Rai yangu kwa Rais Magufuli kuhusu uchumi na wananchi wa kawaida

kababu

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,699
804
Kwanza nianze kwa kumpongeza rais wangu kwa hatua anazochukua za kupambana na rushwa na ufisadi na pia kuwasaidia wananchi wanyonge ila kwenye uchumi ujafanya vizuri kwani mzunguko wa ela umepungua sana mtaan na hili hapa linaweza kuwa suluhisho,

1. Naomba upunguze kodi kero bandarini ambazo zinafanya wafanyabiashara kukimbilia bandari za jirani. Mfano, tutaweza kukusanya kodi kubwa sana, tukiweza kufanya bandari zetu ziwe busy kutakuwa na ajira nyingi sana, compuny za clearing and forward zitaajiri wafanyaka na pia zitaongezeka, malori ya kubeba mizigo ya yatakuwa mengi hivyo ajira kupatikana kwa madereva, wauza vipuri etc, malori ya kusafisha yatatumia mafuta kwa wingi hivyo serikali itakusanya kodi nyingi sana kutokana na mafuta, road fees etc

2. Serikali ijitahidi kulipa madeni kwa supplier wao. Sisi ambao tunafanya kazi na serikali tunateseka sana kwani tumeshindwa kurudisha mikopo, kulipa wafanyakazi mishahara, kuliapa kodi za serikali pia tunashindwa, tunateseka kwa kweli hali ni mbaya, tumekuwa tunauza hadi nyumba zetu ili tuweze kuaccomodate credit with gvnt,
Saidia rais saidia, mfano, ni kama ulivyotembelea vyombo vya uhuru publication jinsi wanavyoudai serikali mpaka wanashindwa kulipa mishahara, hata sisi wafanyabiashara ambao tunaofanya kazi na serikali tunateseka kwa kweli tunaomba serikali ilipe madeni ili na ss tuweze kulipa mishahara wafanyakazi na wao waweze kulea familia zao

3. Serikali itoe kodi kero kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kwani hawa wafanyabiasha wadogo wanajiajiri wenywe kutokana na ukweli kumba serikali haiwezi kumwajiri kila mtu, mfano mtu unakuta anayo mtaji wa 300,000/= unaenda tra wanakukadiria malipo ya kodi kwa mwaka ili iweze kukupa tax clearance sh. 361,000/ na bado hapo ujapata lessen ya biashara manispaa, tuhurumie jamani rais, hii inatupa sisi wafanya biashara wadogo wakati mgumu kweli kweli kuweza kuanzisha biashara.

4. Serikali irudishe hela walizoamisha za mashirika ya umma kutoka benk za biashara kwenda BoT, (waziweke kwenye fixed account ili wapate faida) hii itaipa uwezo bank za biashara kuweza kukopesha wafanyabisha na mzunguko wa ela utarudi kama kwaida.


5. Serikali kupitia BoT ipunguze interest rate kwa bank za biashara na ilazimishe bank za biashara kupunguza interest rate kwenye mikopo wanayotoa

6. Rais wangu toka ndani kutuletee chakula, sisi wanao tunakufa na njaa, usiogope kuomba kwani bado sisi wanchanga hatujaweza kujitegemea, ukamwone trump akupe dollar itatusaidia, rais wangu kumbuka kuwa uwezo wetu wa kuuza nje ni mdogo hivyo ela za kigeni tunapata kwa misaada mara nyingi,rai wangu magufuli tunakutegemea na najua wewe unaushawishi mkubwa sana huko nje,

Rais wangu sikia kilio cha wananchi wako, tunateseka sana
 
Kiufupi mawazo yako hayatekelezeki...........

Hapo uliposema kurudisha pesa kwenye bank za kawaida.......

Bila kuja na solution how we will solve wastage of our tax money as a nation through FD.........

Uzi wako umenigusa sana lakini ndio hivyo is the time of one man show others we are fans.....

Watakuita mpiga dili hapo chini subiri kidogo......
 
Uzi wako Mzuri..

Ila pa kumpa ukweli mpe ukweli...

Hakuna lolote ambalo limeshafanyika kwenye kumuwezesha mwananchi maskini wa Tanzania kwenda kwenye uchumi ulio bora.. Kwenye hili umemsifia kwamba anafanya jitihada but there's absolutely nothing that has been done so far to improve that...!!

Sana sana hali za wananchi ndio zimekuwa ngumu kwelikweli.

Mengine yote ulio mshauri ni mazuri sana.

Ila kama alivyosema Mkuu Technically.. Uendeshaji wa hii Nchi kwa sasa is a one man show...

Let us watch and see.
 
Rais Mwongo

Eti ni Mtetezi wa Wanyonge..hizi ni Swaga za kisiasa ili apate umaarufu....

Kama ni Mtetezi wa wanyonge kwa nini amebariki kuondolewa FAO LA KUJITOA?

Mikopo kwa wanafunzi...Wanafunzi wengi masikini walikosa mikopo na wako nyumbani....It is pure true

Wanyonge gani anawatetea: au hao nzi wa green wanashinda kwenye mitandao kukashifu mawazo mbadala?

Mfumuko wa bei....anaumiza watanzania wa hali ya chini kwa tamaa yake ya kodi akanunue ndege

na mengine mengi

Ameshindwa kukamata mafisadi wa ESCROW, LUGUMI Na RICHMOND
 
Back
Top Bottom