Mimi mwenyewe nawashangaa ccm maandamano ya chadema sehemu zote za kanda ya ziwa yamefanyika kwa amani bila vurugu zozote. Ukweli ni kwamba zama za ccm ziko mbioni kutoweka, hoja iliyopo mbele ni hali ngumu ya maisha, mfumuko wa bei, malipo ya dowans, mgao wa umeme n.k. CCM wanatakiwa kutimiza madai hayo siyo kukomalia uvunjifu wa amani. Wanachofanya chadema ni kutoa elimu ya uraia kwa wananchi kitu ambacho ni kazi ya chama chochote cha kisiasa. CCM hawataki wananchi wafahamu ni jinsi gani nchi inatafunwa na wajanja wachache kwa sababu wanajua mtaji wao ni ujinga na umasikini wa watanzania kwa maana hiyo watanzania wakipata elimu ya uraia watawatosa katika uchaguzi ujao. Nawasilisha.........