Hapa ndipo tunarudi kwenye kujiuliza, hivi ni kweli Gardner na Kibonde wote wafanye mistake hii pamoja?
Kibonde na Gardner wote ni watu wa mizaha, na inawezekana huo ulikuwa ni mzaha, the pun being ile office ina nguvu sana, hence "overhaul" office.Kwa hiyo kama wewe si mtu wa kuelewa sanaa unaweza usijue kwamba wanafanya mzaha, ni sawa sawa na Michuzi anavyosema "my wife wangu" halafu umkomalie wakati unajua Michuzi ni bonge la clown.
Ingekuwa Radio inayojulikana kwa u serious wake labda ningekuelewa, Clouds chata lao ni mizaha na kuwa informal, kwa hiyo inawezekana kabisa asiyeelewa hapa ni wewe msikilizaji, umeenda kusikiliza redio ya mizaha wakati wewe si mtu wa mzaha.
Siamini kwamba mtu kama Ephrahim Kibonde hajui tofauti ya "Oval Office" na "Overhaul Office" especially kama wameisema mara mbili mbili kuweka msisitizo unajua kabisa wana jive tu.