Rafiki yangu , mbaya wangu , hewala

Mlupembe

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2014
Posts
446
Reaction score
217
Dah , rafiki yangu m baya wangu ! Tuliishi pamoja kama marafiki , siri yangu ni yake , hakuna tulilofichana hata mtaji wa biashara ya mtumba tumechanga ! Jana nikaenda kumuaga swahiba kuwa leo j mosi naenda dom kufuata kuku nilete magomeni kuuza , swahiba kaniaga safiiii ! Lakuvunda halina ubani , leo skuamka fresh nikaona niondoke kesho , mapemaa sa nne nkaona nkamfahamishe swahiba magomeni ddc , nafika naona majirani wanashtuka afu wananon'gonezana , me si nkajua kama kawa ni utani nlozoea kuwatania ndo wananzingua tu ! Nkawapita hayooo chumba cha swahiba , me pale ka kwangu 24hrs , chubwi ndani dah , lahaula walahkuwata , swahiba yuko juu ya mtu kakurupuka kunigeukia , kumcheki aliyekuwa kitandani duh ! Mpenzi wangu wa moyo , wangu tuliyepeana mapenzi ya thati tangu miaka 2 ilopita kwao wananijua kwetu wanamjua mahari nshatoa december ! nilishindwa kuongea nilinywea , Mpenzi wangu akaniita kwa mshtuko jina langu, skuwa na ham nikatoka kimyaaa nje nkakuta majirani wamejaa mlangoni ! Nikajifanya najichekesha kuwazuga kiaina mtoto wa kiume ! Mungu akanipa ujasiri nikatoka kuelekia home , kutokana na kupagawa bahati mbaya nikagongwa na bodaboda pale mwembechai nashkuru sijaumia sana nipo home ila moyo naona kama kuna mtu anauchoma sindano ! Naumia sina pa kupeleka maumivu yangu , ila sababu najua mpenzi wangu na swahiba wangu wote hupendelea jf.. Napenda kuwaambia mungu atanilipia hewala.
 
Mkuu kwel au hadithi??
 
Kma ni kwel pole sana ila wew ni mwanaume wa kweli
 
Mademu sio watu ni viumbe cc . [MENTION=188383]okw[/MENT







MADEMU NI VIUMBE
 
Si mtaalam wa hadithi ila leo yamenikuta..... Tangu saa nne nimejiinamia home siwazi maumivu ya ajali ila moyo unachoma kila nkikumbua lulu alivoshtuka na kuvuta shuka kuuficha mwili wake !
 
Ningekuwa wewe ningerudisha shukrani ya sadaka kwa Mungu maana amekuonyesha haya kabla hujaingia kwenye hiyo ndoa.
 
Hata siku moja simuamini rafiki hata niwe nnamfahamu tokea kitambo. Marafiki hugeuka maadui ndani ya usiku mmoja,
 
Mkuu pole sana. Mungu ndio hakimu wa kweli. We mshukuru kwa yote
 
Nashangaa mtu akiweka moyo wake rehani, kisa binadam mwenzake! Watu hawatabiriki, pole!!
 
Si mtaalam wa hadithi ila leo yamenikuta..... Tangu saa nne nimejiinamia home siwazi maumivu ya ajali ila moyo unachoma kila nkikumbua lulu alivoshtuka na kuvuta shuka kuuficha mwili wake !

Kwanza natoa pole na pongezi pia kwa uamuzi uliochukua.Ngumu kumeza wala kutafuna, na huwezi kutema maumivu yake. Ila fimbo uliyowachapia kuwaacha ukachukua hamsini zako baada ya kuwafuma hiyo ni adhabu kwao kuliko ungepigana au kumpiga demu wako.Mkuu Mlupembe, wahenga wana msemo wao "muda huponya",maumivu uliyoyapata siku ya tukio sidhani kama yatabakia hivyo hivyo kwa wiki 2 zijazo, kadiri muda utavyokuwa unasonga na maumivu yatakuwa yanabakia kumbu kumbu tu.Songa mbele mkuu. Ila,nenda hospital (Kama baada ya ajali ulikuwa hukuenda) ukapime kuangalia kama umepata athari yoyote mwilini, usijione mzima kwa vile tu baada ya ajali umenyanyuka na kuanza kutembea ukajiona mzima. Nina mifano kama 3 ya matukio kama yako ya ajali, 1 ktk mifano hii ilimkuta mshikaji wangu, alipuuzia kwenda hospital baada ya tukio kwa vile tu hakusikia maumivu yoyote mwilini. Keshatangulia mbele ya haki, ajali ilimpa athari, mpk alipokuja kushtuka alikuwa keshachelewa.Pole sana kwa matukio yote hayo.
 
Ndo maana unapigiwa, unajiita 'mtoto wa kiume'??? Na mwandiko wako umelegeza sauti huku imeabana pua.
 
Hapa nafikiria ndoa ya mkataba

Uknizingua kesho unapaki unasepa

Walahi vile
 
kweli binadam wa Leo niwagum washukrani kwa muumba aisee.

MKUU hembu Fanya hizo pesa nusu yake uliokuwa unaenda kununua kuku toa sadaka kwa mola wako aisee.

mungu kakufanyia kitu kikubwa sana aisee baada ya kumshukuru na kufurahia ww unalialia hapa..

mm ndio maana nakataaga kabisa kuwekeza kwa hawa watu aisee sito kuja jaribu hata siku 1 wengi huishia kusema sieleweki coz ukieleweka tuu mbele yao wanakufanyia ushenzi huoo.
tatizo lenu watoto wakiume mnanyoosha sana Maelezo kwa wapenZi wenu ndio maana akikutana na ngum kumeza kama sie mbona ananyoka.
wanawake WA sasa hivi na dunia ilivyo kusaliti imekuwa kama fashion aisee.hata umjengee ATM mashine home akitaka any time anabonyeza na kutoa mkwanja lakini lazima akagongwe tuu njee.

inafika kipindi huwa mpaka namlaum mungu sijui nikwanini binadam alitupendelea hivi kwenye suala la mapenzi asingelifanya kama wanyama wengine au mimea?? iwe nikwaajili ya kuzaa tuu??

asante kwa hadithi yako yenye mafundisho.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…