Rais Magufuli asiharibu vitu ambavyo vimemjenga!!!

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,704
9,060
Rais wa JMT Mhe. John Joseph Magufuli ameamua kwa maksudi kutangaza vita dhidi ya vitu au watu ambao/ambavyo vimemjenga na kumfikisha hapo alipo leo!
Kitendo cha Rais kutishia kuvifungia au kuviadhibu vyombo vya habari vinavyo andika habari zinazohusu migogoro ya Wakulima na Wafugaji kuwa ni UCHOCHEZI kinasikitisha!
Lakini pia Rais amekwenda mbali zaidi kutoa tangazo kupitia Mwandishi wake wa Ikulu Bwana Gerson Msigwa kuwa mitandao yote ya Kijamii itafungiwa kama itaonekana inaandika habari za uchochezi!! Pengine ni muhimu kwa Serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli kuweka bayana nini maana ya habari za uchochezi kiasi cha kupelekea MAUAJI YA KIMBARI kama ya RWANDA 1994!

Hivi kuandika habari za migogoro ya Wakulima na Wafugaji ni uchochezi kweli? Hivi kuandika habari za RC Makonda anayetuhumiwa kuvamia Clouds TV usiku wa manane na kutishia waandishi wa TV na kulazimisha warushe kipindi alichokiandaaa na kukihariri mwenyewe kwa ajili ya kumdhalilisha Mtanzania mwenzake ni uchochezi? Hivi kuandika habari za RC Makonda kuwa ameghushi vyeti na anatumia jina siyo lake ni uchochezi? Hivi kuandika habari za kuwa kuna njaa au ukame ni uchochezi?

Katika utawala wa Sheria kuna mihimili 4; Serikali, Mahakama, Bunge na Media. Kila muhimili una play role yake ili kusukuma maendeleo ya nchi yasonge mbele bila ya kuingiliana. Media ina jukumua kubwa sana la kuhabarisha Wananchi juu ya matukio mbalimbali yanayotokea nchini na nje ya nchi yawe mabaya au mazuri, yawe ya kivita au ya kiusalama, yawe ya kiuchumi au kisiasa. Kwa Viongozi waliojaa Hikima na Busara vyombo vya Habari ni kama KIOO cha kujitazama na kuona wapi Serikali inafanya vizuri au vibaya ili iboreshe iweze kuweka mambo vizuri zaidi.

Kiongozi anayepambana na Vyombo vya Habari kwa vile hataki viandike udhaifu wa Serikali yake au yeye mwenyewe binafsi, ni sawa na mtu KUJIANGALIA KWENYE KIOO NA KUONA SUTI YAKE HAIJAMPENDEZA HALAFU AKAAMUA KUVUNJA KIOO KWA KUKIPIGA NA RUNGU AU RISASI!! Ieleweke kwamba Media ndiyo zilizomsaidia Magufuli na CCM yake kuingia Ikulu baada ya Kampeni za Urais mwaka 2015! Iwe TV, Redio, Gazeti, JF, FB, Twitter,Whatsapp, Instagram, Youtube, Wasanii wa muziki n.k! Rais Magufuli bado amekwenda mbali zaidi kwa kuanza kuwatumbua au kuwafukuza kwa kuwaondoa kwenye nafasi za kazi hata watu ambao wanataka kusimamia Haki na Sheria. Watu ambao walifanya kazi Usiku na Mchana kuhakikisha Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. JPM anapata ushindi wa kishindo. Mtu kama Nnape Nauye unapomtumbua kwenye nafasi ya Uwaziri eti kwa kosa la kuunda Kamati ya kuchunguza Tukio la RC Makonda kuvamia Studio za Clouds TV inakuwa hueleweki.

Je, kwa muktadha huu wa Rais kuamua kutaka kunyamazisha media badala ya kujenga Viwanda ili kuwaletea maendelea Watanzania kama alivyoahidi wakati akiomba kura, nini mustakabali wa Tanzania baada ya miaka 5? Tujadili.
 
Back
Top Bottom