Rais Magufuli kureallocate funds: Watu wanachemka na kujidhalilisha

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,750
6,448
Ndugu wanajamvi..kumekuwa na mjadala kama Mh Rais anafanya sawa kureallocate funds kutoka eneo moja kwenda jingine. Watu bila kutathimini kwa kina, wameishia kusema kuwa anaharibu mipango ya Bunge na hivyo kuwa dictator. Mambo yamekuwa mazito baada ya kuhakikisha pesa za sikuu ya ukimwi, Siku ya Kusherehekea Muungano kupelekwa kwenye shunguli zingine za kijamii.

Kwanini nasema wanaohoji na kumtuhumu Mh Rais hawajielewi juu ya hili suala. Nitatoa maelezo ya kimahesabu kama ifuatavyo:

  • Budget nzima ya mwaka 2015/16 ni 22 tillions Tsh Zikiwemo ahadi za wafadhili na Mikopo
  • Pesa zinazotarajiwa kupatika hadi June 30 2016 ni kama tillioni 20.(Baadhi ya Wafadhili hawatatoa pesa zao).
Maana yake hadi mwisho wa budget ya Mwakahuu, kutakuwa na upungufu wa tillion 2 Tsh. Je Kazi zilizokuwa zimepangwa kutekelezwa kwa hizi pesa zitakuwaje?Jibu ni kuwa hazitatekelezwa mwaka huu.
Kwa hiyo ukiwa na mapato pungufu kuliko mipango ya Matumizi basi kunakazi hazitafanyika. Pesa iliyopo itabidi itumike kwa vitu vya Msingi tu. Je kama pesa tengwa kwa ajili ya shuguli ya sherehe za muungano ni 4 Billion na pesa tengwa kwenye budget kwa ajili ya upanuzi wa barabara ya Morocco to Mwenge ni Billioni 4. Wewe kama mwamzi ungepeleka wapi? Mh Magufuri kaamua ziende kwenye barabara ili na habari ya Sherehe nayo ione uchungu wa kukoswa funds.

Tatizo tulilonalo watu wengi ni mazoea kuwa upungufu wa fedha lazima uwe kwenye shughuli za maendeleo tu lakini ikija kwenye sherehe lazima pesa iwepo. Hapo sasa Magufuri ndo kafanya tofauti kwa kupeleka hicho kidogo kwenye shughuli za maendeleo na akaziminya Sherehe pesa kwani rasilimali hazitoshiji kufanya kila kitu kama kilivyopangwa kwenye budgeti.

Ningeelewa hoja ya wanaombeza maamzi ya mh Rais kama Serikali ingekusanya tillioni 22 kama ilivyo kwenye budget, na Mh Rais akaamua kuchukua pesa kutoka kazi husika na kupeleke au kuongezea kwenye budget line nyingine.

Hivyo Ushauri wangu kwa wabunge na Wataalamu mbalimbali ni vizuri wajiridhishe kabla ya kulaumu. La sivyo mda si mrefu watadhalilika sana kwani najua Mh Magufuri anawalia timing ya kuwajibu na watajikuta wanasinyaa.

Ni hayo tu kwa leo
 
Hiyo sherehe ilikuwa inajulikana hata kabla bunge halijazinduliwa labda mambo ya budget hayabadilishwi kwa hati ya dharura yanabadilishwa na rais.
 
Hiyo sherehe ilikuwa inajulikana hata kabla bunge halijazinduliwa labda mambo ya budget hayabadilishwi kwa hati ya dharura yanabadilishwa na rais.

Budget iko palepale kwenye Makaratasi lakini suala la pesa iliyopo wakati husika ndo muhimu kuamua je tukale na kunywa siku nzima au ifanye kazi fulani ya maana zaidi ya Sherehe husikia
 
Budget iko palepale kwenye Makaratasi lakini suala la pesa iliyopo wakati husika ndo muhimu kuamua je tukale na kunywa siku nzima au ifanye kazi fulani ya maana zaidi ya Sherehe husikia
Unajipiga chenga mwenyewe rudi kusoma halafu tafakari kisha jiongeze.
 
Back
Top Bottom