ambaye hajui atakaye shinda labda ni wewe tu, na ni unafiki! Raisi atakuwa ni Raila Amolo Odinga (Mjaluo) na hii imekaa kimkakati zaidi; Odinga ameshafikisha na kupitiliza ile miaka 70 ya biblia ya kuishi, na kwa anavyosinzia hata mbele ya hadhara za watu (wapigakura); automatically raisi ajaye kabla ya miaka mitano kwisha atakuwa Martha Karua (Mkikuyu). Baba kwa umri alionao hataweza kuhimili mikikikiki ya ikulu zaidi ya miaka mitatu, atapumzika mwenyewe au kupunzishwa na system. HIVYO HISTORIA YA KITI CHA URAISI KUWA KWA WAKIKUYU ITAENDELEA, MOI ALIKUWA RAISI AKIMSUBIRIA UHURU AKUE.
Endelea kukataa, lakini Raila (Mjaluo) atatangazwa kuwa raisi si kwa sanduku la kura bali ili amshikie Martha Karua (Mkikuyu). Akishinda Dr. Ruto (Mkalenjini), na ifluence yote ya Uhuru aliyoweka, Kenya mtakuwa mwalimu wa demokrasia afrika na duniani. Nitakuja hapa na kuanzisha uzi wa ukubwa wa demokrasia ya kenya.Wapiga kura ndio wenye maamuzi ya nani awe rais, hizi nadharia unaandika humu zilipaswa wakati wa kampeni, ila leo tunaingia kila mmoja kwenye kijisehemu cha siri kufanya maamuzi bila shinikizo lolote.
hamna mchezo, kenya hawajafikia level hiyo ya ujasusi wa kisiasa, anachokifanya kenyatta ndiyo anachokiamini, anamwona Ruto ni tishio kwake na masilahi ya kabila lake kwa ujumla.MCHEZO WALIOCHEZA KENYATTA NA RUTO NI BALAAAA.Mutashangazwa na Matokeo
Endelea kukataa, lakini Raila (Mjaluo) atatangazwa kuwa raisi si kwa sanduku la kura bali ili amshikie Martha Karua (Mkikuyu). Akishinda Dr. Ruto (Mkalenjini), na ifluence yote ya Uhuru aliyoweka, Kenya mtakuwa mwalimu wa demokrasia afrika na duniani. Nitakuja hapa na kuanzisha uzi wa ukubwa wa demokrasia ya kenya.
Katika demokrasia ya uchaguzi Tanzania na Kenya ni ndugu hamna wa kumcheka mwingine, Tanzania kuna UCCM na Kenya kuna ukabila, Kabila ni kigezo kikubwa cha mshindi wa Raisi wa kenya na Tanzania Chama ni kigezo kikubwa cha uraisi. Ni mpumbavu ndiye atakayefikiri kenya kuna demokrasia kuliko Tanzania.Hamna sehemu nimekataa au kukubali maana uwezo huo wanao Wakenya nikiwa mmoja tu wa wapiga kura, naelewa ni kitu haujakizoea Tanzania maana huko kwenu kuna wazee hukusanyika pale Dodoma kumchagua atakayegombea kwa tiketi ya CCM, panafanyika figisu za kila aina, ila akishachaguliwa mmoja wa CCM, basi huyo ndiye rais, mengine yanakua maigizo tu, kwamba hata akizunguka nchi yote akifanya maigizo ya push up, ana uhakika wa kuukwa urais.
sasa atashinda kwa sababu anaungwa mkono na wakikuyu kwa masilahi yao FULL STOP hamna jipya, na akibadilika wakikuyu watamfanyia kitu mbaya ili raisi awe MarthaHata hivyo ameshashindwa mara nyingi, sababu zilizomfanya akataliwe na Wakenya ameshazirekebisha?
Sent using Jamii Forums mobile app
Umebugi this time around. Usipende kukariri inaonekana hata siasa za Kenya hujui unadandia dandia tu. Raila is the PresidentRaila hawezi kamwe kushinda nafasi ya urais, ninakuhakikishia!
Acha ufala ww ina maana hata siasa za kwenu huzijui!!!!?Ndio utamu wa demokrasia, yaani nchi yote hakuna mwenye uhakika nani atashinda, ila atakayeshinda nitakua wa kwanza kumpongeza humu JF hata kama sikumpigia......tuishi kiuzalendo na kumpa ushirikiano.
Hakuna kitu kama hichoMCHEZO WALIOCHEZA KENYATTA NA RUTO NI BALAAAA.Mutashangazwa na Matokeo
Katika demokrasia ya uchaguzi Tanzania na Kenya ni ndugu hamna wa kumcheka mwingine, Tanzania kuna UCCM na Kenya kuna ukabila, Kabila ni kigezo kikubwa cha mshindi wa Raisi wa kenya na Tanzania Chama ni kigezo kikubwa cha uraisi. Ni mpumbavu ndiye atakayefikiri kenya kuna demokrasia kuliko Tanzania.
Nina uhakika. Kuna ma spin master wameshamaliza mchezo. Siasa za Tanzania sisi kila mgombe wa CCM lazima ashinde ila Kenya ni ballots 🗳 inaamua hata kwa mtu kufa ila kura zitimie siyo kama TanzaniaUmebugi this time around. Usipende kukariri inaonekana hata siasa za Kenya hujui unadandia dandia tu. Raila is the President
katika awamu ya pili ya mwai kibaki mbona alishindwa na akatangazwa kuwa mshindi? yote yanawezekanaHamna kabila moja linaloweza kumchagua rais, tuna makabila zaidi ya 40, hivyo lazima ushawishi sana, pia katiba imeweka wazi ushindi sio wingi wa kura tu, lazima ushinde kwenye idadi ya gatuzi zinazokidhi na kuonyesha umependwa na asilimia kubwa ya Wakenya kutoka matabaka mbali mbali.
Bahati mbaya yake wakenya umri hauwahusu wao wanaangalia makabila yao.Umri umeenda na Kenya vijana ni wengi watampa tu Hustler