Punguza tui utie mchele

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,985
1,286
PUNGUZA TUI UTIE MCHELE.

Kobe hugeuka paka, kwa uchungu wa mwanawe,
Atoe sumu ka nyoka, kiasi asichezewe,
Kama tai ataruka, kwa makucha aparuwe,
Tua nasema jituwe, siku zako zimefika.

Nasema likinifika, hilo kwanza ulijuwe,
Nilo nayo nafutika, hata shari nifanyiwe,
Sikuponyi hilo shika, dawa lazima upewe,
Tua nasema jituwe, siku zako zimefika.

Naona wahangaika, utakacho upokewe,
Jasho lina kumwaika, waona maruweruwe,
Tafuta alokutwika, hilo zigo akutuwe,
Tua nasema jituwe, siku zako zimefika.

Ukingoni umefika, hino sakafu ujuwe.
Hupaoni pakushika, ghururi zina mwishowe,
Tahdabu na pulika, kiumbe usitiriwe,
Tua nasema jituwe, siku zako zimefika.

Dotto Rangimoto Chamchu (Njano5)
0622845394/0784845394 Morogoro
 

Attachments

  • kucha.jpg
    kucha.jpg
    7.6 KB · Views: 39
Mkuu nautafuta utenzi mmoja niliwahi usoma gazetini zamani...

ulikuwa unahusu mtu anamlilia Rais
kuna sehemu anasema
'niliemtuma kwako nae amenigeuka'
akimaanisha wabunge....
 
Mkuu nautafuta utenzi mmoja niliwahi usoma gazetini zamani...

ulikuwa unahusu mtu anamlilia Rais
kuna sehemu anasema
'niliemtuma kwako nae amenigeuka'
akimaanisha wabunge....
mkuu siujui huo utenzi, uliona katika gazeti gani??
 
Back
Top Bottom