Proved: Halima Mdee alinena

Hilo lipo wazi hata dada wa Mbatia kupata ubunge wa EAst Africa
ndo maana kila nikimwangalia yule dada naona anafanana na mtu fulani ambaye namjua, sasa jina ndo likanipiga chenga kabisa, aiseeeeeeeeh !
 
cdm hakiendi na wakati wenzenu wanapanua demokrasi nyie ubinafsi2, hamfiki mcal4
 

Njaa mbaya ndugu yangu asikwambie mtu
 
Pia Mdee alisema mbatia ni 'chakula', sasa uki connect dots utaona JK anatekeleza maagizo ya cameron, kwamba watu kama kina James nao wapewe nafasi...

Hivi yule Mateo Quares yuko wapi siku hizi?
Mbatia kweli anahitaji mwingine au yule kazeeka!!
 
huyu mbatia aliwahi kuiwekea pingamizi CUF on favor of CCM ni kweli yametimia,kuishi kwingi kuona mengi ni mengi tutayaona tusubiri na baraza jipya lijalo.Mungu tubariki wote.
 
JAJI nimeipenda hiyo picha kwenye avatar yko,nimecheeakaa weeee mpaka basi.hebu i zoom iwekwe mbele ya gazet la kila siku watu wawe makini na ukimwi.duuuu
 

Kaka hapa umetema points. Well done.
 
hoja hapa sio watu hawataki Demokrasia kama unavyotaka tuamini. La hasha! Mbatia ni kiongozi wa chama cha NCCR Mageuzi. Chama ni itikadi ''Idiology'' CCM ina itikadi yake toka zamani hata kabla ya kuanzishwa kwa NCCR Mageuzi. NCCR Mageuzi ilianzishwa kwa sababu ilkuwa haikubaliani na itikadi ya CCM.

James Mbatia, akiwa M/Kiti wa NCCR Mageuzi alionekana kuunga Mkono sera zote za CCM na kuweka kando sera za chama chake. Sasa kama anakubaliana na sera za CCM, kwa nini alijiunga na NCCR Mageuzi. Jibu ni moja tu. Kufanya ukibaraka PURPET. Uteuzi wake kuwa Mbunge wa Viti Maalum kama alivyoteuliwa na Rais JK ni wa uwazi wa yale aliyoyasema Mheshimia Halima Mdee wa CDM na Mhe. David Kafulila wa NCCR Mageuzi.

Mapenzi ni Kikohozi kamwe hayawezi kufichika. Kwa maneno na matendo James Mbatia alishindwa kuficha mapenzi yake kwa CCM hadi jamii ikayaona baya na CCM pia imeshindwa kuficha mapenzi yake kwa Mbatia imeamua kuweka mambo hadharani. Wale wasiotaka kuuona ukweli huu wameamua kuwa vipofu makusudi kwa sababu wanazozijua wao au la upeo wao hauwawezeshi kuyaona yaliyofichika kidogo. Kundi hili la pili sina ugomvi nalo kwa sababu wakifunuliwa wataona na wataelewa, lakini kundi la pili ni hatari kwa kuwa ni wapotoshaji. Hawa hawana ukweli hugeukageuka kama bendera kufuata upepo.
Huweza kutetea hata uozo ili kujipendekeza. Lakini kibaya zaidi hata wanaowatetea ie Mbatia na JK wanawaona watu hawa kama mazuzu vile.
Kama Raisi angemteua Prof. Baregu, au mtu mwingine yeyote asiyewahi kuonyesha kujipendekeza kwa kusimamia sera za CCM, hoja ya kujenga demokrasia ingalieleweka. Kulinganisha Hillary Clington na Obama sio sahihi kwa sababu hawa wawili wako chama kimoja Demokrat, ingekuwa na mshiko kama kama Hillary angetoka chama cha Republican
 
ila hapo mbatia anatakiwa awe makini asije kuwa kama self alivyopotea kwenye siasa
 
Mwenyekiti wa upinzani upewapo ubunge na mkiti wa chama tawala ndo tatizo linaanzia hapo! Unaujasiri wa kumkosoa?
 
Jaji kwani Mbatia ni Mtani wako? Viti maalumu ni kwa wanawake tu,yeye ni Mbunge wa Kuteuliwa! Upoozi?
 
Dalili ya mvua ni mawingu.Na hii ndio moja ya sababu zinazodumaza maendeleo ya demokrasia hapa nchini.Sasa nimeamini maneno ya Mh.Mdee kwamba Mbatia anatumiwa na chama tawala ili kuua upinzani nchini.Mungu hamfichi mnafiki.Siku zake zinahesabika.

Mkuu, labda JK kafikiri akimchagua, ataonekana anawajali sana wapinzani!! Kumbe sivyo, kanifanya nikumbuke jinsi alivo2miwa 2006 kuwawekea pingamizi wagombea wa cuf zanzibar na hivo kutolewa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge. Ndo ikaibuka ishu ya kura za maruhani.
 
Jamani muwe wakweli wengine ikiwa kwenu hamsemi,mbona alipoteuliwa prf.WESIGA BAREGU Kwenye tume ya katiba hamkusema pandikizi?na zaidi ya yote Baregu akamsifia jk nkwa uteuzi mzuri
 
kwani Mbatia analiwa na nani?

mtujuze vinginevyo ni tetesi
 
Judas mkubwa,amewasaliti watanzania, bara na visiwani. Amesalilti chama chake, hadi walezi wake. Wonder how much he was paid kukana utu wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…