RAG atishiwa kuuawa na Simba....!!

RAG atishiwa kuuawa na Simba....!!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741


[TABLE="class: tr-caption-container, width: 541, align: center"]
[TR]
[TD]
RAGE1.JPG
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Ismail Aden Rage.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

MWENYEKITI aliyesimamishwa Simba, Ismail Aden Rage, ameanza kupata wakati mgumu baada ya kutishiwa kuuawa endapo ataendelea kung’ang’ania madarakani.

Rage amethibitisha kuhusiana na hilo jana wakati akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kamati ya utendaji ya klabu hiyo, kutangaza kumsimamisha katika nafasi hiyo, katika kikao chao kilichofanyika mapema wiki iliyopita jijini Dar ambapo tukio la kushangaza ni kitendo cha mwenyekiti huyo kukataa maswali yoyote kutoka kwa waandishi.

Rage amesema kufuatia vuguvugu linaloendelea sasa baina yake na kamati ya utendaji, amepokea simu inayomtaka kuachana na nafasi hiyo, ambapo endapo ataendelea kung’ang’ania atapoteza uhai wake mara moja.

“Nimeshangazwa sana, sasa hivi endapo kama unaweza kufanya vitu vya namna hiyo, ni wazi utashikwa kirahisi, tayari mtu huyo tumeshapata jina lake, nimewasiliana na jeshi la polisi ili kuweza kumsaka na kumtia hatiani,” alisema Rage.

Aidha, katika mkutano wake huo wa jana, Rage ameonyesha kupingana na maamuzi ya Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kufuatia rais Jamal Malinzi kumpa siku 14 za kuitisha mkutano mkuu wa dharura.

“Nimeshangazwa na kusikitishwa sana na ujumbe huu ambao TFF imenitumia, nilitegemea kwanza wangeanza kwa kukemea juu ya hili la kufanyiwa mapinduzi, lakini badala yake wamenitaka kuitisha mkutano mkuu wa dharura, kitendo ambacho ni kuniingilia majukumu yangu.

“Katiba ya Simba inasema wazi katika ibara yake ya 22 kwamba mwenyekiti na kamati ya utendaji wanaweza kuitisha mkutano mkuu wa dharura endapo wataona haja ya kufanya hivyo. Mimi sioni haja ya kufanya hivyo kwa sasa, nasema sitaitisha mkutano na kama watanilazimisha nitajiuzulu

Kuhusiana na hilo, Malinzi alisema watasubiri barua kutoka kwa Rage kuhusiana na kulipinga hilo halafu watalifanyia kazi.

“Suala lile halikuamliwa na Malinzi, ni Kamati ya Utendaji ya TFF. Hivyo tutasubiri barua kutoka kwa Rage halafu tutakaa tena na kulifanyia kazi,” alisema Malinzi.


Wakati Rage akitangaza hayo, amefanya uteuzi mwingine wa viongozi katika uongozi wake, ambapo amemteua Rahma Al Kharusi maarufu kama Malkia wa Nyuki kuwa Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya Simba na Michael Wambura akichukua nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji iliyoachwa na Malkia.

“Nilipokea maombi ya Malkia wa Nyuki, akiniomba nimuondoe katika nafasi ya awali ya kamati ya utendaji, kutokana na kuzidiwa na majukumu yake ya kikazi, lakini bado tunamhitaji,” alisema Rage.

Kuhusiana na Rage kukataa kuitisha mkutano mkuu wa dharura, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Zakharia Hans Pope, alisema watakaa katika kikao na kulijadili hilo, kisha kutoa tamko la pamoja.


Akizungumza kutoka Dubai, Hans Pope, alisema ndani ya kikao hicho, pia ataeleza hatima yake ya kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba.


---GPL
 
Atishiwe Kuuwawa Kwa Lipi? Kwa Umuhimu gani Kwetu Wana Simba? Wote Mnaomshabikia na Kumtetea Rage ni Conservatives!!!!!! Simba Wenzangu Tuache Unafiki na Njaa hizi Zitatuponza na Naomba Mungu hata Tushuke Daraja na Hakika Tutashuka tu Labda Upesi Tukubaliane na Maamuzi na Tumtoe Rage na Kuna Jambo Linakuja Wiki Ijayo ndipo Mtajua Kuwa Mtani Wangu Mhaya TFF hana Masihara na Rage huyu huyu Aliyewadhihaki TFF Atawaomba Mwenyewe Msamaha na Wana Simba Wenzangu Tunaotaka Mabadiliko Msihofu Kuna Habari Njema Wiki Ijayo na Rage Anaondoka Sasa Kama Vile SADDAM HUSSEIN na MUAMAR GHADAFFI Walivyoondolewa na Baba Wa Dunia Marekani na Washirika Wake. CECAFA, CAF na FIFA hawasikilizi Clubs bali Wanasikiliza kile Wanachoambiwa na FA tu za Nchi Husika na Hapa Kwetu TFF ndiyo Mwenye Mpira Wake. Rage Amenyea Kambi!
 
Huyu alshabab mpumbv sana. Ni rafiki mkubwa wa Magulu chemba mpaka akalazimisha timu ikacheze mechi bure singida ili kuvuruga M4c ktk viwanja duni na players wakaumia !
Nina uhakika hii ya kuuawa amesaidiwa na gaidi mwenzake magulu ktk kutafuta sympathy. Nasema aende tuu, akigoma apigwe. Tumechoka na usanii na biashara haramu ulikatiwa ukamuuza twite kwa hao mabulushi, ukamuuza Okwi kisanii sanii na sasa sisi hatuogopi bastola, tuna makombora !!

Hatuwezi kuendelea kwa uongozi wa kisanii sanii nenda kahudumie waliokuchagua na unaowaongopea kwa kofia na kanga.

Utawalipa akina kamna mpaka lini wakushangilie na kukubeba lakini mwisho wako umefika !!
 
Nadhani hili tishio la KIFO litamtoa Rage madarakanai! Akikomaa, let him die nicely just like Sgt. Samwel DOE!
 
huyo Tutu Vengere bana amuwezi kumtoa nyie nyamaume ata kwa vitisho
 
Back
Top Bottom