Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Polisi nchini Uhispania wamemtia mbaroni mtaalam wa kompyuta kutoka Urusi kwa madai ya kudukua mitandao wakati wa uchaguzi marekani, habari kutoka vyombo vya habari vya Uhispania vimesema.
Pyotr Levashov, ambaye alishikwa tarehe 7 Aprili, kwa sasa amewekwa rumande.
Shirika la habari la AFP pia ilijulishwa kwamba Marekani ilikuwa imetoa ombi la Levashov kurudishwa nchini humo.
Ombi hilo litapelelezwa na mahakama ya jinai ya Uhispania, AFP iliongezea.
El Confidencial, tovuti ya habari Uhispania ilisema kuwa hati ya kukamatwa kwa Levashov ilitolewa na Marekani kwa kile kilichokisiwa kuwa kudukua mitandao hatua iliodaiwa kusaidia kampeni ya Trump.
Chanzo: BBC