BabaTina
JF-Expert Member
- Aug 29, 2008
- 429
- 580
Wandugu nawasalimu,
Mh. Magufuli apitie hapa asome na anielewe pia.Naandika ujumbe huu kwa hasira na uchungu mkubwa sana, hizi habari ambazo zinashika kasi kila kukicha kwamba PPF imepokea agizo toka juu kusimamisha mafao ya 'Withdraw benefit' zimezima speed yangu na munkari wa kuanzisha ajira yangu binafsi ambayo nilishaanda vijana we gine 4 kufaidika kupitia ajira hiyo.
Mh. Rais, kimsingi mie kuanzia mwezi wa 8 ntakuwa sina ajira kwani mradi ambao umeniajiri tayari utakuwa umefunga rasmi na waajiriwa wengi watalazimika kutafuta namna nyingine ya kuishi.
Kati yetu wapo ambao walishajiwekea misingi ya kuingia kwenye fursa za kujiajiri tena kwa kupitia taratibu zote za serikali lakini kwa bahati mbaya sana zuio la mafao yao kupitia PPF linaenda kuwanyima haki hiyo na kuwalazimisha waendelee kuwa watumwa kwa kuendelea kuajiriwa pekee!
Binafsi, Nilijipanga kabisa kuwa kuanzia mwezi unafuata yaani mwezi wa 9 ofisi yangu itakuwa inakimbia kwa spidi ya hatari sana kwani tayari huduma zangu zishaanza kuvutia wahitaji.
Now, Kampuni hii haiendi kuanza kwa kuwa mtaji mkubwa kwa asilimia 80 ukitakiwa utoke kwenye mafao hayo yaliyopo PPF na hawa PPF ndio wamezuia na Mh. Ukiwa kama Rais natambua unafahamu suala hili. Je, hii si kweli kwamba unachangia kuzima ndoto zangu!?
Mh. Rais hawa PPF mie nikiwa sina kazi nipo nyimbani pesa yangu watafaidika nayo wao.
Watajenga maofisi na kuwapangisha watu wengine wenye uwezo zaidi yangu mie nitabakia kuyaangalia tu sababu sina uwezo huo wa kupanga kwenye ofisi zao ingawa majengo hayo yamejengwa pia kwa mchango wangu mie kapuku!
Tazama hata nikuugua hawana namna ya kunisaidia kabisa kwani hawatoi mafao ya afya kwa wanachama wao. Je, huu si ni utumwa wa hali ya juu!
Mh. Rais, mfuko huu faida pekee ambayo ilikuwa inatusaidia sisi makapuku ni fao la kujitoa na hilo wengi wetu tunalitumia kwa maendeleo yetu binafsi sababu vijimishahara vyetu vimethibitisha kushindwa kutununilia gari, nyumba nk! Hivyo kupitia kafao hako ndipo ambapo sisi makabwela tunaweka mipango yetu ili tusije kuhadhirika tukiwa nje ya kazi!
Mh. Rais wanasema mafao yatatolewa mpaka tutakapofikia umri wa kustaafu, Je kustaafu huku kunatafsiriwaje kwa watu tunaotoka sekta binafsi ambao tunafanya kazi za mikataba na miradi ya muda maalumu!?
Lakini pia, mkisema nipewe pesa hiyo nikiwa na umri wa miaka55 nawezaje kuhakikishiwa kuwa mtaipandisha pesa hiyo thamani ilingane na thamani ya pesa kwa wakati huo ili walau ni jenge msingi wa nyumba ili nikifa nifie ndani ya kibanda changu!
Mh. Maisha ni leo, tumeona waliosubiria kesho wamesumbuliwa na mifuko hii na wamekufa mapema kwa kuwa haki zao hazikuwafikia na hivo kuwawaisha ahera!
Mh. Rais basi hawa PPF watupatie mikopo kwa hizo pesa zetu tufanye biashara zetu ama tujenge nk. Lakini hakuna kitu kama hicho sasa je mifuko hii ina maana gani kwetu kama haina misaada yoyote!?
Mh. Rais mabenki hayatusaidii chochote zaidi ya kutunyonya zaidi laiti kungekuwa na utaratibu mzuri wa kupata mikopo ya kufanya maendeleo ya biashara hakuna mtu angesumbuka na hivi vijimafao mh.!
Mh. Rais, Najua mie ni muathirika mmoja kati ya wengi wanaolilia taratibu hizi za kibabe kwenye taasisi zetu! Nafahamu kwa busara zako andiko hili litatukomboa sisi makabwela walau takaweze kujiajiri, tunahitaji kuwa na maisha mazuri kama ninyi basi ikishindimana tuwe na maisha ya afadhali mkuu!
Yapo mengi ya kuandika lakini kwa haya yanatosha kwa leo mh...nawachia na wachangiaje wengine waongezee hapa chini na mwisho wa siku andiko hili likufikie rasmi kwa njia yoyote ile kama kilio chetu mafukara wa Tz kutoka familia za makapuku.
Mungu akubariki unapofanya maamuzi ya hekima kutukomboa makapuku!
Mwananchi mwenye nyongo inayokaribia kutumbuka