Pumzika Baba

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,540
Reaction score
6,295
PUMZIKA KWA AMANI KIONGOZI NA MLEZI WETU KINGUNGE NGOMBARE MWIRU.
Tunabaki na faraja kuwa upo urithi uliotuachia,umetutangulia katika kipindi ambacho bado kuna mengi tulihitaji kujifunza kutokakwako, lakini yapo mengi zaidi tuliyojifunza kutoka kwako,Ukiwa unauguza majeraha ya kuumwa na Mbwa ulipokea taarifa ya huzuni ya kifo cha Mkeo,maumivu ni kama yalizidi mara kumi zaidi,natafakari juu ya hali ya majaribu mazito uliyopitia ndani ya muda mfupi na kwa karibu karibu, siwezi kuzisemea sana hisia za uchungu na huzuni ulizopata kwa namna yako na kwa upekee wako ila nayasema yote haya kwa kujitathmini Mimi kama binadamu mwenzako ningeyapitia hayo yote ningekuwa katika hali gani.
Muda mfupi wa sononeko na huzuni kubwa"naumia hasahasa na hisia ninazohisi ulipitia ndani ya muda mfupi,naiona furaha ya inayopingana na hali halisi ya ndani uliyojaribu kujenga tena muda mfupi baada ya kupatwa na madhila "ni Kama naona ulipokuwa ukiongea na watu waliokutembelea kabla ya kupatwa na mauti ulivyoulinda muonekano wake wa hisia za ndani usijioneshe kwa nje kama ulivyo ili kutowatia fadhaha na huzuni uliyokuwa umeibeba lakini napata hisia kali za mamba ulivyokuwa unajitathmini unapokuwa peke yako...jana niliandika andiko lenye kichwa "Baada ya yote ni maisha yako"naakisi namna ulivyokuwa ukijitathmini pale ulipokuwa peke yako (mengi siyajui juu ya tathmini binafsi ulizojifanyia ila ninachokifahamu ni kuwa yapo yaliyokuwa yakiendelea ulipokuwa peke yako )
Nimeanza kwa kusema yapo mengi uliyotuachia ya kujifunza kutokana na ukweli kuwa umeacha "alama kubwa na ya pekee"..nafahamu siyo yote tuliyoyaona kwa nje ndiyo yaliyokukamilisha ulivyo ila ninaafiki kuwa yapo uliyotaka tuyaone wote na tumeyaona.
Miongoni mwa alama uliyotuachia ni "Maisha ya upekee yanayoisimia misingi uliyoichagua"existential life"ninakubali Kuwait hukujipinga kutuonesha kile ulichotaka tukione kutoka kwako.
Wapo wanaoamini hukuwa na imani(dini)ila Mimi nina uhakika kuwa msingi wa maisha yako ulikuwa na kile ulichokiamini kuwa ni sahihi na kwa mlengo huo nakiona ni imani yako..ulijitendea Haki kwa kufuata kile ulichoona kinafaa licha ya misukumo mingi ya nje.
Ni kama uliweza kuitawala misukumo ya nje licha ya msukumo mkubwa wa nje.
Mungu aijalie familia wepesi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…