Rais Duterte apiga mkwara mzito asema nitaichoma moto umoja wa mataifa endapo nikienda USA

py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,476
4,447
Rais mtata wa Ufilipino Rodrigo Duterte ametishia kuchoma moto makao makuu ya UN yaliyopo Newyork.

"Nenda na kafungue shitaka umoja wa mataifa ,nitaichoma moto umoja wa mataifa kama unataka-alinukuliwa Durtete na jarida la Newyork times.

" Nitaichoma na kuhakikisha inaungua yote endapo nikienda USA

Siku ya Alhamisi pia Duterte alinukuliwa akimuita afisa wa juu wa UN Zeid Hussein mpumbavu na mtoto wa kahaba mara baada ya afisa huyo kutishia atafungua uchunguzi dhidi ya Duterte kuhusiana na mauaji aliyofanya pindi akiwa mayor wa Davao

"Huyu jamaa zeyd ni mchekeshaji na kichaa na ni mpumbavu

" Nyie maofisa wa UN mnaokalia matako yenu hapa,huku tukiwalipa mishahara .Nyie wapumbavu msinielekeze na kunifundisha nini chakufanya ..ni nani aliyewapa mamlaka hayo?alihoji Duterte

Tafadhali fungeni midomo yenu "shut up" sababu akili zenu zimekosekana hapa.

"Rudini shuleni.Nyie umoja wa mataifa hamfahamu diplomasia.Hamfahamu namna ya kujiheshimu kama wafanyakazi wa umoja wa mataifa.

" Hamuwezi kuzungumza na Mimi namna hivyo Nyie watoto wa makahaba "sons of bitch'' -aliongezea Duterte

Wiki iliyopita rais Duterte alithibitisha kuwa yeye binafsi alikuwa anawaua watuhumiwa wa uhalifu pindi alivyokuwa Mayor

" Nilivyokuwa Davao nilikuwa nawaua wahalifu kwa mikono yangu.Nilikuwa ninawaonyesha polisi kama mimi naweza Nyie mnashindwaje.Nilikuwa natembea mtaani na pikipiki kuwatafuta wahalifu ,nilikuwa napiga patrol kutafuta matatizo na pia nilikuwa natafuta nani wakunikabili ili ni muue
8379342e92d97547e9faa526bd07de7e.jpg
 
Back
Top Bottom