Rafu za udiwani zaanza Arusha

Rafu za udiwani zaanza Arusha

pefla

Senior Member
Joined
Jan 31, 2012
Posts
105
Reaction score
74
[TABLE="width: 1013"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD] Rafu za udiwani zaanza Arusha


na Ramadhan Siwayombe, Arusha


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF, align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] [TABLE="width: 599"]
[TR="bgcolor: #ffffff"]
[TD="bgcolor: #ffffff"] MIZENGWE ya uchaguzi wa madiwani wa kata nne za Jiji la Arusha imeanza zikiwa zimebaki siku nne kabla ya kufanyika.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Kaloleni wamelalamika kutishiwa kuhamishwa kata na mabalozi wa nyumba kumi wanaopita majumbani kwao usiku kwa madai ya kugoma kutoa shahada za kura.
Malalamiko hayo waliyatoa jana kwa waandishi wa habari mkoani hapa.
Walisema hivi sasa wanaishi kwa mashaka baada ya kutishiwa na mabalozi wao wa Kata ya Kaloleni kuwa endapo wasipotaka kutoa shahada zao na kunukuliwa na mabalozi hao watahamishwa maeneo hayo wanayoishi.
Balozi wa nyumba kumi Kata ya Kaloleni Magharibi, Edington Mshana akizungumzia suala hilo kwa waandishi wa habari, alisema kuwa walipewa maagizo na Katibu wa Tawi la CCM Kaloleni Magharibi, Kata ya Kaloleni aliyemtaja kwa jina Erinesta John.
Alisema waliambiwa wahakikishe kila balozi anakusanya idadi ya wapigakura wake kwenye nyumba kumi wanazoziongoza ili kujua idadi ya wapigakura na kupata tathimini ya ushindi kwenye uchaguzi utakaofanyika Julai 14 jijini Arusha.
Mshana alisema kila balozi katika Kata ya Katoleni alipewa daftari na kalamu ili apite kwenye mtaa wake na kukusanya idadi ya wapigakura wa CCM kupata tathimini ya ushindi, na kwa mtaa wake alipata idadi ya watu 35 ambao aliwaandikisha kwenye daftari hilo na kisha kupeleka kwa katibu wake.
“Mabalozi wamepewa maelekezo na baadhi yetu tumeyatimiza, sasa sijui kama hilo ni kosa na ikibainika kama nimefanya kosa kupitia chama changu (CCM) basi nitaamua kuachia ngazi kama nimeingizwa kwenye mkenge nisioujua, maana sielewi, nimetimiza wajibu wangu na wala sijamtishia kumwamisha mtu kwenye eneo langu bali ni kweli nilipita kwa baadhi ya wakazi wa mtaa huu na kutekeleza yale tuliyoambiwa kama mabalozi,’’ alisema.
Akizungumzia malalamiko hayo msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Sipora Liana, alisema anaandaa mitego ya kuwakamata wanaohusika na kuendesha zoezi hilo na kampeni za usiku za nyumba kwa nyumba.
“Naomba muwasaidie watu hao kwa kuwapa namba yangu ya simu ili hao wanaowafuata usiku wakifika wanipigie nitume askari wakamatwe kwani wanakiuka sheria za uchaguzi kwa kufanya hivyo,” alisema Liana.
Homa ya uchaguzi huo inazidi kupanda kutokana na taarifa za ndani kutoka serikalini kuwa uchaguzi huo unafanyika wakati Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwepo kutokana na kudaiwa siku ya Jumamosi kuwa wilayani Monduli kwa ajili ya kutoa kamisheni kwa maofisa wa jeshi.
Hali hiyo imeongeza ari kwa viongozi wa CCM kuendelea kujipanga kila kona kuhakikisha wanashinda katika uchaguzi huo na kutomtia aibu Rais Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho tawala.
Naye Katibu Mkuu wa CCM Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, alisema waliishajiandaa vyema tangu mwanzo katika uchaguzi huo na wanaamini wananchi wa Arusha wanawaunga mkono na hivyo kuwapa kura za kutosha.
Tanzania Daima Jumatano, iliwashuhudia askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakiwa katika viwanja vyao eneo la Olasiti wakifanya mazoezi jana kuanzia asubuhi hadi majira ya mchana.
Askari hao wakiwa na viongozi wao walikuwa na vifaa vyote ambavyo hubeba nyakati za kutuliza ghasia wakivitumia katika mazoezi hayo kwa lengo la kuhakikisha wanajiandaa vyema kwa ajili ya uchaguzi huo.
Uchaguzi huo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili ni wa kujaza nafasi za waliokuwa madiwani wa kata hizo kwa tiketi ya CHADEMA waliotimuliwa uanachama. Kata hizo ni Themi, Kaloleni, Kimandolu na Elerai.


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Jamani tuwe na subira,wagombea wa CCM wanajiandaa kurudisha kadi kabla ya ijumaa
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetishia kuuanika hadharani ushahidi unaothibitisha polisi kuhusika na mlipuko wa bomu uliotokea katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani mwezi uliopita na kuua watu wanne mkoani Arusha, huku kikiamua kuanzisha kambi za mafunzo kwa vijana nchi nzima kwa ajili ya kuwalinda viongozi wao.
CHADEMA imesema itauanika hadharani ushahidi huo iwapo Rais Jakaya Kikwete atakataa kuunda tume ya kimahakama itakayokuwa na jukumu la kusikiliza shauri hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema kikao cha dharura cha Kamati Kuu, kilichoketi kwa siku mbili jijini humo kimejadili masuala mbalimbali ya kitaifa ikiwemo siasa, rasimu ya katiba mpya na uanzishaji wa kambi za mafunzo ya vijana.
Alisema CHADEMA hawapo tayari kuwasilisha ushahidi wao kwa polisi ambao ndio watuhumiwa wakuu, bali wanataka Rais Kikwete aunde tume huru ya kimahakama.
Alisema isipoundwa tume hiyo ya kimahakama, watauweka wazi ushahidi huo kwa wananchi wakati ukifika.
Mbowe alisema watausambaza ushahidi huo kwa vyama, mashirika ya kiraia ya haki za binadamu ndani na nje ya nchi pamoja na ofisi za kibalozi za mataifa rafiki na Tanzania pamoja na jumuiya ya kimataifa.
Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuwataka waishinikize serikali kuunda tume huru ya kimahakama kuchunguza tukio hilo na mengine yanayofanana na hayo juu ya mauaji ya kisiasa.
Aliongeza kuwa serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Sera (Uratibu na Bunge) William Lukuvi imetoa kauli isiyostahili ndani ya Bunge kuwa CHADEMA wamejilipua kwa ajili ya kutafuta umaarufu.
“Tunalaani kauli ya serikali kupitia kwa Lukuvi, ni ya kitoto, kijinga na ya kiuendawazimu. Sisi hatuwezi kutafuta umaarufu kupitia damu za Watanzania.
“Kama umaarufu unatufikia kwa kazi tuzifanyazo kwa ajili ya wananchi, serikali inatafuta pa kushikia baada ya polisi kuhusishwa,” alisema Mbowe.
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona Lukuvi akiwakilisha serikali na kujinadi kuwa CHADEMA wanahusika na mlipuko pasipo kuuweka hadharani kwa lengo la kukomesha hatua hiyo.
Kuanzisha kambi
Mbowe alisema mlipuko wa bomu uliotokea Arusha katika mkutano wa CHADEMA mwezi uliopita, umetoa somo kwa chama hicho na sasa wameamua kuanzisha kambi za mafunzo kwa vijana.
Alibainisha kambi hizo zitatoa mafunzo kwa vijana ambao watatumika kuwalinda viongozi wa CHADEMA katika shughuli za kichama na kitaifa.
Mbowe alisema Jeshi la Polisi limeshindwa kuchukua hatua stahiki kuwalinda viongozi wa vyama vya siasa, hivyo Kamati Kuu ya CHADEMA imeamua kutoa mafunzo ya kujilinda.
Alibainisha kuwa sababu ya kuanzishwa kwa makambi ya ukakamavu ni kwa ajili ya kuwalinda viongozi wa CHADEMA kwakuwa polisi wameshindwa kufanya kazi hiyo au wanafuata maelekezo ya viongozi wa CCM.
Alisema vikundi vya ulinzi vya CCM kwa kushirikiana na wakuu wa wilaya na polisi wamekuwa wakiendesha zoezi la kuwadhuru wafuasi wa CHADEMA kwa kuwakata mapanga, kuwachoma visu au kuwapiga marungu pasipo kuchukuliwa kwa hatua yoyote.
“Tunaonewa sisi, tunashitaki sisi na tunakamatwa sisi, na sasa kama chama tunasema hii inatosha. Ni lazima tutafute njia mbadala ya kujilinda, tutakuwa ni wajinga kuendelea kupiga magoti na kulia,” alisema Mbowe.
Kiongozi huyo alisema CHADEMA kimewaagiza vijana wa chama hicho waliopo sehemu mbalimbali nchini kujitokeza kwa wingi ili wapatiwe mafunzo maalumu ya ukakamavu kwa ajili ya kuwalinda viongozi wao.
“Mafunzo haya yatatolewa katika kambi maalumu zitakazokuwepo katika mikoa yote nchini…, kitengo cha ulinzi ndicho kitakachoratibu jambo hili,” alisema.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso akizungumzia mikakati hiyo ya Chedema, alisema kuwa jeshi hilo lipo kwa ajili ya watu wote, hivyo mtu akienda kinyume na kuvunja sheria lazima atachukuliwa hatua.
“Nasema sheria itachukua hatua, polisi ipo na kazi zote zinakwenda vizuri hilo ndiyo jukumu la msingi la jeshi, nina hakika jeshi ni imara, Watanzania wote wapo salama,” alisema.
Alisema jeshi lilianzisha ulinzi shirikishi kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anajilinda na kumlinda jirani yake, hivyo sheria za nchi zipo wazi na majeshi yote yanaanzishwa kwa mujibu wa sheria.
Mlipuko wa Arusha
Mbowe alisema baada ya kutokea mlipuko wa bomu katika mkutano wa mwisho wa kampeni ya chama hicho mkoani Arusha na kuua watu wanne na wengine 70 kujeruhiwa, CHADEMA ilitoa tamko kuwa viongozi wake ndio walilengwa katika shambulio hilo.
Alibainisha kuwa viongozi wa CHADEMA akiwamo yeye na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ni miongoni mwa watu waliokuwapo siku ya kufunga kampeni hizo za udiwani.
Alisema katika tamko walilotoa walibainisha ushiriki wa moja kwa moja wa Jeshi la Polisi juu ya mlipuko huo, na kwamba Kamati Kuu imeridhia tamko hilo baada ya kuelezwa ushahidi uliopo.
Kutokana na ushahidi huo, Mbowe alisema chama chao kimefedheheshwa na kauli ya serikali bungeni iliyolenga kulisafisha Jeshi la Polisi kutohusika.
Alibainisha kuwa serikali inafanya jitihada za makusudi kulihusisha tukio hilo na CHADEMA wakati inajua polisi ndio waliotenda uovu huo.
“Tunashangazwa na kitendo cha serikali kupuuza maafa yaliyowafika wananchi wa Arusha. Nyote mnafahamu rais wetu ni mtu makini katika kuhudhuria misiba na majanga mbalimbali, lakini katika hili hata kauli ya kutoa pole haijatoka utadhani waliopata kadhia hiyo si Watanzania,” alisema Mbowe.
Alisema Bunge ambalo ni taasisi ya kuwawakilisha wananchi lilishindwa kuchukua nafasi yake ya kusimamisha kwa muda shughuli zake au kutuma wawakilishi katika tukio hilo na badala yake viongozi wa serikali wamekuwa wakitoa kauli zenye utata.
Alisema Kamati Kuu imelitaka Bunge, kuueleza umma kama tukio la kulipuliwa bomu kwenye mkutano wa CHADEMA, ni tofauti na mengine kama yale ya mlipuko uliotokea kanisani Olasiti, mabomu Gongo la Mboto au kuzama kwa meli ya Mv Skargit.
Aliongeza pia kuwa Kamati Kuu, imelaani vitendo vya fujo, kushambuliwa, kukatwa mapanga kuchomwa visu na kulipuliwa kwa mabomu viongozi wa CHADEMA.
Alibainisha kuwa licha ya matukio hayo, Jeshi la Polisi limeshindwa kuchukua hatua stahiki kwa watu waliohusika.
Rasimu ya katiba
Mbowe alisema Kamati Kuu ya CHADEMA, imetambua kazi kubwa iliyofanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika kukusanya, kuchambua maoni ya wananchi na kuandaa rasimu.
Alibainisha kuwa CHADEMA imetambua na kuainisha mapendekezo mengine ya msingi ambayo yanastahili kuboreshwa zaidi katika rasimu hiyo.
Alisema msimamo na maazimio ya Kamati Kuu, juu ya rasimu ya katiba mpya yameainishwa na kuchapishwa katika kitabu maalumu watakachokizindua katika mkutano wa hadhara watakaoufanya wakati wowote kuanzia sasa.
CC yasikitishwa na Mtwara
Alisema Kamati Kuu imesikitishwa na hali ya sasa kwa wananchi wa Mtwara wanaopata madhila makubwa kutokana na vipigo wanavyopata kutoka kwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi (JWTZ) huku serikali ikikaa kimya juu ya hali hiyo.
Aliongeza kuwa wananchi wa Mtwara kwa sasa wanateswa na kiu yao ya kutaka kujua watanufaika vipi na gesi inayotoka katika mkoa wao, hali iliyowaingiza katika kadhia ya kubakwa, kupigwa na hata kuifanya Mtwara ionekane kama mkoa unaotawaliwa na jeshi.
Alisema hali hiyo ni hatari kwa mustakabali wa taifa, hasa katika kuhifadhi demokrasia kwa kile alichoeleza kuwa nguvu ya jeshi inaweza kusambaa katika mikoa yote na kulifanya Jeshi la Polisi lisiwe na kazi ya kufanya au nchi kutokuwa na utawala wa kidemokrasia.
 
MOJAWAPO ya mada kali kabisa ambazo nimewahi kuanzisha kwenye mitandao ni ile ya wiki iliyopita ambayo nilisema wazi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aombe radhi kwa kukubali mwaliko wa kwenda kwenye dhifa ya Obama iliyofanyika Ikulu ambako Rais Jakaya Kikwete – Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano alikuwa mwenyeji.
Wapo ambao walikerwa na wengine kuchukizwa vikali kabisa kwanini nimesema hivyo huku wengine katika hasira zao wameniona kama naleta ugomvi fulani.
Niliainisha sababu za maoni yangu katika makala yangu ndefu. Kwa kifupi nilisema kuwa katika mazingira ambayo upinzani Tanzania unakandamizwa, sheria ya uchaguzi bado ni mbaya na watu kadha wa kadha wamekufa katika mikutano ya CHADEMA tena kwa mikono ya vyombo vya dola, itakuwa ni dhambi na kukatisha tamaa kwenda kukaa na kula chakula cha furaha mbele ya Rais Obama badala ya kutumia nafasi hiyo kupinga mambo yanayofanywa, hasa uvunjaji wa haki za binadamu na ukandamizaji wa uhuru wa habari.
Kundi moja kubwa ambalo halikupenda kabisa wazo langu, lilinijia juu kwa sababu kubwa mbili; kwamba kwani “Obama alikuja kwa ajili ya CCM? Si alikuja kwa ajili ya Watanzania?” na pili; “Siyo kila mambo ni ya siasa mengine ni ya kitaifa na Mbowe amefanya jambo la kuonyesha utaifa.”
Sasa hilo la kwanza sitalijibu kwani nina uhakika wa asilimia 100 siku si nyingi zijazo viongozi wa juu wa CCM watajitangazia sifa na kujipongeza kwa ujio wa Obama na kwa haki wanastahili kufanya hivyo.
Ni hili la pili la “utaifa” ndilo ambalo binafsi limenikoroga kiasi cha kuona nililete mbele ya watu wengine waamue huu ‘utaifa’ ambao CHADEMA wanatakiwa kuwa nao lakini siyo CCM, ni utaifa gani huu?
Hivi huu unaoitwa "utaifa" kwanini hatusemi na CCM wauoneshe? CHADEMA imekuwa ikipiga bungeni na nje ya Bunge kwa Rais Kikwete kuunda Tume ya Kimahakama (Judicial Inquiry Commission) ili kuchunguza mauaji yanayotokea mikononi mwa vyombo vya dola au yenye utata; lakini hadi leo Kikwete hajafanya hivyo? Je, siyo maslahi ya taifa kwa yeye kufanya hivyo? Kwanini hatujasikia mwanaCCM hata mmoja akiunga mkono hili au hili ni la " CHADEMA" lakini ujio wa Obama ni la "Kitaifa"? Huu "utaifa" ni nini hasa?
CHADEMA wamekuwa wakilalamika kuwa polisi wananyanyasa sana, Jeshi la Polisi linatumia nguvu mno kwenye mikusanyiko ya amani na limesababisha mauaji; wakataka IGP Mwema, Chagonja na Kamuhanda wawajibishwe; Kikwete akaamua kuwatunukia nishani za "utumishi uliotukuka"? Halafu watu wanasema CHADEMA ionyeshe utaifa! Hivi kwanini Kikwete yeye haonyeshi huo "utaifa"? Kwanini huu "utaifa" uwe wa CHADEMA kushabikia mambo ya serikali na CCM, lakini wao CCM hawatakiwi kushabikia mambo ya upinzani na ukisikia mwanaCCM anafanya hivyo anakuwa ‘labeled’ kuwa ni "mpinzani" kwa nini hao CCM hawaonyeshi huo "utaifa"?
Huu "utaifa" unaosifiwa kwa CHADEMA kwanini hatuudai kwa CCM ili na wao wauonyeshe au haya mambo yote ambayo CHADEMA inapigania na kusimamia ni ya CHADEMA tu na siyo ya kitaifa? Ila yale yanayofanywa na Ikulu ndiyo ya kitaifa? Au wao CCM na serikali yake wanakubaliwa tu kuwa wanayosema wao na kufanya ni ya "kitaifa" na ya wengine ni ya "kikabila, kidini na kikanda"?
Maswali mbalimbali yamejengeka kichwani mwangu kuhusu huu “utaifa”.
Baada ya wabunge wa CHADEMA kumsusia Kikwete wakati anatoa hotuba yake kuonyesha kupinga kwao namna uchaguzi ulivyofanyika na jinsi ambavyo tume ya uchaguzi na vyombo vya dola vilimbeba wapo waliounga mkono kitendo kile na waliopinga. Waliounga mkono walisema wanafanya hivyo ili kumtumia ujumbe wa wazi kuwa hawakupendezwa na jinsi alivyochaguliwa na hawakuwa tayari kumtambua. Wengine waliopinga waliona kitendo kile ni kuvunja heshima na kukosa uzalendo; hawa waliamini kuwa kwa vile rais kishaapishwa na hakuna namna ya kupinga matokeo basi CHADEMA wakubali tu yaishe. CHADEMA walidaiwa waonyeshe utaifa wao.
Miezi michache baadaye uongozi wa CHADEMA ukaamua kumtambua Kikwete kama rais halali. Yeye mwenyewe alisema kuwa “waacheni watoke watarudi” na kweli walirudi. Wakaonyesha “utaifa”.
Mchakato wa katiba mpya ulipoanza ilikuwa wazi kabisa kuwa umetekwa na Rais Kikwete na CCM na vyovyote itakavyokuwa nchi itapelekwa kwenye Katiba Mpya kwa masharti ya CCM na Kikwete. CHADEMA kwa muda walionyesha kusita kuunga mkono na hata sheria ya mapitio ya katiba ilipokuwa inaelekea kupitishwa walikuwa wamegangamala kupinga baadhi ya vipengele vyake.
Mwisho wa siku Rais Kikwete akatoa mwaliko wa kukutana na vyama mbalimbali na CHADEMA ikafika zamu yao. Picha zinazowaonyesha wapinzani hawa wakikoroga chai Ikulu zilibakia kuwa gumzo kuwa “walikwenda kunywa juisi”. Kikwete akapata anachotaka - uhalali – lakini vile vile akawaweka wapinzani sehemu yao – upinzani. CHADEMA wakaonesha “utaifa”.
Wakati wa kuundwa kwa Tume ya Katiba CHADEMA nao wakajikuta wameingizwa ndani na wakakubali – wakaonyesha utaifa.
Mara kadhaa viongozi wa CHADEMA wamejikuta wakilazimishwa kumwaga sifa kwa rais anapokuwa katika eneo lao na hata kuisifia serikali kwa mambo inayofanya. Hakuna hata mmoja aliyesimama na kuwaambia watawala ukweli mbele ya macho yao – kwani wanaamini si mahali pake na kuna hofu ya kuonekana si ‘wataifa’. Hivyo, wameendelea kuonyesha utaifa katika ufunguzi wa miradi mbalimbali kwenye majimbo yao.
Sasa CHADEMA wana haki ya kusifiwa kwa kuonyesha “utaifa” na kuweka mbele “utaifa” hata mahali ambako pachungu. Swali bado linabakia ni lini Kikwete naye ataonyesha utaifa Kwa kuwatimua maofisa wa polisi wanaohusishwa na uvunjaji wa haki za binadamu badala ya kuwavisha nishani na kuwapandisha vyeo? Ni lini ataonyesha utaifa wa kuhakikisha tume ya kimahakama inaanzisha uchunguzi wa mauaji yenye utata yanayofanywa na vyombo vya dola? Ni lini ataonyesha utaifa na kuruhusu uchunguzi huru wa Meremeta ufanyike?
Ni lini serikali yake itaonyesha utaifa wa kutupatia majibu inawezekana vipi ndege ya kijeshi kutoka Qatar kutua nchini, kuchukua wanyama na kutoweka nao huku wakuu wote wa vyombo vya usalama wakiendelea kula na kunywa na kupigiana saluti? Ni lini Watanzania wataanza kudai CCM na serikali nao waanze kuonyesha utaifa kufuatilia na kukubali yanayoletwa na CHADEMA?
Au utaifa ni ukifanywa na serikali na CCM lakini ukitoka kwa upinzani si utaifa tena? Na hadi lini wapinzani wataendelea kucheza ngoma ya CCM na serikali tena kwa mbwembe, lakini wao wakipiga ngoma yao wanaambiwa haisikiki au ndani yake ina mlio wa udini na ukabila? Kuna mistari mingine haipaswi kuvukwa na ikishavukwa ni vigumu sana kurudi nyuma. Hivi CHADEMA wakipigwa tena na kuuawa na serikali ikiendelea kupuuzia hayo bado wataendelea kukubali mialiko ya kukaa na serikali kwa jina la “utaifa”.
Ningekuwa CCM ningesifia sana utaifa wa CDM. Why not?
 
Mtaacha lini uongo arusha mbona kila mtu muongo kuanzia mbunge wao mpaka watoto.
 
[TABLE="width: 1013"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD] Rafu za udiwani zaanza Arusha


na Ramadhan Siwayombe, Arusha


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF, align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] [TABLE="width: 599"]
[TR="bgcolor: #ffffff"]
[TD="bgcolor: #ffffff"] MIZENGWE ya uchaguzi wa madiwani wa kata nne za Jiji la Arusha imeanza zikiwa zimebaki siku nne kabla ya kufanyika.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Kaloleni wamelalamika kutishiwa kuhamishwa kata na mabalozi wa nyumba kumi wanaopita majumbani kwao usiku kwa madai ya kugoma kutoa shahada za kura.
Malalamiko hayo waliyatoa jana kwa waandishi wa habari mkoani hapa.
Walisema hivi sasa wanaishi kwa mashaka baada ya kutishiwa na mabalozi wao wa Kata ya Kaloleni kuwa endapo wasipotaka kutoa shahada zao na kunukuliwa na mabalozi hao watahamishwa maeneo hayo wanayoishi.
Balozi wa nyumba kumi Kata ya Kaloleni Magharibi, Edington Mshana akizungumzia suala hilo kwa waandishi wa habari, alisema kuwa walipewa maagizo na Katibu wa Tawi la CCM Kaloleni Magharibi, Kata ya Kaloleni aliyemtaja kwa jina Erinesta John.
Alisema waliambiwa wahakikishe kila balozi anakusanya idadi ya wapigakura wake kwenye nyumba kumi wanazoziongoza ili kujua idadi ya wapigakura na kupata tathimini ya ushindi kwenye uchaguzi utakaofanyika Julai 14 jijini Arusha.
Mshana alisema kila balozi katika Kata ya Katoleni alipewa daftari na kalamu ili apite kwenye mtaa wake na kukusanya idadi ya wapigakura wa CCM kupata tathimini ya ushindi, na kwa mtaa wake alipata idadi ya watu 35 ambao aliwaandikisha kwenye daftari hilo na kisha kupeleka kwa katibu wake.
"Mabalozi wamepewa maelekezo na baadhi yetu tumeyatimiza, sasa sijui kama hilo ni kosa na ikibainika kama nimefanya kosa kupitia chama changu (CCM) basi nitaamua kuachia ngazi kama nimeingizwa kwenye mkenge nisioujua, maana sielewi, nimetimiza wajibu wangu na wala sijamtishia kumwamisha mtu kwenye eneo langu bali ni kweli nilipita kwa baadhi ya wakazi wa mtaa huu na kutekeleza yale tuliyoambiwa kama mabalozi,'' alisema.
Akizungumzia malalamiko hayo msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Sipora Liana, alisema anaandaa mitego ya kuwakamata wanaohusika na kuendesha zoezi hilo na kampeni za usiku za nyumba kwa nyumba.
"Naomba muwasaidie watu hao kwa kuwapa namba yangu ya simu ili hao wanaowafuata usiku wakifika wanipigie nitume askari wakamatwe kwani wanakiuka sheria za uchaguzi kwa kufanya hivyo," alisema Liana.
Homa ya uchaguzi huo inazidi kupanda kutokana na taarifa za ndani kutoka serikalini kuwa uchaguzi huo unafanyika wakati Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwepo kutokana na kudaiwa siku ya Jumamosi kuwa wilayani Monduli kwa ajili ya kutoa kamisheni kwa maofisa wa jeshi.
Hali hiyo imeongeza ari kwa viongozi wa CCM kuendelea kujipanga kila kona kuhakikisha wanashinda katika uchaguzi huo na kutomtia aibu Rais Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho tawala.
Naye Katibu Mkuu wa CCM Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, alisema waliishajiandaa vyema tangu mwanzo katika uchaguzi huo na wanaamini wananchi wa Arusha wanawaunga mkono na hivyo kuwapa kura za kutosha.
Tanzania Daima Jumatano, iliwashuhudia askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakiwa katika viwanja vyao eneo la Olasiti wakifanya mazoezi jana kuanzia asubuhi hadi majira ya mchana.
Askari hao wakiwa na viongozi wao walikuwa na vifaa vyote ambavyo hubeba nyakati za kutuliza ghasia wakivitumia katika mazoezi hayo kwa lengo la kuhakikisha wanajiandaa vyema kwa ajili ya uchaguzi huo.
Uchaguzi huo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili ni wa kujaza nafasi za waliokuwa madiwani wa kata hizo kwa tiketi ya CHADEMA waliotimuliwa uanachama. Kata hizo ni Themi, Kaloleni, Kimandolu na Elerai.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Mkuu endeleeni kuwadanganya watu mwisho wa siku majibu yatatoka tu.
 
CCM maji ya shingo lazima watumie nguvu za giza ili washinde lakini wajanja tumeshawashitukia. Jumapili watachezea kichapo tu
 
Back
Top Bottom