Rais aunda Tume ya kuchunguza Operation tokomeza

Rais aunda Tume ya kuchunguza Operation tokomeza

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,056
Reaction score
10,729
Hatimae Raisi Kikwete ameunda Tume ya Uchunguzi (Inquiry Commission) ya Kuchunguza madhara yaliyoletwa na Operation Tokomeza.

Tume hii inayoundwa na wanasheria kwa sehemu kubwa itaongozwa na JAJI na BALOZI Mstaafu HAMISI AMIR MSUMI.

Uteuzi huu umeanza rasmi Alhamisi tarehe 01/05/2014.

Baadhi ya majukumu ya Tume ni;

(1) Kuchunguza na Kubaini iwapo wapo watu wowote waliokiuka sheria na kanuni utekelezaji operesheni hiyo.

(2) KUPENDEKEZA Hatua za kinidhamu na Kisheria dhidi ya wote watakaobainika kukiuka sheria na kanuni zilizostahili katika uendeshaji wa zoezi zima.

SOURCE, KATIBU KIONGOZI - IKULU

My Take,
Nimefurahishwa sana na namba mbili (02) Hapo juu iwapo matokeo yake yataheshimiwa!
------------------------------------------------------------------------------------------

Rais aunda Tume kuchunguza mwenendo wa Operesheni Tokomeza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameunda Tume ya Uchunguzi (Commission Inquiry) Kuhusu Vitendo vilivyotokana na Uendeshaji wa Operesheni Tokomeza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam jioni ya leo, Ijumaa, Mei 2, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Rais ameunda Tume hiyo kwa mujibu wa kifungu cha tatu cha Sheria ya Uchunguzi Sura ya 32.

Kutokana na hatua yake ya kuunda Tume hiyo, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji na Balozi Mstaafu Hamisi Amiri Msumi kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.

Aidha, Rais Kikwete amewateua Mheshimiwa Jaji Mstaafu Stephen Ernest Mtashiwa Ihema na Mheshimiwa Jaji Mstaafu Vincent Kitubio Damian Lyimo kuwa Makamishna. Rais pia amemteua Ndugu Frederick Manyanda, Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa Katibu wa Tume hiyo.

Taarifa ya Balozi Sefue inasema kuwa uteuzi huu ulianza jana, Alhamisi, Mei Mosi 2014.

Taarifa ya Balozi Sefue iliyataja majukumu ya Tume hiyo yatakuwa yafuatayo:

Kuchunguza na kubaini Operesheni Tokomeza ilivyoendeshwa.
Kuchunguza na kubaini iwapo Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu za Rejea zilifuatwa na watu waliotekeleza Operesheni Tokomeza.
Kuchunguza na kubaini iwapo yupo mtu yeyote aliyekiuka Sheria, Taratibu na Hadidu za Rejea wakati wa Operesheni Tokomeza.
Kuchunguza na kubaini kama wapo watu wowote waliokiuka Sheria yoyote wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza na kupima kama hatua zilizochukuliwa dhidi yao au mali zao zilikuwa stahiki.
Kupendekeza hatua zozote zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kukiuka Sheria, Taratibu na Hadidu za Rejea za Operesheni Tokomeza.
Kupendekeza mambo ya kuzingatiwa wakati wa kuandaa na kutekeleza operesheni nyingine siku zijazo ili kuepuka kasoro.
Uteuzi huo wa Tume hiyo unatekeleza ahadi ya Rais Kikwete ambayo aliitoa wakati anahutubia Bunge Novemba 18, mwaka jana, 2013 mjini Dodoma.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.



2 Mei, 2014
 
Hatimae Raisi Kikwete ameunda Tume ya Uchunguzi (Inquiry Commission) ya Kuchunguza madhara yaliyoletwa na Operation Tokomeza.

Tume hii inayoundwa na wanasheria kwa sehemu kubwa itaongozwa na JAJI na BALOZI Mstaafu HAMISI AMIR MSUMI.

Uteuzi huu umeanza rasmi Alhamisi tarehe 01/05/2014.

Baadhi ya majukumu ya Tume ni;

(1) Kuchunguza na Kubaini iwapo wapo watu wowote waliokiuka sheria na kanuni utekelezaji operesheni hiyo.

(2) KUPENDEKEZA Hatua za kinidhamu na Kisheria dhidi ya wote watakaobainika kukiuka sheria na kanuni zilizostahili katika uendeshaji wa zoezi zima.

SOURCE, KATIBU KIONGOZI - IKULU

My Take,
Nimefurahishwa sana na namba mbili (02) Hapo juu iwapo matokeo yake yataheshimiwa!

Pongezi kwa jk, Sasa tunaomba pia tume ya mauaji katika mkutano wa CDM Arusha iundwe. Wale nao ni watanzania!
 
Si ajabu Taarifa ya Tume hii inaweza pia kupata mashambulizi kama ile ya Mzee Warioba! Tanzania kila kitu kinawezekana. Tume ya jaji Kisanga pia ilipigwa teke na Mkapa.
 
Kaka kuunda tume sio kazi kazi ni kutekeleza maoni na mapendekezo ya matokeo ya Tume! Iliundwa tume ya katiba hapa kwa mbwembwe ila furaha yote ikawa shubiri kwa walewale walioiteuwa tume baada ya maoni na matokeo ya tume kuwa kinyume na matakwa ya watawala! So let's keep watching the series, tusije kustaajabu huyo huyo Jaji Hamis Amir Msumi akaja kuitwa msaliti
 
Dhumuni la kuanzisha operesheni ndio basi tena!!!!
 
Wasije wakapopolewa na mawe kama Judge Warioba na Team yake,hasa ukizingati Serikali yetu sikivu haipendi kuambiwa ukweli.Kupokea kazi ni wajibu,lakini wajumbe wa kamati hiyo msitegemee outcome ya kazi yenu ipokelewe kama mtakavyofikiri.Poleni.
 
tume sishaundwa nyingi hakuna hata tume moja iliyotoa majibu na wala sijawahi sikiaaa au ona hao watu wakichukuliwa hatuaaa.....wanapoteza tu helaaaa za kodi
 
Rais anapoteza muda na pesa za walipa kodi kwa kuunda viini macho vya tume zisizo na tija pasipo yeye binafsi kuwa na dhamira ya kweli ya kutatua matatizo.
 
Back
Top Bottom