Propaganda zitapelela nchi pabaya.

Propaganda zitapelela nchi pabaya.

GHULA

Member
Joined
Mar 3, 2013
Posts
77
Reaction score
66
Kinachoripotiwa kuhusu Samson Mwigamba leo na mambo ya Mkutano wa Arusha, Waandishi na wachangiaji tutafute ukweli bila kuegemea upande kwa sababu ya hisia za kisiasa au kushabikia Propaganda, Mwigamba amekuwaje mbaya sana kwa Chadema baada tu kumaliza kusoma ripoti ya mkoa na kupigiwa makofi ya kupongezwa? Ilikuwaje akaanza kuposti vitu tofauti na vile alivyovisoma wakati yupo kwenye kikao halali ambacho angeweza kuyasema? Katiba anayodai imechomolewa vipengele mbona ndiyo iliyomweka madarakani? Yeye ni Mjumbe wa Kamati Kuu, yeye ni Mjumbe wa baraza kuu, je haya aliyasema wapi tangu 2006? Mbona asiyaseme kwenye vikao vyote hivyo ambavyo amekuwa akihudhuria?, Suala la Mtu kusema alipigwa jiwe, kwanza ni kuharibu jina la Hoteli ya watu, ukumbi wa ndani ya hoteli nani ataingia na jiwe hotelini? kwamba mtu alipigwa jiwe akaanguka akanusurika kifo wakati hajatibiwa hata katika zahanati tukaona taarifa. Wanaoandika hizi habari watuambie ukweli, isiwe kama propaganda zingine tunaharibu nchi.
 
wachochezi wamechoka kuishi kwa utulivu na uvumilivu. Mungu ibarki Tanzania na watu wake
 
Back
Top Bottom