Testar
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 7,886
- 13,623
Rais ni mtu mwenye influence kubwa sana nchini.Kauli yake mara nyingi huchukuliwa kama sheria na hivyo hufuatwa/hutekelezwa na wengi wa wale anao waongoza.
Tabia za rais mara nyingi huakisiwa na watendaji wengine wa serikali maana kimsingi yeye ndiye mwajiri wao.Tunaweza kupata mfano kutoka kwa rais mstaafu Mh. JK, yeye alijielezea kama mtu mpole, hatima yake watendaji wengine walikuwa wapole zaidi hadi kufikia hatua ya kuathiri utendaji wa serikali.
Hata kwa rais Magufuli tumeshashuhudia jinsi tabia/mienendo yake inavyoathiri tabia za watendaji wengine.
Mara baada ya kuchaguliwa kuwa rais, JPM alifanya ziara kadhaa za kushtukiza kwenye baadhi ya taasis za umma na maeneo mengine. Watendaji wengine wa serikali nao waliiga mtindo huo huo wa kufanya ziara za kushtukiza.Mfano ni Dr Hamisi Kigwangala [NW] alivyomshtukiza Dr J.J Mwaka.
Rais hakuishia hapo tu bali aliongeza tabia nyingine ya kutoa matamko[baadhi ni kauli za kukurupuka] kwenye hizo ziara hata zile za kuandaliwa.
Baadhi ya matamko yake yalitofautiana na sera pamoja na mipango ya maendeleo kitu kilichosababisha watendaji wengine kurekebisha matamko yake kwa njia ya 'kiutu uzima'. Mfano wa matamko ni lile la kufyatua watoto bila kujali sera ya uzazi wa mpango.
Watendaji wengine nao wakaiga tabia za kutoa matamko ama kauli bila kujali jinsi uhalisia ulivyo. Tumeshuhudia RCs, DCs, RPC na mawaziri wengi wakitoa kauli na matamko[Mifano ipo mingi].
Sasa hivi Rais amegeukia utengano kwa misingi ya kisiasa, kubinya uhuru hasa wa kupata habari kama vile kuzuia Bunge Live. Yaani siku hizi kama mtu siyo mwanachama wa CCM au ni mwanachama wa CCM lakini hakubaliani na matakwa ya mwenyekiti, basi huyo ni wa kumfanyia vituko vya kila namna ili atambue kwamba kutokuwa mwanaCCM au kutokufuata matakwa ya M/kiti ni 'kosa kuu'.
Kitakachofuata ni watendaji wengine kuanza kuiga tabia za kibaguzi kwa misingi ya itikadi za kisiasa, kuwa na hulka ya kulipiza visasi, chuki, kuhubiri utengano pamoja na tabia nyingine zenye kuhatarisha ustawi wa taifa.
Kama tutaendelea kwa namna hii, si ajabu siku zijazo itamlazimu mtu athibitishe kuwa yeye ni mwanachama wa CCM ndipo ahudumiwe na taasi yoyote ya kiserikali.
Rais akumbuke kuwa yeye ni rais wa watanzania wote bila kujali tofauti zao. Akubali kuwajibika kuwatumikia watu wote kama alivyoapa, aoneshe mfano bora kwa watendaji wengine wa serikali. Afiche hisia zake hasa zile hasi pindi awapo mbele ya hadhara.