Profesa Lipumba aomba kutengua kujiuzulu kwake Uenyekiti CUF

Lipumba amekwisha kufilisika kisiasa. Kilichobakia sasa ni mihemuko ya mashabiki wake. Uongozi wenye hekima hauwezi kuruhusu arejee kwenye nafasi yake aliyoacha kwa ridhaa yake mwenye alipokua akifuatilia masilahi binafsi. Waliomdanganya wamsaidie!
 
Msaliti na Ndumi la kuwili mkubwa huyu, nitashangaa sana CUF kupokea hili KAPI


kAMANDA ANAYESALITI WENZIE WAKATI WA MAPAMBANO STAHILI YAKE NI RISASI TU-HICHO NDICHO KINACHOMSTAHILI HUYU 'LIPUMBAVU', AENDE ALIPOKIMBILIA KIPINDI KILE CHA MAPAMBANO, HAKUNA CHAKE ALICHOSAHAU HUKU!!
 
MTATIRO.jpg

NGOJA NIWAELEZE UKWELI!
Kama mzee wetu anao washauri, wamwambie kuwa "DALILI ZA MVUA NI MAWINGU". Na kwamba, NGOMA ivumapo sana hupasuka na tena ajulishwe kuwa VITANI hakuna michezo ya KUJIFICHA na KUONEKANA baadaye, jana niliwaambia kuwa najua CUF inao watu makini wanaojua nini haki ya PROFESA LIPUMBA na nini haki ya CUF kama chama.
Kwa wale ambao hawakuelewa ujumbe wangu wa jana nilikuwa namaanisha viongozi wa CUF watakuwa upande wa chama, hawatafuata matakwa ya mtu, na dalili zimeanza kuwa hivyo. Mwisho wa siku mshindi wa mchezo huu ni CHAMA na WANACHAMA wenye UTII na COMMITMENT kwa chama chao, na siyo MTU!
Kuna watu nasikia wanasema WATAGAWANA MBAO, ukweli ni kuwa CUF ni taasisi imara na haiwezi kuwa na MBAO za kugawana. Kutakuwa na machaguo mawili tu, aidha kuondoka na mtu au kubaki na chama, wale watakaobaki na chama watabaki na mbao zote, na wale watakaoondoka na mtu hawatandoka na hata kipande cha ubao - kwa sababu mchezo huu hautahitaji hasira.
Siasa ni maisha halisi ya watu, vyama vikiruhusu zigeuke kuwa mchezo wa KOMBOLELA, zitakosa maana na hapa lazima ieleweke, kwamba kuna mambo ambayo vyama vya upinzani vikiyaruhusu yaendelee kutendeka, vitakuwa vinafanya ujinga wa kiwango cha PhD na Uwendawazimu wa Kiwango cha MWENDOKASI!
Profesa Lipumba ambaye kila mtu anamheshimu sana, apishe kwenye uongozi ili chama kijiandalie ZAMA mpya. Nawarejesha kwenye nukuu yangu ya mwaka jana wakati anajiuzulu, kwamba "Kamanda wa vita akiuawa katikati ya vita, siyo muda wa kuanza kulia na kuomboleza, siyo muda wa kulaumiana, anatafutwa askari mwingine na kutwaa bunduki yake, mapambano yanaendelea mbele".
Ninaamini kuwa, CUF inao watu wenye sifa za kuwa wenyeviti wa chama na tena kisiasa wapo watu bora sana. Chama kisiogope kufanya maamuzi sahihi kwa ajili yake na siyo kwa ajili ya mtu.
Na iwe fundisho kwa wanasiasa kuwa HISIA za wafuasi wa vyama hazichezewi, na iwe FUNDISHO kwa viongozi wa kisiasa kwamba MISIMAMO na KUTOYUMBA ni wajibu wao usiokwepeka.
Katika mgogoro huu wa kutengenezwa makusudi, wanachama imara wanajua wajibu wao, wasimame upande wa chama, wasimame upande wa taasisi, maana taasisi itakuwepo siku zote. Mtu na watu watapita haraka na kunyauka kama maua.
Namshauri Prof. Lipumba, kwa namna yoyote ile, asikubali kutumikia matakwa ya kundi lolote lile, iwe ndani ya chama au nje ya chama. Asikubali kuwa sehemu ya kuanzisha mgogoro na vurumai kubwa ndani ya chama, asikubali kuwa chanzo cha kuleta sintofahamu kama hii, namtambua Mwenyekiti wangu kama mtu makini na muumini safi wa dini ya kiislamu na huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani, hebu na ajitafakari upya ikiwa NIA yake ni salama kwa ajili ya wanachama wa CUF na nchi yetu.
Binafsi nisingelipenda kuona mgogoro mwingine mkubwa CUF, ambao matokeo yake sote tunayajua, kwamba chama ndicho kitashinda na kitabaki salama salmini, na kwamba watu wachache ndiyo wataumia na kufedheheka, akiwemo mtu anayeheshimiwa sana na aliyewahi kushiriki kukijenga chama hiki kwa nguvu zake na akili zake zote.
Mtatiro J
 
Alikuwa mshauri wa uchumi wa Rais (wakati huo) Mzee Mwinyi.
Uchumi uliporomoka, mfumuko wa bei ukawa juu, nchi ikawa hata haikopesheki, pesa zikachapwa za tarakimu kubwa, serikali ikasitisha ajira nyingi kwa wahitimu wa vyuo vikuu nk.
Ndiyo huyu.

Asante kwa ufafanuzi mkuu.
 
Nani mkweli? Wale walimwita jamaa fisadi Lakini mwisho wakawa nyuma yake na sifa zote, mwingine alituaminisha atakuwa rais wa watanzania wote bila kujali vyama vyao, sasa umeona anayofanya? Nchi hii ingekuwa ya kifalme ni bora kabisa tungejua moja tu, kama kwa mswati tu
Mkuu yaani ukiwaza siasa zetu unaweza utokomee porini tu ukaishi kama muhadzabe!! ni ujinga mtupu
 
ama kweli siasa za tanzania zina vioja sana
tungekuwa na lile daftari la kuweka saini kwa matukio ya kushangaza tungemwita mh. lipumba aweke saini yake maana ni kali ya mwaka isiyosahaulika kwenye ulimwengu wa siasa
 
hakuna siasa nzuri kama kutazama maisha yako na family yako tu hiyo ndio inalipa sana
ni kweli mkuu mimi sitaki wala kushabikia siasa..nipo zangu huku Kondoa naimarisha kilimo cha dengu na mbaazi kwa sasa ni "hot cake" wahindi wanazifuata shambani bei unapanga mwenyewe..hizo siasa zenu za matukio mi nishaachana nazo
 
ni kweli mkuu mimi sitaki wala kushabikia siasa..nipo zangu huku Kondoa naimarisha kilimo cha dengu na mbaazi kwa sasa ni "hot cake" wahindi wanazifuata shambani bei unapanga mwenyewe..hizo siasa zenu za matukio mi nishaachana nazo

Dah mkuu tuwasiliane mimi nahitaji kuja kulima alizeti ntakucheki pm tubadilishane namba,siasa tuwaachie wenyewe
 
GTs mpo? Fuatilieni na mng'amue hapa:

Kijijini Kwendambele kulikuwa na mkazi na mfugasamaki maarufu. Aliitwa Mzee Sabuni. Mzee huyu alikuwa anafuga samaki aina ya kambale kwa chakula na biashara. Mzee huyu alinyanyasika sana na kambale wake.

Kila alipowahitaji kambale wake kwa chakula au biashara,kambale wale walijificha kwelikweli chini kabisa matopeni. Hata wakivutiwa na chakula,hawakuwa wakijitokeza. Hitaji la chakula na biashara linapokwisha,kambale walijitokeza waziwazi wakiwa wamenona huku Mzee Sabuni akinuna.

Mchezo ukawa ndiyo huo. Mzee Sabuni,kutokana na kutoyaona matunda ya ufugaji wake,akafanya uamuzi mgumu. Anajaza vifusi bwawa zima na kumaliza kadhia ile. Kambale wakaipandika freshi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mwanza)
 
Back
Top Bottom