Putin alikuwa namuunga mkono au alikuwa anamuogopa George W. Bush?

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
5,784
2,000
Wakuu, katika marais wa hivi karibuni wa US hakuna rais alikuwa Nyamera na mtata Kama Bush mtoto. Huyu rais alikuwa asikilizi la mtu iwe UN, mabunge yake, nk alikuwa akiamua kukugonga unagongeshwa tu na hakuna mtu wa kukusaidia bila shaka wasaidizi walikuwa wanaogopa.
Kuna huyu Putin wakati watu wanatandikwa hovyo hovyo yeye anakaa meza moja na kubwa la maadui wanakunywa wine na kugonga cheers na inaonekana Putin alikuwa anamkubali Sana bush kuliko hawa waliomfuatia wakati bush ndo alikuwa mbabe na mkorofi kuliko hawa waliofuatia, je Putin alikuwa anamuogopa jamaa au alikuwa anaunga mkono harakati zake?

mohamedidrisa789

JF-Expert Member
Jun 20, 2015
1,402
2,000
katika dictionary ya Putin uwa hamna neno kumuogopa mtu, yeye akiamua la kwake basi kikubwa tu usimpinge.Georgia ilipiga na majimbo ya Abkhazia na South ossetia yakachukuliwa kibabe na ilibaki kidogo tu jamaa wachukue na mji mkuu wenyewe wa Georgia pasipo mataifa mengine kuwaombea Georgia msamaha basi Georgia mpaka leo ingekuwa sehem ya Urusi.Bush mwenyewe alikaa tu kimya maana anajua jamaa ni kichwa ngumu wala hana utani hata kidogo
 
Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
5,784
2,000
Alikuwa anamuunga mkono au alikuwa anamuogopa?
katika dictionary ya Putin uwa hamna neno kumuogopa mtu, yeye akiamua la kwake basi kikubwa tu usimpinge.Georgia ilipiga na majimbo ya Abkhazia na South ossetia yakachukuliwa kibabe na ilibaki kidogo tu jamaa wachukue na mji mkuu wenyewe wa Georgia pasipo mataifa mengine kuwaombea Georgia msamaha basi Georgia mpaka leo ingekuwa sehem ya Urusi.Bush mwenyewe alikaa tu kimya maana anajua jamaa ni kichwa ngumu wala hana utani hata kidogo
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
1,820
2,000
Yani unatamka neno kuogopa liwe na mtu anaitwa Vladimir Vladimirovich Putin??
Mtu katoka KGB akiwa chief kabisa, kaishi kwenye siasa za Russia ambazo ni umafia mtupu aje kumuogopa Bush hiyo haiwezekani. Vita ya Georgia mwaka 2008 wakati Urusi anatumia nguvu nyingi na kuvamia Bush ndo alikuwa rais. Then NATO ilimtishia nyau lakini hakujali. Hata wakati anaichukua Crimea kipindi cha Obama NATO waliropoka tu hakuna kitu wamemfanya ukiachana na vikwazo vya kiuchumi
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,145
2,000
Bush alikuwa ni mjeda ndio maana alikuwa na ushawishi wa kuwaambia na kuwaaminisha Congress kuwa tusipovamia tutaporomoka kiuchumi lazima tuibe mafuta ya waarabu

Tofauti na huyu wa sasa ambae ni mfanyabiashara ambae ana miradi kila mahali especially Middle East na Israel ikiwemo

Niguse Ninuke ndio kauli ya Rouhani
 
Nkuba25

JF-Expert Member
Nov 18, 2015
901
1,000
For your record, Bush Jr hakuwai kuwa Askari.
Bush alikuwa ni mjeda ndio maana alikuwa na ushawishi wa kuwaambia na kuwaaminisha Congress kuwa tusipovamia tutaporomoka kiuchumi lazima tuibe mafuta ya waarabu

Tofauti na huyu wa sasa ambae ni mfanyabiashara ambae ana miradi kila mahali especially Middle East na Israel ikiwemo

Niguse Ninuke ndio kauli ya Rouhani
 
Nkuba25

JF-Expert Member
Nov 18, 2015
901
1,000
Kipindi hicho Russia alikuwa na matatizo mengi ukilinganisha na sasa kwa hiyo alikuwa bize kushughulikia matatizo ya nchi yake zaidi badala ya kuingilia mataifa mengine.
Umenena vyema kabisa.

Kuna kipindi baada ya kuanguka USSR na kutawaliwa na Boris Yetsin ambaye alikuwa mlevi, Russia ilipoteza ushawaishi kwenye meza ya kimataifa.

Kwa hiyo kazi kubwa aliyokuwa nayo Putin, Ni kuhakikisha Russia inarudi Tena kwenye ushawishi wa kimataifa.

Kwa hiyo kwa kipindi fulani tusingeweza kuisikia Russia Kama tuisikiavyo Sasa hivi.
 
Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
5,978
2,000
Bush alikuwa ni mjeda ndio maana alikuwa na ushawishi wa kuwaambia na kuwaaminisha Congress kuwa tusipovamia tutaporomoka kiuchumi lazima tuibe mafuta ya waarabu
Tofauti na huyu wa sasa ambae ni mfanyabiashara ambae ana miradi kila mahali especially Middle East na Israel ikiwemo
Niguse Ninuke ndio kauli ya Rouhani
Bush jr alikuwa CIA Boss hakuwahi kuwa mwanajeshi.....
 
Top Bottom