G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,704
- 36,458
Huwezi kumleta waziri mkuu wa Ethiopia kwa gharama za walipa kodi kisha mkajadili Ethiopia kuanza kutumia bandari ya Dar es Salaam jambo ambalo ni ndoto ya mchana.
Huwezi kumleta mfalme wa Morocco nchini kwa gharama za walipa kodi na jinsi tulivyobanwa na haya makodikodi kisha mkajadili eti Morocco kujenga msikiti wa kisasa jijini Dar es Salaam wakati misikiti iliyopo hata waislamu hawajazi!
Anakuja kiongozi wa India kwa mwaliko wa serikali kisha agenda kuu inakuwa ni kufungua soko la dengu na choroko kutoka Tanzania kwenda India wakati ukienda ghala la hifadhi ya chakula la taifa hutakuta hata kikombe kimoja cha hayo mazao. Huku siyo kupoteza muda na rasilimali za watanzania?
Hawezi kuletwa nchini rais wa Congo kisha tukaanza kumuomba atumie tena bandari ya Dar es Salaam na kumpa grace period ya kupitisha mizigo bure kwa mwezi mzima na wakati huohuo unarudi bandarini na kuweka vikwazo vilevile sasa umefanya nini? Mbona enzi za Kikwete hakuwahi kufanya hivyo na Congo DRC walikuwa wanapanga foleni pale bandarini?
Kwa ufupi mwaliko wa viongozi wengi nchini ndani ya awamu hii ya tano wameishia kulitia hasara taifa kwa kugharamiwa kodi za wananchi bila tija yoyote ile.
Hivi kweli waziri mkuu wa Ethiopia alienda bandarini kuangalia fursa ama kutalii na kujionea mamia ya makontena yakiwa yanepigwa "government seal? "
Rais wetu afikirie na kutafakari sana aina ya viongozi wanaokuja nchini na agenda za kuongea nao! Huwezi kumuomba Morocco akujengee uwanja mkubwa kuliko ule wa taifa nchini mwako wakati yeye bado anasaka fursa za kuandaa kombe la dunia kwa kuwa kikwazo chake ni kutokuwa na viwanja bora na vya kisasa! Kamwe tusitarajie njozi zetu kuwa kweli.