Qnet naomba pesa yangu milioni 5, nimenunua saa mpaka sasa najuta kuwafahamu..

wanaojulikana

JF-Expert Member
Sep 14, 2017
577
1,000
Nimepigwa na hawa wezi wa Qnet wamenishawishi nikaingia nikanunua SAA mil 5 nitapata Mara mbili zaidi ya hapo.

Naomba mnipe pesa zangu tutauwana Mwaka huu mil 5 hivi hivi, then mpaka sasa bila bila nitakuja ofisini kwenu na polisi mambo ya utapeli iwe mwisho kabisa.

Qnet naomba muwe waungwana mlimshawishi mke wangu na shemeji watoe milioni 8 ambayo walinunua saa mkasema baada ya miezi 13 watapata bilioni 3.3, mbaya zaidi mkamwambia don't share the information. Yaani mnafanya siri mazungumzo, hela mke katoa lakini mnamzungusha sijui mnasema apeleke mtu mwingine tena ndo alipwe, nyie ni matapeli wakubwa na kesi iko police.

Nawapa onyo mkinishinda mahakamani naenda Gamboshi kuwaroga, nyie watu wa ajabu mlianza kwangu baada ya kunipiga porojo zenu nikawashitukia mkamdanganya mke na shemeji na hii njia yenu kutusalimia good morning hata jioni nahisi ndo njia ya kuwapumbaza watu, nawaambia io hela mtaitoa, mama yangu msukuma.
 

ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
9,110
2,000
D9, Amazon, forever living, Bitblub.nk


hiii michezo ni Upatu Wizi haina faida hamjifunzi to hakuna pesa rahisi

Ngoja tutawaletea mlejesho wa forex hadi mwezi wa kwanza tutawapa majibu naona nnchi za wenzetu wanapiga pesa sana
Hayo yote ni matapeli FX haina connection na utapeli
matapeli labda baadhi ya brokers
 

ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
9,110
2,000
Jamaa wapo mikocheni B na maeneo mengine ya dar . Ukifika unakaribishwa kwa salam kedekede za "goodmorning partner" wana wanawake wazur kweli. Wanakuingiza kwenye chumba unasomeshwa weeee .kisha unaambiwa uje kesho tena. Juzi kuna mpuuzi alinipeleka pale na hakuniambia tunaenda kwenye ule ujinga nilivyotoka sijarudi tena. Pole mkuu wanasema mjini shule
Mkuu vp hujaambulia hata mtoto mmoja mkali
 

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
12,816
2,000
Nashauri tufanye utafiti kwanza wa namna ambayo network marketing inafanya kazi! Network marketing believe it or not is an industry kama ilivyo industry ya mziki, kilimo, uzishaji nakadhalika. It is a legitimate business sema haifanani na biashara tulizozoea na utashi wa biashara tulizozoea hautumiki huku! Me nashauri kila mtu afanye utafiti yakinifu na jaribu kidoogo kuwa open minded msiache hizi negative comments ziwaaminishe kwamba biashara ama kampuni ya Qnet ni magumashi. Kuna wasomi kibao wamemaliza chuo wamo humu, Auditors wa the Big 4, bankers, accountants vijana wadogo tu! Kwani unadhani wao wameona nini?? Hata Kampuni kama Apple, samsung, Tesla, inapata alot of negativity but they still make huge profits so dont let these few negative comments zikuzuie fursa nzuri ya kutengeneza passive income waache wanaobisha wapambane na ajira na small businesses(Mngesoma basi ata Rich Dad Poor Dad na 21st Century Business cha Robert Kiyosaki before spewing all this rubbish)! Nimepata presentations na nafanya mchakato wa kupata iyo hela nijiunge na hii fursa japo mchakato ni mgumu sio siri ila itafahamika tu!
Yaani elimu yoote iliyomwagwa hapa still unataka kuwekeza pesa zako huko?
Wonders will never cease!
 

mgosani

JF-Expert Member
Dec 25, 2014
729
500
Yaani elimu yoote iliyomwagwa hapa still unataka kuwekeza pesa zako huko?
Wonders will never cease!
Mimi kuna jamaa yangu alitaka nijiunge akanipa darasa nianze kununua Bio-disc nikamwambia sina pesa nikopeshe nikianza kupata nitakulipa basi ikawa ndiyo goodbye
 

Linko

JF-Expert Member
Aug 20, 2016
2,162
2,000
Nimepigwa na hawa wezi wa Qnet wamenishawishi nikaingia nikanunua SAA mil 5 nitapata Mara mbili zaidi ya hapo.

Naomba mnipe pesa zangu tutauwana Mwaka huu mil 5 hivi hivi, then mpaka sasa bila bila nitakuja ofisini kwenu na polisi mambo ya utapeli iwe mwisho kabisa.
usilalamike kijana qnet iko poa sema ina hitaji mda sana na wateja wa mara kwa mara kama umetoa pesa halafu unakaa nyumbani usitegeme kuwa utapata cha msingi tafuta mwenzako na yeye atoe milioni tano ili upate commision
 

SPSS

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
715
500
usilalamike kijana qnet iko poa sema ina hitaji mda sana na wateja wa mara kwa mara kama umetoa pesa halafu unakaa nyumbani usitegeme kuwa utapata cha msingi tafuta mwenzako na yeye atoe milioni tano ili upate commision
Duuuh 5m???....ndi upate kamishen???....u guys are not serius
 

Mello

Senior Member
May 7, 2017
110
250
Tufanye Kazi tupate hela halali, Acheni kutafuta Shortcuts. Idiots. Kwanza mm nikishaona tu mshikaji wangu wa zamani akinipigia simu, " bwana nataka tuonane nina jambo nataka tuongee" hua nina block namba kabisa.
 

cdc

JF-Expert Member
Nov 29, 2015
432
500
Hahahaha. Nimejikuta nacheka peke yangu. Kwaiyo wakakuambia ununue saa kwa million 5 afu watakupa million 10?so you mean Qnet ni charity organisation? Au hujatupa maelezo ya kutosha?
 

edwayne

JF-Expert Member
Apr 5, 2013
4,759
2,000
Good morning partner.....
Kwa kiswahili rahisi...QNET ni kikundi cha Matapeli......Yaani unatapeliwa kwanza...kisha unapewa mafunzo ya utapeli ili umtapeli MTU wako wa karibu ndiyo ulipwe kamisheni...
Fact
 
  • Thanks
Reactions: cdc

Rohombaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
11,954
2,000
Hahahaha. Nimejikuta nacheka peke yangu. Kwaiyo wakakuambia ununue saa kwa million 5 afu watakupa million 10?so you mean Qnet ni charity organisation? Au hujatupa maelezo ya kutosha?
Dah..... Dah yaani unafanya unafanya manunuzi ya bidhaa kwa Bei Mara 10 zaidi ya thamani Yake Sokoni ambayo haipungui 5m ndiyo unaingia....kisha utafute watu wengine 2 wafanye manunuzi ya 10m ndiyo upewe laki 4.... Yaani Chini ya 3% ya biashara uliyofanikisha
 
  • Thanks
Reactions: cdc

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom