Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Edward Hoseah

Kama ni Kweli hapa sina cha kupongeza,

Suala sio Dr.Hosea,Tatizo ni TAKUKURU kutokuwa Independent

Nilishauri kuwa Rais asome ripoti ya Jaji Warioba kuhusu Rushwa

Pia Sheria ibadilishwe,TAKUKURU waweze kushitaki bila kupitia kwa DPP

Pia arejeshe maoni ya Rasimu ya Wananchi .Kule mfumo mzima utakuwa umefumuliwa.Kumfukuza kazi Hoseah haimaanishi kuwa amepambana na Rushwa na ufisadi.Amemkomoa tu na kumdhalilisha tu kwa uonevu
Wewe hata ukiletewa maziwa nyumbni kwa bomba, utadai uletewe na ng'ombe!!!
 
Kamanda nzowa yule wa madawa ivi bado yupo kazini?

Ni vizuri akapitia Jeshi la magereza pia Jeshi la polis huku kwenye manunuzi ni balaa hata suma JKT napo kuna mengi siku Magufuli akipita humo Nchi itatikisika.
 
MiCCM inajuuta na hata kazi haijaanza lazima mtaisoma number lana ya wizi wa kura inawalamba wenyewe kwa wenyewe.:spy:
 
Sheria za nchi zinatungwa au kubadilishwa na mhimili unaitwa Bunge.

Wahi kamuone Mbunge wako mpe huu ushauri na dokezo kabisa awasilishe hoja binafsi Bunge la February faster.

Queen Esther

Bado Magufuli hajajua tatizo la hii nchi ni nini. Bila kubadili sheria mbovu zinazonyima uhuru vyombo km hivi hakuna kitakachobadilika. Takukuru inatakiwa iwe huru kumchunguza na kumshtaki mtu yeyote hata rais! Afrika kusini wanamwita mkuu wa hii taasisi Public Protector. Huyu hana mipaka ya kuchunguza! Km hosea alizembea ktk ishu ya bandari na tra vipi mawaziri na makatibu wakuu waliokuwa wanaongoza wizara husika? Walifanya nini kuzuia rushwa bandarini? Hapa kidogo simwelewi Magu!

Halafu mkuu wa taasisi nyeti na sensitiv km takukuru hapaswi kuwa mtu ambaye rais anaweza kuamua kumfukuza mda wowote. Lazima awe na kinga ya kikatiba km alivyo CAG na ikibidi kumfukuza kazi basi kuwe na jopo maalumu la kupitia tuhuma zake ili kujiridhisha isije kuwa labda kagusa maslahi ya mkubwa au rafiki yake basi rsis anaamua tu huyu aondoke! Lazima taasisi km hixi ziwe independent! Bila hivyo hatutafika popote!
 
Wengine wanaanza kuzurula na kufanya maigizo ya shukran kuanzia kesho
 
Kwanini Dr. Hoseah afukuzwe kazi? Hivi anajua kuwa PCCB ipo chini ya mamlaka ya rais na DPP? Mbona Hoseah alifanya kazi yake vizuri tu? Nini maana yake kumuweka naibu akaimu hiyo nafasi?

Sidhani kama hakuna kitu nyuma ya pazia kuhusiana na uchaguzi mkuu!

Lowassa anashughulikiwa kweli kweli!

Sijaelewa dhumuni hasa la kumfukuza Hoseah!! Labda ni kwakuwa "Lowassa" otherwise jamaa kashauriwa vibaya sana!
Kama unauhakika na uandikacho, yaani Hosea ni mtu wa Lowassa, basi kuna kila sababu ya kushughulikiwa kikamilifu.
Mteule wa fisadi hawezi kuupiga vita ufisadi.
 
Safi sana Mr President, hakuna mambo ya kuishi kimazoea kipind hiki cha Magufuli.
Sasa ndio watajua kuwa huyu jamaa si wakumletea Ujanja Ujanja.
 
Mkuu un akili kweli?
Unatumwa kukamata mwizi na wewe unasema mbona yule hajakamatwa, kwa kushindwa kufanya kazi yako?

Sitasahau comment ya Hosea katika sakata la Richmond, eti akasema kuna watu wakubwa nyuma ya hili sakata, tukiwashughulikia nchi itayumba!!
What nonsense!!

Mtu kama kazi haiwezi asiendelee kujaza nafasi ya kazi ya watu wenye uzalendo.
Nahisi na wewe huna akili. Sijasema mbona yule hajakamatwa nachozungumzia hapa ni issue ya double standard. Lazima kuwa consistent. Kosa lilelile lihukumiwe vilevile. Kwanini wanasiasa wanaachwa? Au kwa vile ni makada na viongoxi wa ccm? Hivyo nachosema hapa wote waliokuwa na mamlaka wakati haya yakitokea wawajibishwe. Sio kipick mtu mmojammoja!
 
Wanabodi,

Naomba ku declare interest, mimi ni miongoni mwa ma suppoter wakubwa wa Edward Lowassa humu jf, kwa sababu ni miongoni mwa watu tulioichoka CCM na kuamini kuwa CCM kamwe haiwezi kubadilika, lakini naomba kukiri, wazi, kitendo cha Magufuli, kumfuta kazi Dr. Hosea, kimenifanya kumkubali Dr. Magufuli kuwa he is for real!, hivyo sasa namsupport rasmi Dr. John Pombe Magufuli.

NB. Naomba support yangu hii isitafsisiwe kuwa sasa Pasco wa jf anajiunga na siasa, au anajiunga na CC, no way!, Pasco wa jf, sio mwana siasa, hajawahi kuwa mwanachama, mfuasi, mshabiki wa chama chochote cha siasa!, hivyo support yangu kwa Magufuli, haina maana sasa ndio nimeikubali CCM!, no way!. Nimemkubali Magufuli, kwa sababu, utendaji wake ni tofauti na CCM tuliyoizea!.

Kitendo cha kumfuta kazi Dr. Hosea, kimenipa imani kuwa Magufuli is for real!.

Kwa bandiko hili, natoa wito kwa wale wengine wote waliotaka mabadiliko ya kweli kwa Tanzania, tumuunge mkono Dr. John Pombe Magufuli na falsafa yake ya "Hapa Kazi Tuu!", kwa sababu ina lengo la kuleta mabadiliko ya kweli kwa Tanzania!.

Naamini wale wana mabadiliko wa kweli, watanielewa na wataniunga mkono, lakini wale wanamabadiliko ya 'mahaba niue' ya kupenda watu!, kama sio watu wao, hata wafanye mema vipi, watawabeza tuu!.

Taarifa hii, ndiyo iliyonifanya nimkubali John Pombe Magufuli!.

attachment.php



This man is for real, change for real, jee vipi wewe unamkubali?!.

Pasco.



Sasa unampongeza kwa kipi? kama angebadilisha sheria inayounda takukuru na kuiwezesha takukuru kushitaki watuhumiwa bila kupitia kwa dpp hapo kweli? au na wewe ni mkurupukaji asiejua tatizo kubwa la takukuru ni kua haina meno?
 
Mambo mengine kutafutiana ubaya tu.
Msukuma kakataza ,Wewe unasafiri na hujaomba kibali.
Ukisimamishwa utasema unaonewa.

kweli kabisa mkuu, wame mchokoza wenyewe .
Tena kama huyo kapwani ni afisa mwandamizi
huko TAKUKURU.
 
Waraka UNASEMA walinyimwa kibali. Sasa sijui nguvu ya kukaidi agizo la Mhe. Rais walitoa wapi??? Kazi kweli kweli!!!

Queen Esther

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , ndugu John Pombe Joseph Magufuli
amewasimamisha kazi maafisa waandamizi 4 wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na
Rushwa TAKUKURU kutokana na kukiuka agizo la Mh. Rais la kuto safiri nje ya nchi
bila kupata kibali cha Ikulu.

Pia mh. Raisi katoa onyo kali kwa watumishi wengine watao "beep fire" kwani
yeye atawapigia bila kupepepsa macho , na watakumbwa
na hii kumba kumba inayoendelea hsasa kwa wale wote wasio heshimu mamlaka za nchi.

Maafisa hao waliosimamishwa kazi kutoka makao makuu ya TAKUKURU ni
1.Bi. mary mosha.
2. doreen Kapwani.
3. Ekwabi Mujungu.
4. Rukia NIKITASI

attachment.php
 
Safi sana Mr President, hakuna mambo ya kuishi kimazoea kipind hiki cha Magufuli.
Sasa ndio watajua kuwa huyu jamaa si wakumletea Ujanja Ujanja.

saa hizi ndipo watu wataelewa maana ya nguvu na mamlaka ya Rais wa nchi
kuwa yeye akisema jambo ni amri na utekelezaji mara moja.
 
Back
Top Bottom