Zakumi,
Mkuu wangu haya maswala ya kubishana bila kutumia fact na kuzichambua hayana mpango.. najua wewe msomi mzuri sana na umeelewa vizuri nilichoandika..
Tatizo ni sisi binadamu na uongozi wake sio ukubwa wa nchi..U know it isipokuwa sasa labda unatumia siasa..
Swala la Rwanda na maendeleo yake huwezi kuliweka ktk mjadala huu kwa sababu kuna nchi ndogo nyingi sana Afrika kama Burundi jirani yao tu hazifanyi vizuri kama wao wakati vita yao ilikuwa ndogo na ya muda mfupi sana. Ukitazama upande wa West Afrika kuna lundo la nchi ndogo ndogo mara tano ya Tanzania (i.e Guinea Bissau) lakini zote maskini kuliko zote duniani ukijumlisha na visiwa vya Haiti huko Carribean...Zote tumeona matatizo ya uongozi wa nchi hizo ktk utawala bora..
Nakuomba itazame tena ramani ya Afrika kisha nambie kwa nini nchi hizo maskini..
Ukizungumzia Ulaya, hapo tayario mwenyewe umeisha toa jibu ULAYA! maendeleo yao yametokana na Uongozi pamoja na watu wake, sio ukubwa wa nchi kwani zipo nchi maskini pia zenye majimbo wakati Canada ambayo ni kubwa kwa kila jimbo kuliko Tanzania na nchi hizo za Ulaya imeendelea zaidi..
Unaposema Angola wamebarikiwa resources nyingi una maana gani mkuu wangu!..ikiwa swala ni baraka za resources iweje Kongo wamebakia nyuma! Hivi baraka zote tulizopewa sisi mnashindwa kuzitambua wakati tuna kila madini nchini, gas, maji masafi (Lakes) na ardhi yenye rutuba naweza sema kuliko nchi ZOTE za Afrika..Jamani kuitumia Rwanda na udogo wake huwezi kuona kuwa ni aibu kubwa sana kwetu kusingizia udogo wa nchi hali ambayo imewaingiza wao ktk vita vya wenbyewe kwa wenyewe.. na bado haitakwisha iko siku litaibuka tena maanake hoja ya mgao waardhi ndogo bado kabisa haijapatiwa ufumbuzi..
Anyway, sasa mkuu, kwa maneno yako hayo nadhani hapa ndipo pa kuanzia.. yaani inaonyesha wazi kwamba Watanzania hatufahamu baraka tuliyokuwa nayo...Tukifahamu hilo kwanza kisha tukajiuliza kwa nini hatupigi hatua mbele kimaendeleo zaidi ya kuwa gurudumu la nyuma linalofuata tutaweza jenga hoja maana kujiuliza sisi wenyewe badala ya kusingizia ardhi iliyokuwepo toka dunia iumbwe..
Miaka ya 70 na 80 tulikuwa chini ya Ujamaa siasa mbovu kiuchumi yet tulikuwa ranked 120's leo hii ndani ya Ubepari na opportunities zote zilizopo tumesimama 150's, mkuu kama sisi sio tairi la nyuma ni kitu gani!
Bado unafikiria kweli ni ukubwa wa nchi!...
Mkandara mimi sio msomi. Shule nilipitia kwa bahati mbaya tu kwa sababu ya kutaka visa ya kuja mtoni.
Na vilevile watanzania hacheni uongo wa kusema kuwa mlipiga maendeleo katika miaka ya 70 na 80.
Hakuna maendeleo yoyote yaliopatikana katika miaka ya 70 na 80 bila kutegemea misaada, grants na mikopo. Maendeleo uliyoyaona wewe hayakutegemea mapato halisi ya Tanzania.
Hivyo Tanzania kuwa katika nafasi ya 120 miaka ilikuwa ni uongo uliokithiri. Maendeleo ni lazima uweze kuya-sustain kwa mapato yako mwenyewe au mikopo ambayo unaweza kulipa bila kuathiri ubora wa maisha yako. Tanzania haijawahi kufanya hivyo hata siku moja.
Kuhusu niliyosema huo ni msimamo wangu. Na sasa ngoja ni fanunue. homogeneous ya jamii ni moja ya masharti ya maendeleo au national building. Mataifa ya Africa ni legacy za ukoloni na mipaka ya mataifa hayo ni ramani za kijiografia sio identity ya watu waishio ndani ya nchi hizo.
Tanganyika ni eneo la kijiografia lakini waishio ndani sio watanganyika ni wamakonde, wasukuma, wazigua n.k
Kenya ni eneo la kijiografia tu lakini ndani wamo wakikuyu, wajaluo, wakamba n.k
Hata hizo nchi ndogo za Afrika magharibi zinakabiliwa na matatizo hayo. Kwamba lipo taifa linalotambulika kijiografia lakini ndani watu hawafanani.
Matatizo yaliopo ni kuwa watu hamtaki kuambiana ukweli. Labda tukiambiana tunaweza kupata ufumbuzi wa matatizo yetu na kuelewana.
Mimi na wewe Mkandara tunafafana ngozi tu lakini mambo mengi tupo tofauti. Mimi na profesa Mbilinyi hatufanani kabisa; hata huko kwao sitaki kwenda. Sasa unapokuja ku-impose values zako kwangu, mimi sikuelewi hata kidogo.
Angalia mjadiliano wa IOC peke yake ulivyovuta nchi. Mwislamu atakupa sababu nyingi za kujiunga. Na mkristo atakupa sababu nyingi za kutojiunga, mojawapo ikiwemo national unity. Ni national unity gani kila mtu anakuwa suspicious na mwenzake.