The Consult
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 220
- 252
Kuongoza/kusimamia mradi (managing a project) ni tofauti na kuongoza idara katika kampuni au ,taasisi.
Mradi siku zote huja na bidhaa au huduma mpya na ya kipekee (unique) katika eneo husika, hivyo hata mchakato wa kuleta bidhaa/huduma hiyo huwa si wenye kutabirika sana (uncertain process) Kwa maana hii kiongozi wa mradi (Project leader) hufanya kazi katika mazingira yasiyotabirika (environments of constant uncertainty)
Katika mradi, kiongozi (Project leader) husimamia na kuwaongoza watu wenye utofauti katika; ujuzi (skills), uasili (background), tabia ya ufanyaji wa kazi ( working habit), maadili (ethics) n.k. Mafanikio katika utekelezaji wa mradi kwa kiasi kikubwa hutegemea ushirikiano baina ya watu hawa, na upatikanaji wa ushirikiano huwa ni changamoto kubwa kwa viongozi wa miradi. Hivyo kiongozi wa mradi hana budi kuwa na mbinu za kuwaunganisha watu hawa wafanye kazi kama timu japokuwa hana mamalaka juu yao (He/she doesn't have direct control)
Kutokana na kutokuwa na mamlaka juu ya timu anayoiongoza, kiongozi wa mradi hupaswa kutegemea na kutumia mbinu ya ushawishi (influence & persuasion) ili kupata ushirikiano ambao utafanikisha utekelezaji wa mradi husika. Mbali na sifa ya ushawishi; kiongozi wa mradi hupaswa kuwa na uwezo wa kuijengea timu yake ya mradi hamasa (motivation).
Kwa kiasi kikubwa, msimamizi wa mradi (Project leader) hupaswa;
- Kuwa na fikra pana (Thinks like a generalist)
- Kujitambua (Self-aware)
- Kuwa muwazi na mwenye kuingilika (Open and accessible)
- Kuwa na ushawishi (Persuasive)
- Kuwa na ufahamu juu ya siasa (Politically astute)
- Kuwa muangalifu juu ya kila kinachomzunguuka
The Consult; +255 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania
Kwa huduma za;
- Uandishi wa michanganuo ya miradi (Project proposals) na mipango mkakati (Strategic plans)
- Utoaji wa semina katika maeneo ya Usimamizi wa Miradi (Project management) na usukaji wa mikakati (Strategic planning).