Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,557
- 8,662
Augustine Mahiga ni moja ya maafisa waliotukuka wa usalama [mr x], ambaye rekodi yake sio ya kutia shaka hata kidogo. Katika serikali ya Magufuli ni moja ya mawaziri waandamizi wanaoheshimika, ukiacha umri wake ambao umesongo kiasi, uzoefu wake umekuwa msaada mkubwa sana kwenye serikali, wengine wamesema ndio chaguo bora kabisa la rais katika baraza la mawaziri. Amefanya kazi kama afisa mwandamizi kwenye awamu zote nne na sasa waziri.
Nimelazimika kufanya tathmini kutokana na matukio matatu hivi.
1. Kutangazwa kama moja ya mawaziri ambao hawajawasilisha fomu za tamko la mali , ambapo katika utetezi wake alisema fomu alishajaza lakini hata rais alikuwa na taarifa kuwa alikuwa anamuwakilisha mikutano mbalimbali, mingine ambayo rais alitakiwa kwenda.
2. Tukio la Picha ya kumdhalilisha kama Waziri aliyejikojolea ambapo leo kwa masikitiko katika magazeti amekanusha kwa uchungu kuwa alijikojolea;''Hata mimi sijui lengo lao nini kuisambaza picha ile, maana mimi niliona kama ulivyoona wewe". "Sielewi lengo la walioitengeneza na kuisambaza picha ile".
3. Tukio la mke wake kurekodiwa na kudaiwa ametukana, wakati kwenye clip hakuna tusi kama tusi .. Pia ameeleza limemuuma sana, "wewe umesikiliza hiyo clip, je umesikia neno tusi? Hilo ndio ninalojuwa kwa sasa sijui mengine yanayoendelea".
"Ni kweli mama alikuwa katika barabara ya Namanga ambapo alipishana kauli na askari wa usalama, mimi nilifuatilia suala hilo kwa undani sana. Ninachoweza kusema sitaki kuingia kwenye malumbano juu ya suala hili kwa kuwa limeshamalizika".
4. Kitendo cha rais Magufuli kutangaza hadharani amemuonya waziri ambaye mke wake amehusika kumuonya mkewe [kwa kosa ambalo waziri kwa kinywa chake analalamika halioni kwa mkewe] lakini pia ijulikane kuwa mke wake ni mtu mzima mwenye nafsi na maamuzi yake ambayo huwezi kuyahukumu kwa mume moja kwa moja. Hata ingekuwa mahakamani angepelekwa mke wake. Sasa iweje kumuonya mtu mzima kama vile kosa limetendwa na mtoto wake wa chini ya miaka 18? [watetezi wa haki za wanawake watachukulia rais kamuona mke wa Mahiga kama mtoto]
5. Kitendo cha rais kuagiza polisi aliyemrekodi na kusambaza audio clip ya mtuhumiwa na kumfanya ahukumiwe na umma bila kusikilizwa [sijui sheria zinasemaje juu ya kumrekodi mtu bila ridhaa yake na kusambaza], apandishwe cheo, ni kama kumpiga tena balozi Mahiga kofi.
Sasa kwa kuhitimisha, haya ndio malipo ambayo huyu waziri anastahili hata kwa kazi zote anazozifanya kwa moyo na kujitoa pamoja na umri wake wa utu uzima. Juzi tu kaongoza kwa moyo kabisa akishirikiana na waziri Muhongo juhudi za kuleta bomba Tanzania.
Huenda kuna watu ambao wanaona ukaribu wa Mahiga kama mmoja wa washauri wa kutegemewa wa Magufuli ni hatari katika kupenyeza ushawishi wao na kwa mwendo huu huenda wakamkatisha Waziri Mahiga tamaa na akaamua kuacha kazi.. Ni muhimu kuwafanyia staha wasaidizi wa karibu.