Amani (jina sio halisi) ambaye ni rafiki yangu wa karibu, ndoa yake sasa ina muda wa miaka minne na amejaliwa kupata watoto wawili, wakati mke wake anakwenda kujifungua kijijini, Amani alibaki peke yake nyumbani ambapo kwenye hiyo nyumba aliyokuwa amepanga kunawapangaji wengine wakiwemo wanachuo wa Chuo fulani maarufu jijini. Fursa hii ya kuwa peke yake ilimfanya ajiingize kwenye mahusiano na mmoja wa mpangaji ambaye ni mwanachuo, kilichoendelea hapo ni kuwa mwanachuo kapata ujauzito na alipowaeleza ndugu zake ilibidi Amani aitwe na wazazi wa binti ambapo alikiri kuwa anahusika na huo ujauzito. baada ya hapo ndoa ya mkeka kufungwa huko nyumbani kwa binti bila majirani na watu wengine kujua (majirani wa Amani)
Uhusiano umeendelea na Amani amekuwa akihudumiwa na binti kwa kificho bila majirani wengine kujua. Sasa mke mkubwa kesharudi na Amani hajaeleza yaliyomkuta wakati mkewe hayupo,usiri umetawala na binti ambaye naye ni mjamzito anaishi kwenye hiyo nyumba mimba inaendelea kukua, Amani amekuwa akijiiba usiku wa manane au asubuhi sana akimtembelea bi mdogo, Amani anachofikiri ni kumfahamisha mke mkubwa UKWELI. Mimi binafsi sikufurahishwa na tukio hili na hii nikitokana na ukweli kuwa mke wa Amani ni dada mtulivu mwenye bidii na moyo wa huruma hivyo nimekuwa mzito hata kushauri ila kwa kuwa dini ya Amani haimzuii kuwa na zaidi ya mke mmoja nafikiri anaweza kupata ushauri kwa wabobezi wa dini pamoja na wanajamvi.