VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Dharau kwa Rais haziruhusiwi. Ni marufuku kuu. Rais ni mamlaka kuu kuliko zote nchini. Yuko juu ya zote. Anayemdharau kimaneno au kimatendo hatabaki salama. Hasa anayekiuka amri za Rais.
Muda si mrefu,Rais alifuta vibali vya mashamba makubwa Arumeru. Ni mashamba ya mwekezaji huko. Kufutwa huko kuliendana na kuagizwa kugawiwa kwa mashamba hayo kwa wananchi ili waendeshe shughuli zao. Za kimaisha. Ilikuwa ni amri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Leo imeripotiwa ITV kuwa Mwekezaji amemdharau Rais. Ameuza baadhi ya ekari zilizofutiwa hati yake. Ameuza kwa wawekezaji mbalimbali. Ameuza baada. Halafu,askari wamekutwa wakilinda eneo husika. Difenda mbili. Wanalinda Rais kupuuzwa!?
Hakika,kuna watu lazima wawajibishwe. Kuanzia mwekezaji hadi askari. Rais lazima aheshimiwe!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.