Watu wa pwani hii kitu tunapendaga sana mapishi pia hutofautiana leo nenda fresh food nunua pweza alafu pika kama hivi hutojutia..
MAHITAJI
Pweza - 1 Kilo
Mafuta - ½ kikombe
Chumvi - 1 kijiko cha chai
Tangawizi mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Kitunguu saumu (thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Masala ukipenda - 1 kijiko cha supu
Namna ya kutayarisha na kupika
Osha pweza kisha mkatekate
Mtie viungo vyote ulotayarisha na chumvi
Muache nusu saaa akolee viungo
Mtie ndani ya sufuria bila maji mfunike kisha weka jikoni, atatumbuka maji mwenyewe kwa moto wa kiasi paka awe rangi ya damu yam zee (maroon)
Akishawiva kwa rangi hiyo basi sasa mwaga maji yote,chukua pweza pekee weka kwenye bakuli au sahani
Weka karai au kikaango (frying pan) motoni tia mafuta acha kwa muda wa dakika tano hivi mafuta yapate moto.
Mimina pweza kwenye karai aacha wakaangike paka wabadilike ukiwageuza geuza kila baada ya muda wa dakika kumi hivi. Pweza tayari kwa kuliwa kwa ugali au muhogo
Kidokezo: Unaweza kumwagia masala kiasi baada ya kukaanga kama picha inavyo onyesha.
Kuna jamaa pale kituo cha machinga complex alikula hadi nauli kisa vipweza vya mezani.Alikuwa anaenda Chanika aisee nilimuonea huruma nikampa buku nikamwambia siku nyingine chukua tahadhari.