Prove me wrong;Ustaraabu ulianzia middle East

Pure_sapiens

JF-Expert Member
Dec 25, 2016
2,197
2,025
Habari zenu wandugu.
Kama unafuatilia siasa za kimataifa nadhani hukipitwa na kauli ya Rais wa Ufaransa ya kuwakejeli waafrika.Waafrika kuwa tunazaana hovyo na hatuna ustaarabu.

Pia hata Donald Trump naye alifanya vitendo vya dharau kwa waafrika kwa kitendo cha kutoka nje ya mkutano na kiti chake kukaliwa na mwanawe. Vitendo hivyo si katika ustaraabu.

KUMBE USTARAABU SI ASILI YAO.
Kwa sisi waafrika tunaona kuwa wazungu ni wastaarabu lakini ustaarabu haukuanzia kwao.Jamii zilizostarabika hazikuanza ulaya wala amerika bali zilianzia middle east.

cha utawala Makedonia ndicho kipindi ambacho ustaarabu ulinza.Ustaarabu wa kiyunani ulianza kipindi cha 338k.Kipindi cha fikra na ustaarabu wa kiyunani uliitwa"HELLENIC".

Naomba kuwasilisha kwa majadiliano zaidi.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Unajidanganya

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Habari zenu wandugu.
Kama unafuatilia siasa za kimataifa nadhani hukipitwa na kauli ya Rais wa Ufaransa ya kuwakejeli waafrika.Waafrika kuwa tunazaana hovyo na hatuna ustaarabu.Pia hata Donald Trump naye alifanya vitendo vya dharau kwa waafrika kwa kitendo cha kutoka nje ya mkutano na kiti chake kukaliwa na mwanawe.Vitendo hivyo si katika ustaraabu.
KUMBE USTARAABU SI ASILI YAO.
Kwa sisi waafrika tunaona kuwa wazungu ni wastaarabu lakini ustaarabu haukuanzia kwao.Jamii zilizostarabika hazikuanza ulaya wala amerika bali zilianzia middle east.Kipindi cha utawala Makedonia ndicho kipindi ambacho ustaarabu ulinza.Ustaarabu wa kiyunani ulianza kipindi cha 338k.Kipindi cha fikra na ustaarabu wa kiyunani uliitwa"HELLENIC".
Naomba kuwasilisha kwa majadiliano zaidi.

Post sent using JamiiForums mobile app
Kabla ya utawala wa pharao kulikua na wa waafrika, fanya utafiti
 
Ustaarabu kuanzia kwa Waarabu si tabu.

Kwani sisi tutafika kwa ustaafrika.

Pia, katika mbio Usain Bolt anaweza kujuachia wewe uanze, halafu yeye akashinda.

Sent from my Kimulimuli
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ustaarabu kuanzia kwa Waarabu si tabu.

Kwani sisi tutafika kwa ustaafrika.

Pia, katika mbio Usain Bolt anaweza kujuachia wewe uanze, halafu yeye akashinda.

Sent from my Kimulimuli
ulichosema ni kweli kabisa lakini middle east ya kale kulikuwa na waafrika so wazungu walichukuwa ustaarabu kutoka kwetu

Post sent using JamiiForums mobile app
 
ulichosema ni kweli kabisa lakini middle east ya kale kulikuwa na waafrika so wazungu walichukuwa ustaarabu kutoka kwetu

Post sent using JamiiForums mobile app
Wahenga walisema "Mavi ya kale hayanuki".

Wakasisitiza zaidi "Mla mla leo, mla jana kala nini?".

Sent from my Kimulimuli
 
I prove u wrong: ustaarabu kwa kiingereza huitwa civilization, ukisoma historia mbali mbali utakuta kila taifa au bala lina ustaarabu wake.
 
Mleta mada upo sahihi kabisa..angalia hii vdo clip hapa chini.
 

Attachments

  • VID-20160219-WA0015.mp4
    4 MB · Views: 25
Baadhi ya Waafrika ni watu wa ajabu sana! Wanapenda kuikuza historia potofu, inayowafanya waafrika kuonekana kama si watu kamili, hawajui chochote na hawakuwa na historia yenye ustawi kwa jamii yao ya kale! Hii ni historia iliyoandikwa na watu wasio waafrika. Lengo lao kutaka kuitawala jamii nyingine kifikra.

Kila jamii hapa Duniani ilikuwa na ustawi na maendeleo yake na mfumo kamili wa kujiendesha! Ndio maana tupo. Kama tungekuwa ni jamii yenye mapungufu, tusingeweza kuwepo katika uso wa dunia.

Ni upumbavu wa kiakili kutafuta kuhalalisha kuwa jamii moja ilikuwa bora zaidi ya nyingine! Jamii zote zilikuwa sawa, na kila moja ilikuwa na ustawi na maendeleo yake kulingana na mahitaji ya wakati na mazingira.

Ninarudia tena, ni upumbavu wa kiakili kutaka kuhalalisha kuwa, jamii moja ilikuwa bora kuliko jamii nyingine. Jamii ya wafugaji haiwezi kuwa bora zaidi ya jamiii ya wakulima; jamii ya wakulima haiwezi kuwa bora zaidi ya jamii ya wavuvi; na jamii ya wafugaji, wakulima ama wavuvi haiwezi kuwa bora zaidi ya jamii ya wawindaji. Haya ni mazingira tofauti, na mahitaji tofauti kwa wakati tofauti.

Hivyo, jamii ya waarabu kama unavyotaka kuhalalisha hoja yako, haikuwa bora zaidi ya jamii ya wachina, waafrika, wahindi na hata wazungu. Hilo linawezekana tu kwa mazuzu wa akili wasiotaka kujielimisha na kujua histori ya nzuri ya jamii yao. Lakini kutaka kulinganisha ustawi wa jamii moja kwa kutegemea historia ya jamii nyingine, huoni upumbavu wa kiakili uliopindukia mipaka.

Hiyo nisawa na kujifunza historia ya Tanzania kwa kusoma historia iliyoandikwa na mtu asiye mtanzania, na hajawahi hata kufika au kuishi au kuwaona watanzani! Utaishia kupoteza hata kidogo ulichokijua kuhusu Tanzania.

Kwa hiyo, jamii moja haiwezi kuwa kipimo cha ustawi na maendeleo kwa jamii zingine. Mwisho wake ni kuishia kutukuza jamii nyingine na kudharau jamii yako. Utumwa uliovuka mipaka.
 
Nafikiri umechukua maana tofauti ya neno ustaarabu,ni neno pana kiasi kuna maana nyingi pia, ustaarabu au civilization ni mfumo wa kiutamaduni wa maisha ya mwanadam ambapo watu waliweza kugundua njia tofauti tofauti za kimaendeleo kijamii, kiteknolojia, kisiasa na kiuchumi, mfano ufuaji chuma, ujenz wa majengo, uandishi, matibabu, democracy na vingine vingi.lakin pia ustaarabu umegawanyika kadir ya vipindi vikiwemo ancient, medieval na modern. Pia kila sehemu inasifika na ustaarabu wake ndio maana kuna Chinese civilization ambayo ni kongwe zaid na haipo middle east, Egyptian civilization, mesoamerican civilization, western civilization na nyingine nyingi. So jaribu kuangalia vizuri kuwa ustaarabu haukuanzia middle east bali ulikuwepo toka miaka ming na maeneo mengi. Ingefaa ungesoma kitabu flan nilisoma wakati nasoma advance miaka hyo kinaitwa (world history connect today.)
 
Back
Top Bottom