Rai yangu kwa mhe Rais Magufuli

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
1,487
910
Kuwa Rais na Kiongozi mkuu wa wananchi ni Jukumu kubwa..

Usitarajie hata siku moja kwamba utasifiwa na watu wengi.. jua Malipo halali ya Kiongozi yeyote hulipwa na Mwenyezi Mungu..


Kiongozi mkuu anapoamua kuambatana na Jamii ya watu wanyonge wasio na sauti.. ni kama kujivika mabomu ni kujitosa mzimamzima.. baadhi ya maskini sio tu wana maisha na kipato duni bali hata Tabia zao zinaumiza na kuchosha. Unaweza kujitolea kuwasaidia ukitarajia watafurahi lakini ndio wa kwanza kubeza bidii zako..

Kuwatumikia Watu ni Kumtumikia Mwenyezi Mungu
Watu ni Jeuri, hawana shukrani..wakatili na hawakumbuki wema.. ila Jamii hii hii ndivyo Mwenyezi Mungu anataka tuitumikie.

Endelea na bidii .. Mbwa kubweka ni ada yao Waache wabweke. nikiusoma moyo wako na maneno yako naona una kiu ya kuwatumikia wanyonge hata mimi pia vivyo hivyo ingawa nawelewa wanyonge wenyewe ni HATARI lakini ndio kumtumikia Mwenyezi Mungu huko. JALI KUTENDA HAKI..

Najua wako watu ndani ya Chama chako wanacheza michezo michafu ya Uhuni..wanakurushia kinyesi kwenye harakati za michezo yao .. usipo watolea uvivu utajikuta umenuka ..

Mfano Uchaguzi wa Wenyeviti wa Halmashauri na Mameya unatia sana Dosari Serikali yako ambayo inatokana na Chama kinachofanya sarakasi Yote HII CHAFU. nakushauri kwa mamlaka uliyo nayo Chini ya Waziri wa nchi Amuru Uchaguzi wa Kilombero, Tanga na pengine kwenye migogoro zirudiwe.. na pia elekeza upuuzi unao endelea kumpata Meya wa Jiji la DSM ukomeshwe na wanaoongoza upuuzi huo wachukuliwe hatua kali. ILI Meya wa Jiji apatikane kihalali sio mizengwe inayoendelea.

Pia kwa Mamlaka uliyonayo TAFADHALI Rejesha Heshima na akili ya Jeshi letu la Polisi. Lisimamie sheria na taratibu za kuundwa kwake.Jeshi hili kwa sasa ni mkoba wa siasa za Chama tawala. Wanalitumia watakavyo.. ni Aibu na fedheha kwetu Watanzania tunapoona Jeshi likitumika ndivyosivyo.. TAFADHALI Rejesha akili za Jeshi letu hili..lisichezewe na mtu wala wanasiasa kwa manufaa ya siasa au matumbo ya watu..

SUALA LA ZANZIBAR..

Nashauri tena .. SUALA la Zanzibar najua linakuumiza kichwa sana. Kuna vitisho vingi unapata juu ya serikali ya Zanzibar kubadilika. Wako W anaosema CUF ikichukua Zanzibar watakusumbua hutatawala kwa Raha.. wako W anaosema CCM iking'ang'ania madaraka patachimbika.. mimi kama brain ya nchi nasema , mambo ya Utawala sio kulazimishana au mabavu. Ukiwaongoza watu kimabavu hata yale maendeleo unayotaka kuwapatia hawata yakubali. Na ukiwalazimisha watayafitini.

Kuna sintofahamu kubwa sana ambayo ni zaidi ya Uchaguzi wa Raisi.. sintofahamu ya Muungano wetu..

Mimi nashauri tupitishe karatasi N nyeupe tena.. wananchi tuulizwe kuhusu Muungano.. kama wananchi watasema wanauhitaji Muungano basi tuwe TAIFA moja la Raisi mmoja na serikali moja. Zanzibar iwe mkoa .

Wananchi wakisema hawataki Muungano Zanzibar iachiwe ufanye mambo yake yenyewe kama nchi huru na bara wafanye yao..

Shukria
 
Haka kawazo ni kazuri sana halafu kananukia vizuri kama karafuu, Mimi napiga kabisa na kura yangu kuwa sitaki muungano
Wengi wetu hatujui Muungano ni nini wala Faida zake kwetu ..

Nchi inao wajibu wa kuliondoa Ombwe hili la ielewa kwa Wananchi wake ili tufanye maamuzi tukielewa
 
Back
Top Bottom