Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Anaitwa Profesa Makame Mbarawa, alipewa wizara moja halafu wakubwa juu kabisa wakagundua kuwa alikopelekwa siko kwenye anga zake. Wakampeleka kwenye maeneo yake ya kujidai, huyu ni msomi aliyesomea zile nchini za kirusi. Akikutana na wenzake waliovaa makoti wakati wa ile baridi ya January na February, lazima atasalimiana nao kwa kirusi huku akisema "kak dela drug moi", na hao atakaowasalimia watamjibu "vsyo narmana a kak zhizni idiot?".
Hilo jina Makame Mbarawa kama mtu anayo notebook yake basi aliandike halafu aitunze vizuri hiyo notebook kama ushahidi. Binadamu hupanga lakini Mungu ndio mwenye mamlaka ya mwisho kwa maana ya kuamua kama hiyo mipango yetu ifanikiwe au isifanikiwe. Lolote linaweza kutokea, lakini ikiwa mambo yatakwenda barabara, hilo jina litakuwa kubwa sana miaka kadhaa ijayo.
Huyu bwana mkubwa atakuja kubebwa na elimu yake, uwezo wa kazi pamoja na matakwa ya tamaduni za uongozi wa nchi hii, ambazo ni desturi za kiutawala za chama kikongwe nchini, lakini hapa naongelea miaka ijayo. Kumbuka hili jina Makame Mbarawa, halafu Mungu akitupa uhai waungwana mtakuja kuniambia kwa nini leo hii ninawaambia mlikumbuke hili jina.