Rafael Benitez amefukuzwa kazi kama meneja wa Real Madrid

prezdesho

Senior Member
Dec 30, 2015
150
78
Rafael Benitez amefukuzwa kazi kama meneja wa Real Madrid, miezi saba tu baada ya kupewa kazi hiyo Bernabeu. Benitez, 55, aliondolewa kufuatia mkutano wa bodi ya klabu hiyo siku ya Jumatatu. Kocha wa timu B ya Real Madrid, Zinedine Zidane, 43, ameteuliwa kuwa meneja wa kikosi cha kwanza cha Real Madrid
 
kazi wanayo mwaka huu na huyo nae hata hiyo miezi saba hafiki watamtimua
 
Nilijua japo sukuwahi kulisema Rafael hakuwa na ubavu wa kupambana na Barcelona...hiyo ilikuwa nu ticket yake ya kuondoka
 
Nilijua japo sukuwahi kulisema Rafael hakuwa na ubavu wa kupambana na Barcelona...hiyo ilikuwa nu ticket yake ya kuondoka
na huyu zizou akija pale camp nou lazima akaribishwe kwa 5 kama mourihno na rafa
 
Itafika kipindi makocha wenye heshima zao wataikacha hii timu, toka Del Bosque atimuliwe hakuna stability kabisa
 
Itafika kipindi makocha wenye heshima zao wataikacha hii timu, toka Del Bosque atimuliwe hakuna stability kabisa

Ondoa mawazo hayo, nani umesikia anakataa pesa ya bure, Benitez hapa ndio winner, amefanyakazi miezi sita anakula mshahara wa miaka miwili na nusu. What a dream job, ndio maana alivyopewa mkataba alikuwa analia kwa furaha watu hawakumwelewa walifikiri anaililia Real Madrid. Pesa ya bure tamu.
 
Hahaha...
Lakini mkuu timu zenye pesa zipo nyingi siku hizi, hawa jamaa wanawadhalilisha watu na fani zao
 
Zidane hongera zake jamaa kafight sana mpaka kufikia hapo alipo;ilibidi arudi darasani kabisa ili kusomea ukocha leo matunda ndo hayo.
 
Back
Top Bottom