Rai yangu kwa vijana kuhusu hotuba ya rais JPM

baba stive

Member
Mar 10, 2016
11
10
RAI YANGU KWA VIJANA

Juzi Mh DK J.P. MAGUFuLI baada ya
kuwahutubia wakuu wa mikoa kwa kuwaasa
wakajitahidi vijana hawachezi pool table Na kukaa
vijiweni mida ya asubuhi bila kazi (wapie vita
uzembe) lakini kumekua Na watu wanaotoa
mitazamo dhaifu kupinga hoja nzito. "Kuna
waliosema JPM angetengeneza ajira kwanza kwa
ajili ya vijana",wengine mashamba hayawezi
kulimwa kwa jembe la mkono, Na wengine
wakazidisha utani kuwa fani walizosomea sio za
kwenda shamba hvyo wapelekwe sehemu husika.
Nkakaa Na kutafakali inakuaje watanzania
tunawaza kwakutumia mdomo kila kitu mpaka
tufanyiwe Na serikali Leo hii unamkuta kijana
mwene nguvu Na vyuma anapiga amekaa tu
maskani hata kutafuta kazi ya ulinzi hawazi Na
huyo ni darasa la saba au form four failure
anakaa Na kusema ipo siku atatoka utatokaje
hutaki hata kuchoma mihogo mtaani kwenu? Au
Luna muujiza wa kufanikiwa bila kujituma katika
kazi?
Kuna ambao wamehitimu vyuo mbalimbali nchini
sasa hawa ndio aibu ooh rais hatuna ajira
tumesoma hatuwezi kufanya kazi nje ya
tulichokisoma. Hawa ndio wamegoma hata kurud
kwao wanaishi kwa kubeti Na kucheza pool table
Na kamali za aina nyingi huku wakisubili kuajiliwa
miaka isiojulikana lakini atakaa hvyo hadi miaka
3-5 ndio maisha yake ukimwambia basi Kauze
hata magazeti hayupo tayari huyu baada ya
muda mfupi lazima awe jambazi
Nilichogundua watanzania akili zetu zimelala
hatuwazi kipi tukifanye kutusaidia binafsi badala
yake tunaisubili serikali ije itusaidie Na tumezoea
kulalamika bila sababu ni aibu iliyoje kijana Na
nguvu zako kukaa bila kuzalisha hata shilingi
2000 kwa siku Na hauna majukumu Na pia
tushatambua kuwa Elimu tunayoipata haituandai
kujiajili basi badala ya kukaa Na kusikiliza miziki
Na kuangalia series zisizoisha kaa uangalie CDs
za kujifunza kujiajili lakini yote hayo hatufanyi Na
tunawaza kusaidiwa hata biashara za mtaji wa
50000 elfu au mtaji wa nguvu zako unakosa hii ni
aibu kwa vijana hebu tujifunze kuwajibika sisi
huku hatuwajibiki tumekaa tu Na hatuzalishi
chochote lakini ni wepesi kulaumu viongozi
hawawajibiki bila kujiuliza kuwa sisi tumefanya
nini kwa ajili ya nchi yetu? Wakati mwingine
tunajisababishia umaskini kwa kuwaza ujinga wa
kusubili serikali wakati mkiunda umoja wenu
vijana hata kumi sector binafsi zitawadhamini lkn
kwakua akili zetu ni fupi tutabaki waita vijana
wenzetu kuwa ni ma Freemason kwa kupata pesa
wakiwa wadodo
By
Melkizedeck Bashingwa
Mtanzania
 
Back
Top Bottom