Siamini kama Jitihada zinazofanywa na Nape kuhusu kuhujumu matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni ni maamuzi yake na kwamba hayana baraka za Rais John Pombe Magufuli.
Mwanzoni tatizo lilionekana ni kubana matumizi ya TBC, ikaonekana sawa, TBC waache wazime kuonyesha live, Star TV na Azam TV wakaendelea kuonyesha.
Baadaye, ikajitokeza taasisi isiyo ya serikali ikajitolea kulipia matangazo hayo, maana yake kwamba tatizo la budget lilitatuliwa.
Baada ya kuona hivyo, Nape anakuja na ajenda mpya na kusema Bunge litakuwa na TV yake, na kwamba vyombo vingine vyote vinavyotaka kuonyesha matangazo ya bunge ya-copy kutoka kwenye TV hiyo ya bunge. Hii inadhihirisha kwamba tatizo halijawahi kuwa gharama za uendeshaji, bali kunyima wananchi uhuru wa kujipatia habari ya moja kwa moja kutoka bungeni.
Mimi naamini haya ni maandalizi ya kuja kufanya mambo mabaya zaidi hapo mbele ambayo serikali inauhakika haitaki yaonekane kwa wananchi.
Naomba kwa wenye uwelewa zaidi, watueleze sisi wananchi tunawezaje kupinga kitendo cha kiongozi/viongozi kutunyima haki yetu ya msingi ya kuoata habari! Je, wabunge wetu hawana jinsi ya kukataa maamuzi haya? INAUMA SAAANA.