa kaagiza tena