Rais aweka msimamo mpya wa sera za nje za Tanzania!?

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
36,141
29,670
Ni jukumu letu kama wanaJF na watanzania wazalendo kuielimisha jamii kwa kuleta mijadala yenye afya na ile ya kufikirisha.

Tuachane na umbea kutoka kwa bloggers waliothariwa na background mbaya za utotoni mwao.

Tuachane na tabia ya kushare udaku wa Instagram na badala yake tujadili matamko na hoja critically!!

Leo hii katika uzinduzi wa hostels za wanafunzi wa UDSM zilizojengwa kwa ufanisi na kwa bei nzuri nimemsikia mheshimiwa Rais akiongelea faida mojawapo kati ya nyingi za Tanzania kufungua ukurasa mpya wa kidiplomasia na Israel...hapa nimemsikia Rais akitaja idadi kubwa(watalii 600) ya watalii kutoka Israel Taifa la Mungu waliokuja kutembelea Tanzania mara baada ya kuhuisha uhusiano wetu wa kibalozi na Israel.

Rais ameendelea kuasa kuwa mwenendo wa kidunia wa sasa tunahitaji marafiki wengi zaidi ya maadui kwa maslahi ya nchi yetu.

Amesisitiza kuwa kazi ya ukombozi tuliifanya sana kiasi cha kusahau maendeleo yetu.

Kwa sasa Tanzania haina haja ya kushikilia misimamo isiyo na tija bali misimamo itakayotujengea marafiki wengi zaidi.uadui wa kati ya nchi zao usiwe uadui wetu.

KWA MAONI YANGU RAIS AMEWEKA MSIMAMO MPYA LAKINI KWA MUKTADHA ULEULE WA NON ALIGNMENT MOVEMENT...ILA KWA SASA NCHI IJIKITE KATIKA KUANGALIA MASLAHI YAKE KWANZA !


KUMBUKUMBU:Rais alimkaribisha mfalme wa morroco huku msimamo wa Tanzania kuhusu Polisario ukibakia vilevile...tendo hili limefanya morroco kuingizwa kwenye umoja wa Africa na pengine kulegeza msimamo wake dhidi ya Polisario(wataalamu na wafuatiliji watagundua hili)



kwa wadau wenye weledi wa ki-great thinker njooni tujadili.

Cc: nguruvi @pasco Mzee Mwanakijiji Lizaboni

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Viongozi wetu kila kukicha wanadai "wanamuenzi mwalimu kwa vitendo",hili ni la mwalimu,kulikoni kupingana nae kabla jogoo hajawika mara tatu?
 
Naomba kuuliza hivi hakuna chombo cha kimataifa kinachoweza kuishinikiza hii nchi yetu kufanya uchunguzi dhidi ya upotevu wa Ben Saanane? Basi kama hawawezi hilo watusaidie kuhakiki PhD. Watusaidie kyfahamu kama mfumo wa elimu ya juu udsm unafuatwa au wajanja wachache wana short - cut zao.


"Samahani mama kanambia bado mdogo "

Ngoja nikae kimya.
 
Naomba kuuliza hivi hakuna chombo cha kimataifa kinachoweza kuishinikiza hii nchi yetu kufanya uchunguzi dhidi ya upotevu wa Ben Saanane? Basi kama hawawezi hilo watusaidie kuhakiki PhD. Watusaidie kyfahamu kama mfumo wa elimu ya juu udsm unafuatwa au wajanja wachache wana short - cut zao.


"Samahani mama kanambia bado mdogo "

Ngoja nikae kimya.
Nenda Instagram utapewa majibu na yule mdaku.
 
Watakuwa wameipata turudi kwenye hoja mkuu
Uchwara diplomasia yake imebobea kwenye utekaji na umbali wa futi 6 kuwazika wanaomkosoa.

Hata baraza lake la mawaziri wenyewe kwa wenyewe hakuna dalili za diplomasia; na kwenye chama fukuza fukuza za kibabe.

Diplomasia Bashite style kweli kabobea
 
Kwa mtizamo wa Mtukufu hata angelikuwa Idd Amini bado anatawala Uganda na kufanya mambo yake tulipaswa kunyamaza na kutafuta urafiki naye
Nahisi Kuna mikono ya Kagame na Museveni tuondoke Kongo
 
Uchwara diplomasia yake imebobea kwenye utekaji na umbali wa futi 6 kuwazika wanaomkosoa.

Hata baraza lake la mawaziri wenyewe kwa wenyewe hakuna dalili za diplomasia; na kwenye chama fukuza fukuza za kibabe.

Diplomasia Bashite style kweli kabobea
Unaelewaje kuhusu diplomasia...mambo ya utekaji yana threads zake nyingi sana humu jamvini...rudi kwenye hoja bwa mdogo!
 
Mimi naona msimamo wa Rais ni muafaka kwa wakati huu. Kama umemsikiliza vzr amesema tuangalie maslahi ya nchi kwa sasa. Uhasama kati ya Parestina na Israel unatuhusu nini kama watanzania? Au Uhuru wa Sahara magharibi unatuhusu nini mpaka tumchukie Morocco?

Tumepoteza ndugu na Mali na tumechelewesha maendeleo yetu kwa kutumia raslimali nyingi na muda ktk ukombozi kusini mwa Afrika. Mapungufu mnayoyaona Mikoa ya kusini kwa Tz ni matokeo ya kuunga mkono Flerimo Msumbiji. Tujiulize baada ya Uhuru wa Msumbiji tumefaidi nini kama watz, Mwalimu was right at that time, walidhani Afrika ni moja na kulikuwa na matumaini ya kuunganisha afrika lakini kwa sasa ni wazi kuwa kwa sasa ni kitu kisichowezekana hatutakiwi kurudia makosa, ebu tuwe Rafiki wa yeyote kwa kuangalia maslahi ya nchi. Long live my President JPM
 
Kwa mtizamo wa Mtukufu hata angelikuwa Idd Amini bado anatawala Uganda na kufanya mambo yake tulipaswa kunyamaza na kutafuta urafiki naye
Nahisi Kuna mikono ya Kagame na Museveni tuondoke Kongo
Mkuu naungana na mheshimiwa Rais...kama congo hatuna maslahi napo tuondoke tu.Rwanda na Uganda wapo Congo kwa maslahi gani??
 
Ila kweli ilikuwa ni ujinga kwa mfano Morocco inagombana na nchi gani huko sisi tunakata urafiki na Morocco.

Israeli inagombana na palestina huku tunachukia. Ili iweje?
Hahahaa,kwahyo Nyerere alikuwa mjinga sio?
 
Hahahaa,kwahyo Nyerere alikuwa mjinga sio?
Kwa kipindi kile na nyakati zile alikuwa sahihi...je unaongeleaje kwa nyakati hizi?je nchi tulizozikomboa na nchi za afrika kwa ujumla bado zinakubaliana na mawazo ya viongozi wa enzi zile?

Je msimamo wa Magufuli kwa sasa ni sahihi?
 
Back
Top Bottom