Decree Holder
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 2,559
- 3,745
Wanajamvi salaam!
Naomba Ku declare interest kuwa mimi ni miongoni mwa watu wanaomkubali sana waziri mpya wa katiba na sheria Profesa Palamagamba Kabudi. Licha ya hayo baada ya kuteuliwa kwenye nafasi yake ya uwaziri na kumsikiliza akiwa bungeni nimethibitisha mambo niliyokuwa nikiambiwa kumhusu Profesa huyu mkongwe kutoka kitivo cha sheria pale UDSM.
Profesa unatakiwa ujirekebishe unajiamini mno, unamajigambo na kujiona unajua kuliko mtu mwingine yeyote, na kama ukiendelea hivyo bunge na watanzania watakuchoka ndani ya muda mfupi na unaweza ukavurunda katika wizara hiyo zaidi ya Mawaziri waliokutangulia hususani Mwakyembe!
Ndugu wanajamvi simchukii Profesa Kabudi nina circumstantial evidence kuhusu nalolizungumza na ninaweka hapa scenario kadhaa kuthibitisha hoja yangu juu ya majigambo ya Profesa Kabudi.
1. Profesa Palamagamba Kabudi alifeli mara kadhaa mtihani wa bar exams ambao ilikuwa ni lazima mwanasheria aufanye ili awe wakili kipindi hicho kabla ya law school kuanzishwa. Baada ya kufeli mtihani huo wa bar exams mara kadhaa Profesa Kabudi alitoa maneno ya majigambo dhidi ya watahini wa bar exams ambao wengi wao walikuwa wanafunzi wake aliowahi kuwafundisha. Profesa Kabudi alidai kwamba yeye anajua zaidi yao hivyo wanamfelisha makusudi hivyo hata kama wanamfelisha wajue tu kwamba yeye anawazidi kila kitu na ni mwalimu wao. Baada ya majigambo hayo Profesa Kabudi alipewa uwakili wa viti maalumu kwenye sahani (honorary advocate).
2. Profesa Kabudi amesikika mara kadhaa akijigamba kwa wanafunzi wake kuhusu uwezo wa wanasheria wengine na hasa Tundu Lissu, huku akijisifu kuwa wanasheria wenye first class UDSM wapo wanne tu na wengine si kitu si chochote.
3. Profesa Kabudi aliwahi kujigamba na kumdharau Profesa Shivji kuwa hajui kitu kwenye maswala ya katiba hivyo akae kimya akaenda mbali zaidi na kusema wengine (akina shivji) wamesomea uprofesa wa sheria za ardhi wanajifanya waongeaji wa maswala ya katiba.
4. Profesa Kabudi aliwahi kudharau bunge maalumu la katiba na kuliita la Wapumbavu kwenye mchakato wa bunge la katiba huku akijiita yeye mjinga hivyo anaweza kuelimika.
5. Ushahidi mwingine ni jinsi Profesa huyu anavyojibu maswali bungeni kwa njia ya lecture akiwachukulia wabunge kama wanafunzi wa sheria huku akijionesha kama yeye ndiyo anajua sheria bunge zima.
6. Kitendo cha Profesa Kabudi kulidanganya bunge kwa kusema Uingereza haina katiba ni ishara sasa ameshadharau mhimili huo na watanzania wote. Utasemaje Uingereza haina katiba katika dunia ya sasa ya sheria katiba is not defined in that narrow sense anymore.
Wanajamvi Mheshimiwa Kabudi kama ataendelea kujigamba na kuwaona wengine si kitu atawachosha watu mapema na huenda akaiona kazi ya uwaziri kuwa ngumu zaidi anaweza kuvurunda kwani anaweza fika hatua asikubali ushauri. Profesa Kabudi zingatia taaluma heshimu wengine huna hati miliki ya sheria kuna wanasheria wengi wazuri wametulia usijione wewe ndiyo wewe ndani ya bunge na serikali. Kumbuka avumaye baharini papa kumbe wengine wapo, pia ajionaye amesimama aangalie asianguke