Rais Dr Magufuli: Hata Ikulu wasipolipa Bili ya Umeme TANESCO ruksa kukata umeme

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,358
Rais akiwa ktk ziara huko Mkoa wa Mtwara kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya umeme ametoa maagizo kuwa hata Ikulu wasipo lipa Bill ya umeme basi Tanesco ruksa kukata umeme.

Hata ikiwa ni Jeshini,Polisi au ofisi yoyote ya umma Tanesco wakate umeme tu. Hata Zanzibar ambako wanadaiwa kama hawajalipa deni lao wakatiwe umeme tu. Amesisitiza kuwa ameongea maneno haya mchana kweupe.

Kila Wizara na Ofisi za umma walipe bill zao za umeme kwasababu pesa ya malipo ya umeme inatengwa kila mwaka. Tanesco wasimuogope yoyote yule ktk kukata umeme.

Amemsifu Waziri Prof Mhongo na timu yake kwa kazi nzuri ktk kusambaza umeme hasa vijijini.



Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli ametoa agizo kwa uongozi wa tanesco kukata umeme kwa Wizara au taasisi yoyote inayokwepa kulipa bili za umeme.

Mh Rais ameyasema hayo leo katika ziara yake ya kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa umeme wa msongo wa Kv 132 Mtwara " Tanesco pasitokee taasisi ama Wizara hata Ikulu isipolipa umeme we kata tu, hatuwezi kujiendesha kwa hasara wakati kuna watu wanakwepa kulipia gharama" wakati serikali inatoa ruzuku zake humu sasa ni wakati Tanesco ijiendeshe kwa faida.

Aidha Mh Rais ameonya tanesco kutoingia mikataba ya hovyo na makampuni ya nje yanayokuja kwa ujanja na alisema kampuni ikitaka kuja kuwekeza umeme nchini basi waje wazalishe umeme wao na wauze tanesco na wasitegemee umeme huu kufanya ujanja ili kutorudia mikataba mibovu kama symbion na makampuni mengine

Chanzo: TBC LIVE
 
NINAMUUNGA MKONO MH RAIS KWA HILI..HATA ZANZIBA WAKATIWE TU

Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli atoa agizo kwa uongozi wa tanesco kukata umeme kwa Wizara au taasisi yoyote inayokwepa kulipa bili za umeme, Mh Rais ameyasema hayo leo katika ziara yake ya kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa umeme wa msongo wa Kv 132 Mtwara " Tanesco pasitokee taasisi ama Wizara inayokwepa kulipa umeme wasipolipa we kata tu, hatuwezi kujiendesha kwa hasara wakati kuna watu wanakwepa kulipia gharama" wakati serikali inatoa ruzuku zake humu sasa ni wakati Tanesco ijiendeshe kwa faida, Aidha Mh Rais ameonya tanesco kutoingia mikataba ya hovyo na makampuni ya nje yanayokuja kwa ujanja na alisema kampuni ikitaka kuja kuwekeza umeme nchini basi waje wazalishe umeme wao na wauze tanesco na wasitegemee umeme huu kufanya ujanja ili kutorudia mikataba mibovu kama symbion na makampuni mengine

Chanzo: TBC
 
NINAMUUNGA MKONO MH RAIS KWA HILI..HATA ZANZIBA WAKATIWE TU
Mkuu kuhusu taasisi kukatiwa umeme mimi siungi mkono maana taasisi zinazoongoza kwa Madeni ni za serikali mfano mashule ya bording Wanacheleweshewa ruzuku watalipaje kwa wakati maana nakumbuka wakati nasoma a level mpaka ilikuwa inafika mkuu wa shule anatoa hela yake mfukoni kununua umeme ruzukj ikija ndo areplace Mungu ampe maisha marefu mwalimu yule
 
Hili ni sawa. Tena serikali iwalipe on time hata wafanyabiashara wote ambao wametoa huduma kwa serikali
 
Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli atoa agizo kwa uongozi wa tanesco kukata umeme kwa Wizara au taasisi yoyote inayokwepa kulipa bili za umeme, Mh Rais ameyasema hayo leo katika ziara yake ya kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa umeme wa msongo wa Kv 132 Mtwara " Tanesco pasitokee taasisi ama Wizara hata Ikulu isipolipa umeme we kata tu, hatuwezi kujiendesha kwa hasara wakati kuna watu wanakwepa kulipia gharama" wakati serikali inatoa ruzuku zake humu sasa ni wakati Tanesco ijiendeshe kwa faida, Aidha Mh Rais ameonya tanesco kutoingia mikataba ya hovyo na makampuni ya nje yanayokuja kwa ujanja na alisema kampuni ikitaka kuja kuwekeza umeme nchini basi waje wazalishe umeme wao na wauze tanesco na wasitegemee umeme huu kufanya ujanja ili kutorudia mikataba mibovu kama symbion na makampuni mengine

Chanzo: TBC LIVE
Sawa kabisa naunga mkonyo hoja.
 
Kuna walimu huwalea wanafunzi kama watoto wao.....Mungu awabariki sana
Mkuu kuhusu taasisi kukatiwa umeme mimi siungi mkono maana taasisi zinazoongoza kwa Madeni ni za serikali mfano mashule ya bording Wanacheleweshewa ruzuku watalipaje kwa wakati maana nakumbuka wakati nasoma a level mpaka ilikuwa inafika mkuu wa shule anatoa hela yake mfukoni kununua umeme ruzukj ikija ndo areplace Mungu ampe maisha marefu mwalimu yule
 
Rais akiwa ktk ziara huko Mkoa wa Mtwara kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya umeme ametoa maagizo kuwa hata Ikulu wasipo lipa Bill ya umeme basi Tanesco ruksa kukata umeme.

Hata ikiwa ni Jeshini,Polisi au ofisi yoyote ya umma Tanesco wakate umeme tu.

Hata Zanzibar ambako wanadaiwa kama hawajalipa deni lao wakatiwe umeme tu.

Amesisitiza kuwa ameongea maneno haya mchana kweupe.

Kila Wizara na Ofisi za umma walipe bill zao za umeme kwasababu pesa ya malipo ya umeme inatengwa kila mwaka.

Tanesco wasimuogope yoyote yule ktk kukata umeme.

Amemsifu Waziri Prof Mhongo na timu yake kwa kazi nzuri ktk kusambaza umeme hasa vijijini.
Presidential Affairs Act-sheria inayoongoza taasisi ya urais hairuhusu
 
Back
Top Bottom