Leo wakati naangalia BBC nilicheka Sana!!!
Kwamba Rais Putin wa urusi kampigia simu Kiranja wa dunia mkuu wa taifa kubwa lenye nguvu,kivita,kiuchumi na fitina Marekani, wengine hupenda kuliita USA,US au America!!
Bwana Putin kamuomba kiranja wa dunia wakae kitako,watete kuhusu mgogoro wa Yukireini, au Ukraine!!!
Warusi wanalitaka jimbo la cremia ambalo ni mali ya Ukraine,marekani na umoja wa ulaya hawataki jimbo hili liende kwa Putin!! Sababu mimi sijui!!
Sasa hv kiranja wa dunia yuko Saudi Arabia, anaomba wauze mafuta kwa marekani na marekani atawalinda kijeshi saudi Arabia!! Nani asiyekubali ulinzi?? Kama unataka kujua utamu wa ulinzi muulize baba rizi!!
Na wataalam wa masuala ya mafuta wanasema baada ya miaka miwili,kiranja wa dunia ndo ataongoza kwa wingi wa mafuta!! Kayatoa wapi mimi sijui, Si Putin au Saudi Arabia tena!!
Sasa wewe Putin kaa na mibomu yako,wenzako wanatumia akili kukutawala,kama wewe ni kidume kweli,tena mbishi kama Saddam Hussein au Gadaff mbona umenyanyua waya kumcall mkulu wa marekani??
Acha ubabe wa kijinga!! Wenye nguvu Waite power!!!
Putin ondoa wanajeshi wako Ukraine!!!