kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,255
- 16,185
Baadhi ya viongozi wa CCM sio waaminifu kwa CCM, kwa wananchi na kwa taifa pia. Viongozi hawa walikifikisha chama, wananchi na taifa hapo vilipo sasa. Viongozi hawa walikuwa wanafiki mwanzo mwisho bila kujali elimu zao, dini zao, makabila yao wala taaluma zao.
Viongozi hawa ni wale ambao walikuwa wanafahamu kuwa nchi inaporwa lakini hawafanyi kitu, walikuwa wanafahamu kwamba sheria mbovu zinapitishwa lakini hawafanyi kitu, walikuwa wanafahamu kuwa mikataba mibovu inapitishwa lakini hawafanyi kitu. Viongozi hawa walikuwa wanawaongoza wanachama na watanzania kuimba iyena iyena CCM nambari one hata kama taifa linaporwa na kuliwa kama mchwa.
Rais Magufuli wabaini na kuwaondoa bila huruma viongozi hawa bila kuchelewa kwani hata wana-CCM tunawafahamu na unafiki wao kwa CCM na kwa taifa.
Sifa kubwa ya Viongozi hawa ni watu ambao hawakubali kustaafu hata kidogo, lazima watajichomeka kwa gharama yoyote kwenye uongozi wa chama, ubunge, kamati au bodi za mashirika nyeti. Wakishindwa wao watawachomeka watoto, ndugu au marafiki kwenye nafasi fulanifulani.
Nadhani Rais Magufuli kaletwa na Mungu kuiponya CCM na nchi, sio bure walahi!!!